Swali la 2: Unashuhudia kwamba Mungu amekuwa mwili na kuwa Mwana wa Adamu ili kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, na bado wengi wa wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanakiri kwamba Bwana atarudi akija na mawingu, na wanategemeza hili hasa aya za Biblia: "Huyu Yesu … atakuja kwa namna hiyo hiyo ambayo mmemuona akienda mbinguni" (MDO 1:11). "Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye" (UFU.1:7). Na zaidi ya hayo, wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa pia hutufundisha kwamba Bwana Yesu yeyote asiyekuja na mawingu ni wa uongo na lazima aachwe. Kwa hiyo hatuna uhakika kama mtazamo huu unakubaliana na Biblia; ni sahihi kuchukua huu kama ukweli au la?
Jibu:
Ndugu, ikija kwa kungoja kushuka kwa Bwana na mawingu, lazima tusitegemee mawazo ya mwanadamu na fikira! Mafarisayo walifanya kosa kubwa kwa kungoja kufika kwa Masiha. Walitumia kabisa mawazo na fikira ya mwanadamu kumtathmini Bwana Yesu ambaye alisharudi tayari. Mwishowe, walimsulubisha Bwana Yesu msalabani. Je, huu sio ukweli? Je, kungoja kufika kwa Bwana ni rahisi kama tufikiriavyo? Ikiwa Bwana atarudi na kufanya kazi kati ya binadamu kama jinsi Bwana Yesu kwa mwili Alikuwa Amefanya, na hatumtambui Yeye, basi pia sisi tutamhukumu na kumshutumu Yeye kama vile Mafarisayo walivyofanya na kumsulubisha Yeye mara nyingine?