Jumamosi, 20 Aprili 2019

Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu

Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu
Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake. Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu. Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya. Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake. Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana. Tunatafakari, kufikiri maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu anatuangazia. Tunaondolewa vizuizi na ubaguzi wetu, tunaishi ndani ya upendo wa Mungu.

Ijumaa, 19 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 9

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 9

Katika mawazo ya watu, Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu haneni lugha ya mwanadamu, wala mwanadamu hawezi kunena lugha ya Mungu, na kwa Mungu, madai ya mwanadamu Kwake ni rahisi, ilhali matakwa ya Mungu kwa mwanadamu hayafikiki na hayafikiriki kwa mwanadamu. Ukweli, hata hivyo, ni kinyume kabisa: Mungu anataka tu “asilimia 0.1” ya mwanadamu. Hili si la kushangaza tu kwa kila mtu, lakini pia huwafanya wahisi kukanganyikiwa sana, kama kwamba wote wamechanganyikiwa.

Alhamisi, 18 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili



Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. 
Maudhui ya video hii: 
Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote 
Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri
 Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Kiini Chake 
Mtu Hafai Kutegemea Uzoefu na Fikira Ili Kujua Tabia ya Haki ya Mungu

Jumatano, 17 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 98

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 98

Mambo yote yatakuja juu ya kila mmoja wenu, na yatawawezesha kujua zaidi juu Yangu na kuwa na uhakika zaidi juu Yangu. Yatawawezesha kunijua, Mungu mmoja Mwenyewe, kunijua Mimi Mwenye uweza, kunijua Mimi Mungu Mwenyewe mwenye mwili. Baadaye, Nitatoka katika mwili, Nirudi Sayuni, Nirudi katika nchi nzuri ya Kanaani, ambayo ni makazi Yangu, ndiyo hatima Yangu, na ndio msingi ambao niliumba vitu vyote. Sasa hakuna yeyote kati yenu anayeelewa maana ya maneno ambayo Ninasema, hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kuelewa maana ya maneno haya.

Jumanne, 16 Aprili 2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
 Maudhui ya video hii: 
3. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu

Yaliyopendekezwa: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"

Tufuate: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatatu, 15 Aprili 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 26

Kutoka kwa maneno yote yaliyonenwa na Mungu, inaweza kuonekana kwamba siku ya Mungu inakaribia kila siku inapopita. Ni kama kwamba siku hii iko mbele ya macho ya watu, kama kwamba itafika kesho. Hivyo, baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu wote wanajawa na hofu, na pia wana hisia kiasi fulani ya ukiwa wa dunia. Ni kama kwamba, jinsi majani yanavyoanguka na manyunyu kushuka, watu wote wametoweka wasionekane tena, kama kwamba wote wameondolewa kabisa kutoka duniani.