Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Tatu
Mwenyezi Mungu anasema, “Katika moyo wa Nuhu na fahamu yake, uwepo wa Mungu ulikuwepo na bila shaka, na hivyo basi utiifu wake kwa Mungu ulikuwa haujatiwa doa wala toa na ungeweza kustahimili majaribio. Moyo wake ulikuwa safi na wazi kwa Mungu.
Hakuhitaji maarifa ya mafundisho ya dini mengi mno ili kujishawishi kufuata kila neno la Mungu, wala hakuhitaji ukweli mwingi kuthibitisha uwepo wa Mungu, ili akubali kile Mungu alimwaminia na kuweza kufanya chochote kile ambacho Mungu angemruhusu kufanya. Hii ni tofauti muhimu kati ya Nuhu na watu wa leo, na pia ndio ufasili wa kweli hasa kuhusu binadamu mtimilifu alivyo machoni mwa Mungu. Kile anachotaka Mungu ni watu kama Nuhu. Yeye ni aina ya mtu anayesifiwa na Mungu, na pia hasa mtu wa aina ile ambaye Mungu hubariki. Mmepokea nuru yoyote kutoka haya? Watu huangalia watu kutoka nje, huku naye Mungu anaangalia mioyo ya watu na kiini chao.”
Yaliyopendekezwa: Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Tatu
Tufuate: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni