Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?
Watu wengi hawaelewi ni kwa nini, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu katika siku za mwisho, Bwana Yesu anaitwa Mwenyezi Mungu wakati Anapokuja kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa nini haendelei kuitwa Bwana Yesu? Kwa kweli, Mungu ana jina jipya kila wakati Anapofanya hatua moja ya kazi Yake. Jina hili jipya linachukuliwa na Mungu Mwenyewe kama inavyofaa kazi hii–siyo kitu ambacho watu humuita Yeye kama wanavyotaka. Jina analolichukua Mungu katika kila hatua ya kazi lina msingi wake katika Biblia.
Jina la Bwana Yesu aliyerejea wa siku za mwisho lilitabiriwa zamani katika Biblia. Isaya alisema "Na Watu wa Mataifa wataweza kuiona haki yako, nao wafalme wote watauona utukufu wako; na wewe utaitwa kwa jina jipya, jina ambalo kinywa cha Bwana kitalitamka "(Isaya 62: 2). Katika Kitabu cha Ufunuo, ilisemwa pia kuwa " Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika…. Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, na nitaliandika jina la Mungu wangu juu yake, na jina la mji wa Mungu wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu: na nitaliandika juu yake jina langu jipya"(Ufunuo 3: 7, 12). “Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, Akasema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi” (Ufunuo 1: 8). “Na nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu Mwenyezi humiliki.” (Ufu 19: 6). Jina la Mwenyezi Mungu wa Enzi ya Ufalme ni utimizaji kamili waunabii wa kitabu cha Ufunuo. Jina ambalo Mungu huchukua katika kila enzi lina umuhimi mkubwa na limeshikamana kwa undani na kazi ya Mungu wakati wa enzi hiyo. Mwenyezi Mungu alifichua mafumbo yanayohusiana na hili Aliposema, “Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake? Kwa njia hii, lazima Mungu aitwe kwa jina tofauti katika enzi tofauti, lazima atumie jina kubadilisha enzi na kuwakilisha hiyo enzi, kwa kuwa hakuna jina moja linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe kikamilifu. Na kila jina linaweza tu kuwakilisha tabia ya Mungu wakati wa enzi fulani na linahitaji tu kuwakilisha kazi yake. Kwa hivyo, Mungu Anaweza kuchagua jina lolote ambalo linafaa tabia yake kuwakilisha enzi nzima. Bila kujali iwapo ni enzi ya Yehova, au ni enzi ya Yesu, kila enzi inawakilishwa kwa jina.” (“Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“‘Yehova’ ni jina ambalo Nilichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, na linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Lina maana Mungu Anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. “Yesu” ni Imanueli, na lina maana sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, na Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, na Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja tu ya mpango wa usimamizi. Hivyo ni kusema, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wa Uyahudi waliochaguliwa, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa na Mungu wa Wayahudi wote. Na sasa katika enzi hii, Wayahudi wote isipokuwa kabila la Uyahudi wanamwabudu Yehova. Wanatoa kafara Kwake kwa madhabahu, na kumtumikia wakivaa mavazi ya kikuhani hekaluni. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Ambayo ni kusema, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, na kuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu liliwepo ili kuwezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, na ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hivyo jina Yesu linawakilisha kazi ya wokovu, na kuashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliwi bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” Anawakilisha Enzi ya Sheria, na ni jina la heshima kwa Mungu Aliyeabudiwa na Wayahudi. “Yesu” Anawakilisha Enzi ya Neema, na ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kufika kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anatarajia Afike na picha Aliyokuwa nayo kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, na usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, na enzi isingefikishwa kikomo. Hii ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni wa ukombozi na wokovu wa mwanadamu peke yake. Nilichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, na silo jina ambalo nitatumia kuleta wanadamu wote kufika kikomo. Ingawa Yehova, Yesu, na Masiha yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria wakati tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, na hayauwakilishi ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Kwa hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, na wala sio Masiha, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitaleta enzi nzima kufikia tamati. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Niliitwa pia Masiha, na watu wakaniita Yesu Mwokozi pia wakati mmoja kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi sio Yehova au Yesu Ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu Ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu Ambaye ataleta enzi kufika mwisho. Mimi ni Mungu Mwenyewe Ambaye Anainuka katika kingo za dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu” (“Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Mwenyezi Mungu alisema kwa dhahiri kwamba kuna umuhimu mwakilishi kwa jina ambalo Mungu huchukua katika kila enzi: Kila moja huwakilisha kazi ya Mungu na tabia Anayoonyesha katika enzi hiyo. Wakati wa Enzi ya Sheria, Mungu alitumia jina la Yehova kutangaza sheria na amri Zake na kuyaongoza maisha ya wanadamu duniani; wakati wa Enzi ya Neema, Mungu alitumia jina la Yesu kufanya kazi ya ukombozi wa wanadamu; na wakati wa Enzi ya Ufalme, Mungu anaitwa Mwenyezi Mungu, Yeye hufanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu kumtakasa, kumbadilisha, na kumwokoa mwanadamu. Mungu hubadilisha enzi akitumia jina Lake, na hutumia jina hili kuwakilisha kazi ya enzi. Wakati Yehova Mungu alifanya kazi ya Enzi ya Sheria, ni kwa kuomba tu kwa jina la Yehova na kutii sheria na amri Zake ndipo watu wangeweza kubarikiwa na kulindwa na Mungu. Kwa kuwasili kwa Enzi ya Neema, Mungu alitumia jina la Yesu kufanya kazi ya ukombozi, na watu hawakuwa na budi ila kumkubali Bwana Yesu kama Mwokozi, na kuombea toba kwa jina la Bwana, kusamehewa dhambi zao na kufurahia ukweli na neema iliyotolewa na Bwana Yesu. Ikiwa watu bado walishikilia jina la Bwana na kukataa kumkubali Bwana Yesu, basi walipoteza utunzaji na ulinzi wa Mungu, na walianguka katika giza, wakilaaniwa na kuadhibiwa na Mungu kama Mafarisayo Wayahudi. Pamoja na ujio wa siku za mwisho, Mungu hutumia jina la Mwenyezi Mungu kutekeleza kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu. Ni kwa kukubali jina la Mwenyezi Mungu tu, kwenda sambamba na hatua za kazi ya Mungu, na kufanyiwa hukumu na kuadibiwa kwa Mwenyezi Mungu, ndipo watu wanaweza kuelewa na kupata ukweli, kujitenga na dhambi, kutakaswa, na kupokea wokovu wa Mungu. Wote wanaokataa kulikubali jina la Mwenyezi Mungu na kukataa kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho hawawezi kujitoa wenyewe kutoka kwa utumwa wa dhambi, na milele hawatakuwa na sifa kamili kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni