Fang Li Jiji la Anyang, Mkoa wa Henan
Hivi karibuni nilidhani nilikuwa nimeingia katika ubia wenye kuridhisha. Mshirika wangu na mimi tuliweza kujadili kitu chochote, wakati mwingine hata nikamwomba aonyeshe dosari zangu, na hatukupigana kamwe, hivyo nilidhani tulikuwa tumefanikisha ubia wenye kuridhisha. Lakini kama ukweli ulivyofichua, ubia wenye kuridhisha kwa kweli haukuwa kama kitu chochote nilichosadiki.
Siku moja katika mkutano, mshirika wangu alionyesha baadhi ya dosari zangu mbele ya mkuu wetu, akisema nilikuwa na kiburi, wa kutokubali ukweli, mwenye kudhibiti, mwenye kutiisha …. Kumsikia akisema hivyo kulinikasirisha mno, na nikawaza: "Jana nilikuuliza kama ulikuwa na maoni yoyote kunihusu, ulisema hapana, lakini sasa, mbele ya mkuu wetu, unasema mengi hivyo! Huo ni unafiki mkubwa!" Nilidhani mshirika wangu na mimi tulikuwa na uhusiano wa amani, lakini alikuwa na maoni mengi sana kunihusu, ambalo lilithibitisha kuwa bado kulikuwa na kutoelewana kati yetu na kwamba uhusiano wetu haukuwa wa amani hata kidogo.
Kama nimekabiliwa na ukweli wa mambo, sikuweza kujizuia tena kurejelea tabia yangu mwenyewe katika ubia huo: Katika mikusanyiko, ingawa ndugu yangu alifanya ushirika pia, alinena kidogo, kwa sababu nilizungumza kwa mingi ya mikutano na ni kwa nadra nilimpa nafasi ya kuongea; kazini kweli tulijadili matatizo yoyote yaliyotokea, lakini maoni yetu yalipotofautiana, daima nilishikilia maoni yangu na kuyakataa yake, na masuala yalitatuliwa wakati ndugu yangu alipoacha kubishana; kutoka kwa nje hakukuwa na ubishi au migongano kati yetu, lakini ndani daima kulihisi kama kulikuwa na kizuizi kati yetu, kitu kilichotusimamisha kuwa wazi kabisa. Ni hapo nilipotambua kwamba wakati sisi wawili tulionekana kuwa washirika waliofanya kazi pamoja, kwa kweli nilikuwa nikitoa maagizo yote, na kamwe hakupata nafasi ya kutimiza wajibu wake kweli. Nilidhani uhusiano wetu ulikuwa wa washirika wawili kukamilishana na kuwa sawa, lakini kwa kweli ulikuwa ni wa kiongozi na aliyeongozwa. Ukweli ulinifichulia kuwa kile nilichokifikiria kama ubia wenye kuridhisha yalikuwa tu ni matendo ya juujuu. Kwa hiyo, kwa hakika ubia wenye kuridhisha ni nini? Nilitafuta majibu ya swali langu katika neno la Mungu, na nilipata maneno haya, “Nyinyi mlio kwenye viwango vya juu husikia ukweli mwingi, na kuelewa mengi kuhusu huduma. Ikiwa ninyi watu ambao mnaratibu kufanya kazi katika makanisa hamjifunzi kutoka kwa kila mmoja, na kuwasiliana, kufidia mapungufu ya kila mmoja, mnaweza kujifunza masomo kutoka wapi? Mnapokutana na chochote, mnapaswa kushirikiana na kila mmoja, ili maisha yenu yaweze kufaidika. Na mnapaswa kushirikiana kwa makini kuhusu mambo ya aina yoyote kabla ya kufanya maamuzi. Ni kwa kufanya hivyo tu ndio mnakuwa na jukumu kwa kanisa na si kuwa wazembe. Baada ya kutembelea makanisa yote, mnapaswa kukutana na kushiriki juu ya masuala yote mnayotambua na matatizo mnayokabiliwa nayo kazini, na kuwasiliana kuhusu nuru na mwanga ambao mmepokea—huu ni utaratibu wa lazima wa huduma. Lazima mfikie ushirikiano wa upatanifu kwa kusudi la kazi ya Mungu, kwa manufaa ya kanisa, na kwa kuwachochea ndugu na dada kuendelea. Unashirikiana pamoja naye na anashirikiana na wewe, kila mmoja akimbadilisha mwingine, mkifikia matokeo bora ya kazi, ili kutunza mapenzi ya Mungu. Huu tu ndio ushirikiano wa kweli, na watu kama hao tu ndio