Jumatatu, 4 Machi 2019

Nyimbo za kuabudu | 318. Maana ya Kweli ya Imani kwa Mungu

I
Watu wengi sana wanaamini, lakini wachache sana wanaelewa maana ya imani katika Mungu,
kile wanachohitaji kufanya ili kwenda pamoja na moyo wa Mungu.
Wengi sana wanajua neno "Mungu," wanajua maneno kama "kazi ya Mungu,"
lakini hawamjui Yeye, wala kile Anachofanya kweli.
Sio ajabu imani yao ni pofu.
Hawalichukulii hili kwa uzito kwa sababu ni geni na lisilo la kawaida.
Hivyo wamepungukiwa sana na mahitaji ya Mungu. Ee …
Kama watu hawamjui Mungu na kazi Yake, basi hawastahili kwa matumizi ya Mungu,
sembuse kuridhisha hamu ya Mungu.
Kuamini kuwa Mungu yupo hakutoshi.
Hiyo ni rahisi sana, ni ya dini sana.
Sio sawa na imani ya kweli Kwake.
Imani ya kweli katika Mungu inamaanisha unapitia kazi Zake na maneno Yake
kwa imani kuwa Anatawala juu ya kila kitu.
Kisha unaweza kujiweka huru kutoka kwa tabia potovu
na utimize hamu za Mungu katika maisha yako na uje kumjua Yeye.
Hiyo ndiyo njia ya imani ya kweli kwa Mungu. Hiyo ni njia ya imani ya kweli Kwake.
II
Wengi sana wanafikiria kuamini ni kama kitu rahisi na cha juu juu.
Imani kama hii haina maana. Mungu atawezaje kuidhinisha?
Wako katika njia mbaya.
Wale wanaoamini katika barua, katika mafunzo matupu bado hawajui
kwamba imani yao si ya kweli na hawatakubaliwa na Mungu.
Bado wanaomba amani na neema.
Chukua muda na ufikirie kama imani ni rahisi hivyo. Je, ni kuomba tu amani na neema? Aa …
Unaweza kutimiza hamu Yake, kama bado unampinga, kutomjua?
Kuamini kuwa Mungu yupo hakutoshi.
Hiyo ni rahisi sana, ni ya dini sana.
Sio sawa na imani ya kweli Kwake.
Imani ya kweli katika Mungu inamaanisha unapitia kazi Zake na maneno Yake
kwa imani kuwa Anatawala juu ya kila kitu.
Kisha unaweza kujiweka huru kutoka kwa tabia potovu
na utimize hamu za Mungu katika maisha yako na uje kumjua Yeye.
Hiyo ndiyo njia ya kweli ya imani kwa Mungu. Hiyo ndiyo njia ya imani ya kwa Mungu.
Hiyo ndiyo njia ya imani ya kweli Kwake.
kutoka katika "Dibaji" katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni