"Kaa Mbali na Shughuli Zangu" (1) - Tushughulikie Vipi Umeme wa Mashariki kwa Njia Inayolingana na Mapenzi ya Bwana?
Wakati watu wanaposhuhudia kwamba Umeme wa Mashariki ndiko kurudi kwa Bwana Yesu, waumini wengi wanahisi kwamba Umeme wa Mashariki ndiyo njia ya kweli, na wanafaa kulitafuta na kulichunguza kwa bidii ili kuisikia sauti ya Bwana. Wachungaji na wazee wa kanisa wa dini, hata hivyo, wanaifasiri vibaya Biblia ili kulipinga na kulishutumu Umeme wa Mashariki.