Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 28 Novemba 2018

Sura ya 47. Wale Ambao Wamepoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi

Sura ya 47. Wale Ambao Wamepoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi

Katika kazi ya kueneza injili ya Mungu ya siku za mwisho, watu walio wachache tu ndio wanaweza kuacha kila kitu na kuziacha familia zao, kufikia kiwango ambacho wanahisi hawatarudi nyumbani kwa miaka kumi au kwa maisha yao yote, na hawahisi mateso yoyote kwa sababu ya kufanya hivyo; hii ndiyo nguvu inayopewa watu na Roho Mtakatifu. Lakini kiwango hiki hakiwezi kufikiwa kupitia kwa kimo cha mtu, kwa sababu watu hawaumiliki ukweli, uaminifu fulani tu wa kutumia kwa ajili ya Mungu. Kama watu wanao uamuzi fulani wa kuutafuta ukweli, na Roho Mtakatifu kisha awape neema fulani, basi watahisi hasa kuwa na shukrani na watakuwa na nguvu za aina fulani, na hivyo wataweza kujitokeza na kutumia kwa ajili ya Mungu—hii ndiyo neema ya Mungu. Lakini wapo baadhi ya watu wasioifuata njia sahihi wakati wanapoutekeleza wajibu wao, hawautafuti ukweli hata kidogo na hata wanakosa adabu, na katika hali kama hiyo Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yao. Yaani, mtu huyo hayuko sahihi, na hata kama Roho Mtakatifu aliwahi kufanya kazi ndani yake, kazi hiyo itaharibiwa na wao watafuata bila kukusudia njia ya kwenda chini.

Jumatatu, 16 Julai 2018

Uzoefu wa Kutenda Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Ukweli, Umeme wa Mashariki

Uzoefu wa Kutenda Ukweli

Hengxin     Jiji la Zhuzhou, Mkoa wa Hunan
Sio muda mrefu mno uliopita, nilisikia "Ushirika na Kuhubiri Kuhusu Kuingia kwa Maisha," jambo ambalo lilinielekeza kuelewa kwamba ni wale tu wanaotenda ukweli wanaoweza kupata ukweli na hatimaye kuwa wale ambao wanaomiliki ukweli na ubinadamu hivyo kupata kibali cha Mungu.

Jumatatu, 11 Juni 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | 53 Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | 53  Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu

Je, mnaona kwa dhahiri njia ya imani yenu kwa Mungu na njia yenu ya kufuata ukweli? Imani katika Mungu kweli ni nini? Je, mmetosheka baada ya kupitia shida kidogo? Watu wengine hufikiri kwamba baada ya kupitia hukumu na kuadibiwa, kupogolewa na ushughulikiwaji au baada ya kufichua hali yao ya kweli, wamemaliza na matokeo yao yameonekana. Wengi wa watu hawawezi kuona suala hili kwa dhahiri, na wao wote husimamishwa hapo, bila kujua jinsi ya kuitembea njia iliyo mbele. Kwa ujumla, wasipopitia ushughulikiwaji na upogolewaji au hawana vikwazo vyovyote, watahisi kama kutafuta ukweli wakati wakiamini katika Mungu, na watahisi kwamba wanapaswa kuyatosheleza mapenzi ya Mungu.

Alhamisi, 7 Juni 2018

Sura ya 16. Imani Tatu katika Mungu wa Vitendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Sura ya 16. Imani Tatu katika Mungu wa Vitendo

Mwenyezi Mungu alisema, Ndani ya familia ya Mungu, kuna imani kadhaa tofauti katika Mungu; imani hizi tofauti lazima zitambulishwe ili kuona wewe ni wa gani.

Alhamisi, 15 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 40. Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa MasharikiKanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 40. Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako

Mwenyezi Mungu alisema, Katika miaka yote ya kuipitia kazi na kusikiliza mahubiri, kuna watu wengine ambao wanajifahamu, na watu wengine ambao hawana ufahamu wowote kujihusu; watu wengine wanaweza kuzungumza kuhusu vitu fulani halisi, na kuwasiliana hali halisi zao wenyewe,

Jumapili, 18 Februari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 35. Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Petro an yesu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 35. Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro
Mwenyezi Mungu alisema, Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake.

Jumatano, 14 Februari 2018

Umeme wa Mashariki | Sura ya 91. Kupitia Aina Tofauti Za Mazingira Kuna Manufaa Kwa ukuaji Wa Maisha Ya Binadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Umeme wa Mashariki | Sura ya 91. Kupitia Aina Tofauti Za Mazingira Kuna Manufaa Kwa ukuaji Wa Maisha Ya Binadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Ni vyema kupitia mazingira ya aina tofauti. Mungu hakupangii mazingira haya bila sababu. Yeye hakuongozi popote pale bila makusudi, bali Yeye huandaa mazingira fulani spesheli kwa kila mmoja—mazingira ya kifamilia, mazingira ya kimaisha, mazingira uliyokulia, na mazingira unatekeleza majukumu yako punde utakapo mwamini. Yeye hutayarisha hali au mazingira fulani spesheli kwako wewe kuzipitia.

Sura ya 44. Kuutoa Ukweli Ndiyo Njia ya Kweli ya Kuwaongoza Wengine

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 44. Kuutoa Ukweli Ndiyo Njia ya Kweli ya Kuwaongoza Wengine
Mwenyezi Mungu alisema, Ikiwa mnataka kufanya kazi nzuri katika kuwaongoza wengine na kuhudumu kama mashahidi wa Mungu, la muhimu zaidi, lazima uwe na ufahamu wa kina wa kusudi la Mungu katika kuwaokoa watu na kusudi la kazi Yake. Lazima uyaelewe mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake mbalimbali ya watu. Unapaswa kuwa mwenye utendaji katika juhudi zenu; upitie tu kiasi unachoelewa na kuwasiliana tu kile unachokijua.

Ijumaa, 9 Februari 2018

Sura ya 49. Unapaswa Kuutumia Ukweli Kumaliza Hali Yako Hasi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 49. Unapaswa Kuutumia Ukweli Kumaliza Hali Yako Hasi
Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wana hali hizi ambazo tumejadiliana hapo awali, hata ingawa si wazi kama hapo awali. Hii ni kwa sababu watu hawakuwa na ufahamu wowote wa ukweli wakati huo, na hawakuelewa chochote. Siku hizi, unasikiliza zaidi, na kwa kiwango cha chini kabisa, nyote mnaelewa baadhi ya mafundisho. Hata hivyo, una hali fulani zilizojikita ndani ambazo hazijafunuliwa.

Jumanne, 6 Februari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 39. Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa MasharikiSura ya 39. Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia
Mwenyezi Mungu alisema, Ni nini mnafahamu kuhusu mabadiliko katika tabia? Asili ya mabadiliko katika tabia na mabadiliko katika mwenendo ni tofauti, na mabadiliko katika matendo pia ni tofauti—yote ni tofauti kwa asili. Watu wengi wanaweka mkazo maalum kwa tabia yao katika imani yao kwa Mungu, matokeo yakiwa mabadiliko yanayofanyika katika mienendo yao. Baada ya kuamini katika Mungu, wanakoma kubishana na wengine, wanakoma kupigana na watu na kuwatukana, wanakoma kuvuta sigara na kunywa, hawaibi mali ya uma—hata iwe msumari ama kipande cha mbao pekee—na hata wanaenda

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 37. Kanuni Kuu za Jinsi Wafanyakazi Hufanya Kazi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa MasharikiSura ya 37. Kanuni Kuu za Jinsi Wafanyakazi Hufanya Kazi

Mwenyezi Mungu alisema, Katika kazi yao, wafanyakazi wanapaswa kuzingatia mambo mawili: Moja ni kufanya kazi kabisa kulingana na kanuni zilizowekwa masharti na mipangilio ya kazi. Wafanyakazi hawapaswi kukiuka kanuni hizi, wasifanye kazi kulingana na mawazo yao wenyewe, na siyo kulingana na mapenzi yao. Wanapaswa kuonyesha uhusiano kwa kazi ya familia ya Mungu, na kuweka maslahi ya familia ya Mungu kwanza katika kila kitu wakifanyacho. Jambo jingine pia ni muhimu, na ni kwamba, katika kila kitu wakifanyacho, kuzingatia kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, na kufanya kila kitu kwa ukali kulingana na neno la Mungu.

Jumapili, 4 Februari 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 92. Njia ya Utendaji katika Kusuluhisha Ukaidi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 92. Njia ya Utendaji katika Kusuluhisha Ukaidi

Mwenyezi Mungu alisema, Mtu huwa na tatizo lipi anapopenda kupeana visingizio? Ni nini kiini chake? Yeye ni mkaidi. Watu wakaidi hawakubali ukweli kwa urahisi; sio watiifu, na wanaposikia neno moja ambalo haliambatani na dhana, mitazamo, wanayopenda, hisia au mihemko yao wenyewe, basi hawalikubali; husema, “Sijali iwapo liko sahihi au ni mbaya, ni nani aliyelinena,

Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini
Mwenyezi Mungu alisema, Nguzo inapopandishwa kidogo, mnaweza kupiga hatua kidogo. Si jambo baya kuwa na mahitaji ya juu kutoka kwenu na wala si jambo baya kuwauliza maswali magumu. Lengo ni kuwafanya muwe na ufahamu zaidi juu ya elimu na maarifa ya kawaida ya kipengele cha weledi cha wajibu wenu.[a] Huenda labda nyinyi bado hulalamika katika nyoyo zenu, mkisema: "Tumejifunza mambo mengi mazuri lakini Mungu huwa hayataji kamwe au kuturuhusu kuyatumia. Kwa hiyo hatuthubutu kuyataja au kuyatumia.

Jumamosi, 3 Februari 2018

Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu
Mwenyezi Mungu alisema, Ninaibua maswali machache kwa tafakari yenu: Tangu mara ya mwisho tuliposema kwamba kutakuwa na miaka saba mingine ya majaribu makubwa, iwe ni kwa dhiki au majanga, je, mmegundua kusudi la Mungu kupitia kwa hayo? Ni asili gani ya binadamu mnaweza kuona katika mijibizo na mitazamo ya watu kwa miaka hii saba ya majaribu? Hili litachanganuliwa vipi? Fikirieni hilo. Ninazungumzia asili ya binadamu katika kila ushirika, kufikia chanzo, kuchanganua asili ya binadamu, na kuchanganua kiini.

Sura ya 51. Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, imani ya kidini

Sura ya 51. Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?
Mwenyezi Mungu alisema, Ninyi nyote mara nyingi mmepata uzoefu wa hali ya kuwa katika mkutano, na kuhisi kana kwamba huna chochote cha kuhubiri kuhusu—hatimaye unajilazimisha na unasema kitu cha juu juu. Unajua vizuri kuwa maneno haya ya juu juu ni kanuni, lakini unahubiri kuyahusu hata hivyo, na mwishowe unahisi kuwa huna shauku, na watu chini yako wanasikiliza na wanahisi kuwa yanachosha sana—je hilo halijafanyika?

Ijumaa, 2 Februari 2018

Sura ya 28. Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 28. Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kutoa kwenu "muhtasari kuhusu ukweli" hakufanywi ili kuwawezesha watu kupata maisha au kupata mabadiliko katika tabia zao kutoka kwa ukweli. Badala yake, kunafanywa ili watu waweze kuwa weledi wa maarifa na mafundisho fulani kutoka kwa ukweli. Wao huonekana kana kwamba wanaelewa lengo lililokusudiwa katika kazi ya Mungu, wakati kwa kweli wamekuwa weledi wa baadhi ya maneno ya mafundisho tu. Hawaelewi maana iliyokusudiwa ya ukweli, na si tofauti na kusomea theolojia au kusoma Biblia.

Umeme wa Mashariki | Sura ya 15. Kutoka katika Siasa Isiyo na Kadri hadi Kutafuta kuwa Msaliaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

1. Uhamaji wa Watu kuelekea kwenye Siasa Isiyo na Kadri
Je, nyote mmekuwa mkitafuta nini hivi karibuni? Je, imekuwa mabadiliko ya tabia na kuwa na ushuhuda wa Mungu? Haijakuwa hiyo! Nawaona watu wengi tena wakitafuta kufa kwa ajili ya Mungu ili kumuaibisha Shetani. Je, mnasubiri tu kuadhibiwa badala ya kupanga kutenda ukweli ama kutafuta kubadilishwa kwa tabia, kulipiza upendo wa Mungu? Baada ya kusoma “Usaliti (1) “na “Usaliti (2), “watu walikuwa na mipango ya kufa.

Jumatano, 31 Januari 2018

Sura ya 52. Dalili za Udanganyifu Ndani ya Mwanadamu na Asili ya Mwanadamu Ambazo Humsaliti Mungu

Sura ya 52. Dalili za Udanganyifu Ndani ya Mwanadamu na Asili ya Mwanadamu Ambazo Humsaliti Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Ugumu ambao watu wanaweza kuukabili kwa urahisi katika uzoefu wao, vitu ambavyo vinawasababisha watu kuanguka kwa urahisi, na pahali ambapo udhaifu wa jaala wa kila mtu upo yote ni masuala ambayo lazima mtu awe na ujuzi nayo. Kwa nini unaanguka, unamwacha Mungu na kupoteza imani ya kuendelea na ukimbiziaji wako wa ukweli unapokabiliana na mambo fulani? Kwa sasa, kila mtu yumo hatarini mwa mambo haya.

Sura ya 55. Usieleze Kile Mungu Alicho Nacho na Kile Alicho

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 55. Usieleze Kile Mungu Alicho Nacho na Kile Alicho
Mwenyezi Mungu alisema, Kazi na matamshi ya Mungu ya miaka michache iliyopita yote yamerekodiwa kimsingi katika kitabu, Neno Laonekana katika Mwili. Baadhi ya maneno katika kitabu hiki ni ya kinabii na yanatabiri vile enzi za baadaye zitakavyokuwa. Unabii kwa kweli ni mfumo wa jumla, na zaidi ya nusu ya kitabu kinajadili kuingia kwa mwanadamu kwa maisha, kinaweka wazi utu, na kinazungumzia kuhusu kumwelewa Mungu na tabia Yake.

Jumamosi, 27 Januari 2018

Sura ya 38. Yeye Ambaye Hukosa Ukweli Hawezi Kuwaongoza Wengine

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 38. Yeye Ambaye Hukosa Ukweli Hawezi Kuwaongoza Wengine

Mwenyezi Mungu alisema, Je, kweli mnaelewa kuhusu mabadiliko katika tabia ya mtu? Mabadiliko katika tabia yanamaanisha nini? Je, mnaweza kutambua mabadiliko katika tabia? Ni hali zipi zinaweza kufikiriwa kuwa mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu, na ni hali zipi ambazo ni mabadiliko tu katika tabia ya nje? Tofauti ni ipi kati ya mabadiliko katika tabia ya mtu ya nje na mabadiliko katika maisha ya mtu ya ndani? Je, mnaweza kueleza tofauti?