Jumatatu, 22 Oktoba 2018

Swahili Gospel Video Clip "Mungu Kuja Duniani na Kuwa Sadaka ya Dhambi"


Swahili Gospel Video Clip "Mungu Kuja Duniani na Kuwa Sadaka ya Dhambi"

    Wakati wa Enzi ya Neema, Bwana Yesu alikuja miongoni mwa mwanadamu na kusulubiwa kwa ajili yake. Alimkomboa mwanadamu kutoka kwa utumwa wa sheria, na kwa sababu ya sadaka ya dhambi, wanadamu walifurahia upendo wa Bwana na huruma…. Kuja kwa Bwana Yesu kumleta mwanadamu kwa enzi mpya.  Wakati huo huo, kuliimarisha uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, na kufungua asili mpya, mwanzo mpya kwa kazi ya Mungu ya usimamizi miongoni mwa binadamu.
Bila ukombozi wa Yesu, wanadamu wangeishi milele katika dhambi, na kuwa watoto wa dhambi, kizazi cha mapepo. Kama ingeendelea hivyo, Shetani angechukua makazi duniani, na dunia nzima ingekuwa makao yake. Lakini kazi ya ukombozi ilihitaji huruma na fadhili kwa wanadamu; kupitia kwa kazi hiyo tu ndio mwanadamu angeweza kupokea msamaha na mwishowe afuzu kufanywa kuwa mkamilifu na kupatwa kikamilifu. Bila hatua hii ya kazi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeweza kuendelea mbele. Kama Yesu hangesulubiwa, kama Yeye Angewaponya tu watu na kufukuza mapepo, basi watu hawangesamehewa dhambi zao kikamilifu. Miaka mitatu na nusu ambayo Yesu Alifanya kazi Yake hapa duniani ilikamilisha tu nusu ya kazi Yake ya ukombozi; kisha kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuwa na mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kukabidhiwa kwa mwovu, Yeye Alikamilisha kazi ya kusulubiwa na Akaanzisha hatima ya mwanadamu. Baada ya Yesu kukabidhiwa mikononi mwa Shetani tu, ndipo mwanadamu alikombolewa. Kwa miaka thelathini na mitatu na nusu Aliteseka duniani, Alidhihakiwa, Akatukanwa, na Akaachwa pweke, Aliachwa hata bila mahali pa kulaza kichwa chake, Hakuwa hata na mahali pa kupumzika; kisha Akasulubiwa, nafsi Yake yote—mwili safi na usio na hatia—kupigiliwa misumari msalabani, na kupitia kila namna ya mateso. Wale waliokuwa madarakani wakamdhihaki na kumcharaza mijeledi, na askari hata wakamtemea mate usoni; ila Alibaki kimya na kuvumilia mpaka mwisho, Akinyenyekea na kujitoa bila masharti mpaka wakati wa kifo, ambapo Yeye Alikomboa binadamu wote. Hapo tu ndipo Aliruhusiwa kupumzika. Kazi ya Yesu inawakilisha tu Enzi ya Neema; haiwakilishi Enzi ya Sheria na si mbadala wa kazi ya siku za mwisho. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, enzi ya pili ambayo binadamu amepitia—Enzi ya Ukombozi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni