"Kaa Mbali na Shughuli Zangu" (2) - Je, Kuikubali Injili ya Kurudi kwa Pili kwa Yesu Kristo ni Uasi wa Dini?
Kwenye Biblia, Paulo alisema, "Nashangaa kwamba mmejiondoa upesi hivi kwake yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kuelekea injili nyingine" (Wagalatia 1:6). Wachungaji na wazee wa kanisa huyafasiri vibaya maneno haya ya Paulo na kuwashutumu watu wote wanaoikubali injili ya kurudi kwa pili kwa Bwana Yesu, wakisema kwamba huu ungekuwa uasi wa dini na kwamba ungekuwa kumsaliti Bwana.