Jumatatu, 22 Oktoba 2018

Swahili Gospel Video Clip "Mungu Kuja Duniani na Kuwa Sadaka ya Dhambi"


Swahili Gospel Video Clip "Mungu Kuja Duniani na Kuwa Sadaka ya Dhambi"

    Wakati wa Enzi ya Neema, Bwana Yesu alikuja miongoni mwa mwanadamu na kusulubiwa kwa ajili yake. Alimkomboa mwanadamu kutoka kwa utumwa wa sheria, na kwa sababu ya sadaka ya dhambi, wanadamu walifurahia upendo wa Bwana na huruma…. Kuja kwa Bwana Yesu kumleta mwanadamu kwa enzi mpya.

Jumapili, 21 Oktoba 2018

Swahili Gospel Video Clip "Ahadi ya Mungu kwa Waisraeli"


Swahili Gospel Video Clip "Ahadi ya Mungu kwa Waisraeli"

    Baada ya mamia ya miaka ya kuwekwa chini ya sheria, Waisraeli hatimaye walikabiliwa na hatari ya kuhukumiwa na kuuawa na sheria kwa sababu ya dhambi zao. Walimwita Mungu kwa haraka, ambaye aliwapa ahadi—ahadi ambayo ingezibadilisha kudura zao na kuweko. Hivyo ahadi hii ilikuwa nini hasa? Jibu limefichuliwa katika dondo hii ya filamu ya kustaajabisha ya Kikristo, Ahadi ya Mungu kwa Waisraeli.

Jumamosi, 20 Oktoba 2018

Swahili Gospel Video Clip "Mungu Akitoa Sheria"


Swahili Gospel Video Clip "Mungu Akitoa Sheria"
      Baada ya Musa kuwaongoza Waisraeli kutoka Misri, Mungu alitangaza sheria na amri, ambazo ziliyaongoza maisha ya Waisraeli duniani na kuwafundisha watu jinsi ya kumwabudu Mungu.

Ijumaa, 19 Oktoba 2018

Swahili Gospel Video Clip "Maangamizi ya Mungu ya Sodoma na Gomora"


Swahili Gospel Video Clip "Maangamizi ya Mungu ya Sodoma na Gomora"

     Ikifurika na uovu na uzinzi, miji hii miwili mikubwa ya Sodoma na Gomora iliichokoza tabia ya Mungu. Mungu alinyesha moto wa jahanamu kutoka mbinguni, akiiteketeza hiyo miji na watu ndani yayo hadi kuwa majivu, na kuwafanya watoweke katikati ya hasira Yake…. Tazama dondoo ya filamu ya Kikristo Maangamizo ya Mungu ya Sodoma na Gomora ili kujua zaidi juu ya tabia ya ghadhabu, isiyokiukwa ya Mungu na onyo Lake kwa vizazi vijavyo.

Kupotoka kwa Sodoma: Kunakasirisha Binadamu, Kunaghadhibisha Mungu

Kwenye usiku huo, Lutu alipokea wajumbe wawili kutoka kwa Mungu na akawatayarishia karamu. Baada ya chajio, kabla hawajalala, watu kutoka kila pahali kwenye mji walizunguka makazi ya Lutu na kumwita nje Lutu. Maandiko yanawarekodi wakisema, “Wako wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu?

Alhamisi, 18 Oktoba 2018

5. Ni zipi tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu?

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

5. Ni zipi tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Mimi nawabatiza na maji ili mtubu. Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake. Atawabatiza na Roho Mtakatifu, na moto" (MT 3:11).
Maneno Husika ya Mungu:
Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe.

4. Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

4. Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana" (YN. 5:22).
"Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu" (YN. 5:27).
Maneno Husika ya Mungu: