Jumapili, 3 Juni 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 61. Si Rahisi Kuwa Mtu Mwaminifu

Zixin    Jiji la Wuhan, Mkoa wa Hubei
Kupitia kula na kunywa neno la Mungu na kusikiliza mahubiri, nilikuja kuelewa umuhimu wa kuwa mtu mwaminifu na hivyo nikaanza kufanya mazoezi kuwa mtu mwaminifu. Baada ya muda, niliona kuwa nilipata kuingia kiasi katika kuwa mtu mwaminifu. Kwa mfano: Wakati wa kuomba au kuzungumza na mtu, ningeweza kuongea ukweli na kutoka kwa moyo; niliweza pia kuchukulia kutekeleza wajibu wangu kwa uzito, na wakati nilipofichua upotovu niliweza kujiweka wazi kwa watu wengine. Kwa sababu ya hili, nilifikiri kuwa mtu mwaminifu lilikuwa jambo rahisi sana kutenda, na sio vigumu hata kidogo kama ilivyodaiwa kuwa na maneno ya Mungu: “Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu.” Ni baadaye tu nilipoweza kufahamu kupitia uzoefu kwamba kwa kweli si rahisi kwa mtu mpotovu kuwa mtu mwaminifu. Maneno ya Mungu kwa kweli ni ya kweli kikamilifu na hayajatiwa chumvi kabisa.

Jumamosi, 2 Juni 2018

Maigizo Yaliyosimuliwa ya Hadithi za Kweli "Upendo wa Kweli wa Mungu" (Swahili Subtitle)


Maigizo Yaliyosimuliwa ya Hadithi za Kweli "Upendo wa Kweli wa Mungu" (Swahili Subtitle)

Ili kujitengenezea nafasi yake mwenyewe duniani, mhusika mkuu alilazimika kufuata mwenendo wa duniani humu, akihangaika na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya umaarufu na hadhi. Maisha yake yalilikuwa hasa matupu na yenye maumivu. Baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu, alipata maana ya maisha ya binadamu ndani ya maneno ya Mwenyezi Mungu, na akiwa amejawa na furaha, akamfuata Mungu na kutimiza majukumu yake. Hata hivyo, kwa sababu moyo wake ulikuwa chini ya udhibiti wa umaarufu na hadhi, katika kutekeleza majukumu yake mara kwa mara alitenda kwa mujibu wa mawazo yake mwenyewe, na alikuwa dhalimu na mwenye udikteta. Kwa sababu hii, alipogolewa na kushughulikiwa na ndugu. Kwanza, alibishana na hakukubali. Kupitia hukumu na kuadibiwa na maneno ya Mungu, alikuja kujua ukweli wa upotovu wake. Hata hivyo, kwa sababu hakuelewa nia ya Mungu, alimwelewa Mungu visivyo na kufikiri Mungu hangeweza kumwokoa. Kwa wakati huu, neno la Mungu lilimtolea nuru polepole, likamwongoza, na kumfanya kuelewa nia ya Mungu yenye ari ya kumwokoa mwanadamu, na alipitia upendo wa kweli wa Mungu kwa wanadamu …

66. Ubia wa Kweli

Fang Li    Jiji la Anyang, Mkoa wa Henan
Hivi karibuni nilidhani nilikuwa nimeingia katika ubia wenye kuridhisha. Mshirika wangu na mimi tuliweza kujadili kitu chochote, wakati mwingine hata nikamwomba aonyeshe dosari zangu, na hatukupigana kamwe, hivyo nilidhani tulikuwa tumefanikisha ubia wenye kuridhisha. Lakini kama ukweli ulivyofichua, ubia wenye kuridhisha kwa kweli haukuwa kama kitu chochote nilichosadiki.
Siku moja katika mkutano, mshirika wangu alionyesha baadhi ya dosari zangu mbele ya mkuu wetu, akisema nilikuwa na kiburi, wa kutokubali ukweli, mwenye kudhibiti, mwenye kutiisha …. Kumsikia akisema hivyo kulinikasirisha mno, na nikawaza: "Jana nilikuuliza kama ulikuwa na maoni yoyote kunihusu, ulisema hapana, lakini sasa, mbele ya mkuu wetu, unasema mengi hivyo! Huo ni unafiki mkubwa!" Nilidhani mshirika wangu na mimi tulikuwa na uhusiano wa amani, lakini alikuwa na maoni mengi sana kunihusu, ambalo lilithibitisha kuwa bado kulikuwa na kutoelewana kati yetu na kwamba uhusiano wetu haukuwa wa amani hata kidogo.

Ijumaa, 1 Juni 2018

"Siri ya Utauwa: Mfuatano" (6) - Bwana Yesu ni Mwana wa Mungu au Mungu Mwenyewe

"Siri ya Utauwa: Mfuatano" (6) - Bwana Yesu ni Mwana wa Mungu au Mungu Mwenyewe

Imeandikwa waziwazi katika Biblia kwamba Bwana Yesu ni Kristo, kwamba Yeye ni Mwana wa Mungu. Lakini Umeme wa Mashariki unashuhudia kwamba Kristo aliyepata mwili ni dhihirisho la Mungu, kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe. Kwa hiyo Kristo aliyepata mwili ni Mwana wa Mungu? Au Yeye ni Mungu Mwenyewe? Mwenyezi Mungu asema, "'Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, ambaye anapendezwa Naye'.... Huyu alikuwa Mungu akijitolea ushuhuda Mwenyewe, ila kutoka katika mtazamo tofauti, ule wa Roho aliye mbinguni akitolea ushuhuda kupata Mwili Kwake. Yesu ni kupata mwili Kwake, si Mwanake mbinguni. Je, unaelewa? Je, maneno ya Yesu, 'Baba Yu ndani Yangu Nami ni ndani Yake,' hayaonyeshi kuwa Wao ni Roho mmoja? Na si kwa sababu ya kupata mwili kulikosababisha kutenganishwa Kwao kati ya mbinguni na duniani? Uhalisi ni kwamba Wao ni kitu kimoja; hata iweje, ni Mungu anajitolea ushuhuda Mwenyewe" (Neno Laonekana Katika Mwili).

Alhamisi, 31 Mei 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | "Siri ya Utauwa: Mfuatano" (5) | Kufahamu Umuhimu wa Mungu Kupata Mwili Mara Mbili

"Siri ya Utauwa: Mfuatano" (5) | Kufahamu Umuhimu wa Mungu Kupata Mwili Mara Mbili

Kupata mwili wa Mungu wa kwanza Alipigiliwa misumari msalabani, hivyo kuhitimisha kazi ya kuwakomboa wanadamu. Katika siku za mwisho, kupata mwili wa Mungu wa pili anaonyesha ukweli na Anafanya kazi Yake ya hukumu na kuadibu, Akiwaokoa wanadambu kabisa kutoka kwa miliki ya Shetani. Mungu kupata mwili mara mbili kuna umuhimu mkuu, kama tu anavyosema Mwenyezi Mungu, "Yesu alifanya hatua ya kazi ambayo ilitimiza tu kiini cha "Neno alikuwako kwa Mungu": Ukweli wa Mungu ulikuwako kwa Mungu, na Roho wa Mungu alikuwa na mwili na alikuwa asiyetenganishwa kutoka Kwake, yaani, mwili wa Mungu mwenye mwili ulikuwa na Roho wa Mungu, ambalo ni thibitisho kuu zaidi kwamba Yesu mwenye mwili alikuwa aliyepata mwili wa kwanza wa Mungu. Hatua hii ya kazi ilitimiza maana ya ndani ya "Neno lapata mwili," ilichangia kwenye maana ya kina zaidi ya "naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu,’…” (Neno Laonekana Katika Mwili).

70. Kazi ya Mungu ni Ya Hekima Sana!

Shiji    Jiji la Ma’anshan , Mkoa wa Anhui
Wakati wa kufanya kazi kwangu kama kiongozi katika kanisa, kiongozi wangu mara nyingi angeshirikiana mifano ya kushindwa kwa wengine ili kutumikia kama somo kwetu. Kwa mfano: Viongozi wengine walizungumza tu kuhusu elimu na mafundisho lakini walikosa kutaja upotovu wao au kuwasiliana kwa karibu kuhusiana na ufahamu wao wa jinsi ukweli unavyotumika kwa ukweli. Kama matokeo, viongozi kama hao mara nyingi hawakuwa na ufanisi katika miaka yao ya utumishi na hata wakawa wale ambao hufanya uovu na kumpinga Mungu. Viongozi wengine wangejionyesha, kujiinua na kujishuhudia wenyewe ili kulinda hadhi yao. Mwishowe, viongozi hao wangekuwa wapinga Kristo, wakiwaleta wadogo wao mbele yao katika mashindano ya wazi na Mungu. Viongozi wengine, wakati wa kazi yao, wangeonyesha nadhari kubwa mno kwa miili yao wenyewe, wakitamani wasaa wa burudani na bila kufanya kazi yoyote halisi kamwe. Viongozi hao walikuwa kama vimelea wanaotegemea faida za hadhi ya kanisa. Hatimaye, walifichuliwa na kuondoshwa. …