Alhamisi, 18 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili



Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. 
Maudhui ya video hii: 
Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote 
Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri
 Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Kiini Chake 
Mtu Hafai Kutegemea Uzoefu na Fikira Ili Kujua Tabia ya Haki ya Mungu

Mwenyezi Mungu anasema, Namna Mungu alivyoshughulikia binadamu wote wa ujinga na kutojua ulitokana kimsingi na huruma na uvumilivu. Hasira yake, kwa upande mwingine, imefichwa kwenye wingi mkubwa mno wa muda na wa mambo; haijulikani kwa binadamu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati binadamu anakabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya kuvumilia na kusamehe binadamu—yaani, wakati onyesho la mwisho la Mungu la huruma na onyo Lake la mwisho linapowafikia—kama bado wangali wanatumia mbinu zile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali huruma Yake, Mungu hataweza tena kuwapatia uvumilivu na subira yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, ni katika wakati huu ambapo Mungu atafuta huruma Yake. Kufuatia hili, Atatuma tu hasira Yake. Anaweza kuonyesha hasira Yake kwa njia tofauti, kama vile tu Anavyoweza kutumia mbinu tofauti kuwaadhibu na kuwaangamiza watu.

Tazama Video: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Nne

Yaliyopendekezwa: APP ya Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni