Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kazi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kazi-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 20 Agosti 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake

Katika mkondo wa sasa, kila mtu anayempenda Mungu kwa kweli ana fursa ya kukamilishwa na Yeye. Bila kujali kama yeye ni kijana au mzee, mradi tu anatazamia kwa hamu kumtii Mungu na kumheshimu Yeye, wataweza kukamilishwa na Yeye. Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi zao tofauti. Mradi tu umefanya yote kwa nguvu yako na kuitii kazi ya Mungu utakuwa na uwezo wa kukamilishwa na Yeye. Kwa sasa hakuna hata mmoja wenu aliye mkamilifu.

Jumamosi, 27 Julai 2019

1. Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli,

Sura ya 2 Lazima Ujue Ukweli wa Majina ya Mungu

1. Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Je, Jina la Yesu "Mungu pamoja nasi," linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru!

Jumamosi, 20 Julai 2019

Maisha ya Ushindi | 72. Ndio Nimeanza Tu Kutembea Njia Sahihi ya Uzima

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ushuhuda,

Maisha ya Ushindi | 72. Ndio Nimeanza Tu Kutembea Njia Sahihi ya Uzima

Shi Han Mkoa wa Hebei


Nilizaliwa kwa familia maskini ya wakulima. Nimekuwa mwenye busara tangu utotoni, ikimaanisha sijawahi kupigana na watoto wengine na niliwatii wazazi wangu, jambo lililonifanya “msichana mzuri” wa kawaida machoni mwa watu wazima. Wazazi wengine wote walikuwa na wivu sana kwa wazazi wangu, wakisema kuwa walikuwa na bahati kuwa na binti mzuri hivyo. Na hivi tu, nilikua kila siku nikisikiliza sifa kutoka kwa watu waliokuwa karibu nami. Nilipokuwa katika shule ya asili, rekodi yangu ya kitaaluma ilikuwa nzuri hasa, na daima nilipata nafasi ya kwanza katika mitihani.

Jumamosi, 18 Mei 2019



Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Wale wasiofahamu hatua tatu za kazi watakosa kuelewa njia mbalimbali na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu; wale wanaoshikilia tu imara mafundisho ya dini yanayosalia kutoka katika hatua moja ya kazi ni watu wanaomwekea Mungu mipaka kwa mafundisho ya dini, na wale ambao imani yao kwa Mungu haina udhahiri na uhakika. Watu kama hao kamwe hawawezi kupokea wokovu wa Mungu.”

Yaliyopendekezwa: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"
Tufuate: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Jumapili, 5 Mei 2019

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | 31. Mawazo Kuhusu Kubadilishwa

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | 31. Mawazo Kuhusu Kubadilishwa

Yi Ran Mji wa Laiwu , Mkoa wa Shandong
Wakati fulani awali, kwa sababu yangu kutoelewa kanuni iliyotumiwa na kanisa ya masahihisho ya wafanyakazi wa kanisa, wakati kanisa lilibadilisha kiongozi, dhana iliibuka ndani yangu. Kutoka kwa kile nilichoweza kuona, dada aliyebadilishwa alikuwa mzuri sana kwa kupokea na kushirikiana ukweli, na aliweza kuwa wazi juu ya maonyesho yake ya upotovu. Kwa hiyo sikuweza kujua asilani jinsi mtu fulani aliyetafuta ukweli sana angeweza kubadilishwa.

Jumatatu, 15 Aprili 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 26

Kutoka kwa maneno yote yaliyonenwa na Mungu, inaweza kuonekana kwamba siku ya Mungu inakaribia kila siku inapopita. Ni kama kwamba siku hii iko mbele ya macho ya watu, kama kwamba itafika kesho. Hivyo, baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu wote wanajawa na hofu, na pia wana hisia kiasi fulani ya ukiwa wa dunia. Ni kama kwamba, jinsi majani yanavyoanguka na manyunyu kushuka, watu wote wametoweka wasionekane tena, kama kwamba wote wameondolewa kabisa kutoka duniani.

Jumamosi, 13 Aprili 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 1

Kama tu Mungu alivyosema, “Hakuna anayeweza kuelewa mzizi wa maneno Yangu, wala kusudi la maneno haya.” Kama Isingekuwa uongozi wa Roho wa Mungu, kama isingekuwa kwa majilio ya maneno Yake, wote wangeangamia chini ya kuadibu Kwake. Ni kwa nini Mungu humjaribu mwanadamu kwa muda mrefu hivyo? Na kwa muda mrefu kama miezi mitano? Hili ndilo wazo la kulenga la ushirika wetu na vilevile wazo kuu katika hekima ya Mungu.

Jumanne, 9 Aprili 2019

Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme

Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme

1. Mwanadamu hapasi kujitukuza wala kujipa sifa. Anapaswa kumwabudu na kumsifu Mungu.
2. Unapaswa kufanya lolote ambalo lina manufaa kwa kazi ya Mungu, na hupasi kufanya chochote ambacho kitaleta madhara kwa manufaa ya kazi ya Mungu. Unapaswa kutetea jina la Mungu, ushahidi Wake, na kazi ya Mungu.

Ijumaa, 5 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sisitiza Uhalisi Zaidi

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sisitiza Uhalisi Zaidi

Kila mtu ana uwezekano wa kukamilishwa na Mungu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuelewa ni huduma gani kwa Mungu inayofaa zaidi makusudi ya Mungu. Watu wengi hawajui kumwamini Mungu humaanisha nini na hawajui kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu. Yaani, watu wengi zaidi hawana ufahamu wa kazi ya Mungu au lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu. Hadi leo, watu wengi zaidi bado wanadhani kumwamini Mungu kunahusu kwenda mbinguni na roho zao kuokolewa.

Jumamosi, 30 Machi 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumwabudu Mungu,

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Utakatifu wa Mungu (III)

Mnahisi vipi baada ya kusema sala zenu? (Tunafurahia na kuguswa sana.) Wacha tuanze ushirika wetu. Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini hasa mada inayohusiana na kiini cha Mungu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu.

Alhamisi, 28 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hukumu,

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu.

Jumatano, 27 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Pili

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Zaidi ya mwanadamu kutafuta kwa tamaa umaarufu na faida, daima anaendelea kutekeleza uchunguzi wa sayansi na utafiti wa kina, kisha bila kikomo huridhisha mahitaji yake ya mwili na tamaa; yapi tena ni matokeo ya mwanadamu? Kwanza kabisa hakuna tena usawa wa ikolojia na, pamoja na hili, miili ya wanadamu yote imetiwa doa na kuharibiwa na mazingira ya hali hii, na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na mapigo kusambaa kila mahali.

Jumanne, 26 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Unaona nini katika haya? Wakati Mungu alipofanya kazi katika ubinadamu, mbinu, maneno, na ukweli Wake mwingi vyote vilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu. Lakini wakati uo huo tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mapenzi Yake vyote vilionyeshwa kwa watu kuweza kujua na kuvielewa.

Jumapili, 24 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Tatu

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika moyo wa Nuhu na fahamu yake, uwepo wa Mungu ulikuwepo na bila shaka, na hivyo basi utiifu wake kwa Mungu ulikuwa haujatiwa doa wala toa na ungeweza kustahimili majaribio. Moyo wake ulikuwa safi na wazi kwa Mungu.

Jumamosi, 23 Machi 2019

Matamshi ya Kristo | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ukweli

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)

Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Je, "Mungu Ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote" ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Je, una ufahamu wowote wa juujuu kuhusu jambo hilo? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu.

Ijumaa, 22 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Pili

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Hakuna kizuizi chochote katika kazi Yake na kile Anachokifanya, na haitawekewa kizuizi chochote na binadamu yeyote, kitu chochote, au kifaa chochote, na haitakatizwa na nguvu zozote za kikatili.

Jumanne, 19 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ukweli,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)
Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya mada hii: Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.

Jumatatu, 4 Machi 2019

Nyimbo za kuabudu | 318. Maana ya Kweli ya Imani kwa Mungu

I
Watu wengi sana wanaamini, lakini wachache sana wanaelewa maana ya imani katika Mungu,
kile wanachohitaji kufanya ili kwenda pamoja na moyo wa Mungu.
Wengi sana wanajua neno "Mungu," wanajua maneno kama "kazi ya Mungu,"
lakini hawamjui Yeye, wala kile Anachofanya kweli.
Sio ajabu imani yao ni pofu.

Jumatatu, 25 Februari 2019

33. Mungu Mwenye Mwili Awaongoza Binadamu Kuingia Katika Enzi Mpya

Mungu mwenye mwili, Anaitamatisha enzi
wakati tu mgongo wa Yehova ulionekana.
Pia Anahitimisha enzi ya imani
ambapo kutokuwa yakini kwa Mungu kulifikiriwa.
Kazi ya Mungu wa mwisho mwenye mwili
humleta mwanadamu katika enzi ya utendaji zaidi.

Jumatano, 20 Februari 2019

Maneno ya Mungu | Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji

Mwenyezi Mungu anasema:" Kama unamwamini Mungu, ni lazima umtii Mungu, uweke ukweli katika vitendo na utimize wajibu wako wote. Zaidi ya hayo, ni lazima uelewe mambo unayopaswa kupitia. Ikiwa unapitia tu kushughulikiwa, kufundishwa nidhamu na hukumu, kama wewe unaweza tu kumfurahia Mungu, lakini huwezi kuhisi wakati Mungu anakufundisha nidhamu au kukushughulikia, hili halikubaliki. Labda katika wakati huu wa usafishaji unaweza kushikilia msimamo wako. Hii bado haitoshi; ni lazima uendelee mbele.