wana kuingia kwa kweli” (“Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kupima kwa uangalifu maneno ya Mungu, moyo wangu kwa ghafla ulielewa. Ubia wa kweli una maana kwamba washirika wanaweka kazi ya kanisa kwanza; kwa maslahi ya kanisa na maisha ya ndugu wa kiume na wa kike, wanaweza kufanya ushirika wao kwa wao na kukamilisha udhaifu wa wao kwa wao, ili matokeo bora yaweze kufanikishwa katika kazi yao; hawana kutoelewana au chuki dhidi ya wao kwa wao na hawadumishi tofauti yoyote katika hadhi. Kwa kulinganisha tabia yangu mwenyewe na hiyo, nilihisi aibu na majuto yasiyosemeka. Kuangalia nyuma kwa tabia yangu, nilitambua sikuwahi kuzingatia maslahi ya kanisa kamwe, daima nilijiweka kwanza, niliongoza kwa kuegemea hadhi yangu na kwa uangalifu nilitunza sifa yangu mwenyewe na cheo, na niliogopa tu kwamba wengine wangenidunisha au kuniangalia kwa dharau, na ushirika wangu na ndugu wa kiume na wa kike haukuwa wa kukamilishana au kuendeshwa kwa njia ya usawa, kwa hiyo haukuwahi kufanikisha kamwe kusudi la kuingia kwa pamoja neno la Mungu, kwa kitegemeo cha pande mbili. Wakati kwa nje mshiriki wangu nami tulionekana kuwa tukijadili jinsi ya kufanya kazi yetu, katika moyo wangu sikuyakubali mawazo yake, na hatimaye niliyashikilia mawazo yangu mwenyewe badala ya kuzingatia kile kilichokuwa bora kwa kazi ya kanisa; ingawa wakati mwingine nilimuuliza aonyeshe dosari zangu, badala ya kuzikubali, daima nilibishana, nikatetea mambo, na kujitetea mwenyewe, mambo ambayo yalimwekea vikwazo na kumfanya awe na hofu sana ya kuzungumza nami wazi na kutotaka kutaja dosari zangu tena, ambayo yalisababisha kutoelewana kati yetu na kutugharimu uwezo wa kukamilisha kazi ya kanisa kwa dhamira moja. Miongoni mwa ndugu zangu wa kiume na wa kike nilitenda hata na kiburi zaidi na ubora, daima nikidhani kwamba nilikuwa kiongozi wao kwa sababu ufahamu wangu mkubwa wa ukweli ulinistahilisha kuwaongoza. Nikiwa nao, sikuonyesha kabisa unyenyekevu au utafutaji wa kweli, badala yake nikijifikiria kuwa stadi wa ukweli na kusisitiza kwamba kila mtu anisikilize. … Hapo ndipo nilipogundua kuwa ubia wangu katika huduma haukuwa na kiini chochote cha ubia, au kwa maneno mengine makubwa, nilikuwa nikijihusisha na udhalimu na udikteta. Kutenda jinsi hiyo kama kiongozi na mshirika sio tofauti na jinsi joka kubwa jekundu hushikilia mamlaka! Joka kubwa jekundu huweka udhalimu katika matendo, likisisitiza mamlaka ya mwisho katika vitu vyote na likihofia kusikiliza sauti ya umma au kutawala kupitia kanuni za kisiasa tofauti na zake. Na mimi, nikiwa na hadhi yangu ndogo niliyo nayo leo, nataka kuwa msimamizi wa eneo finyu ninalolidhibiti. Kama siku moja nitamiliki mamlaka, nitakuwaje tofauti na joka kubwa jekundu? Nikifikiri juu ya yote haya, kwa ghafla nilihisi hofu. Kuendelea jinsi hii kungekuwa hatari mno, na ikiwa singebadilika, mwisho wangu ungekuwa sawa na wa joka kubwa jekundu—kuadhibiwa na Mungu.
Baada ya kutambua yote haya, sikushikilia tena maoni yoyote dhidi ya ndugu yangu. Badala yake, nilikuwa na shukrani kwa Mungu kwa kunisaidia kujijua mwenyewe katika mazingira kama hayo na kwa kunionyesha hatari ndani yangu. Baadaye, niliposhirikishwa na ndugu zangu wa kiume na wa kike, nilijifunza kujishusha, kuwa na moyo wa kuyatunza mapenzi ya Mungu kuwajibika katika kazi yangu, na kusikiliza zaidi maoni ya wengine, na baada ya muda fulani, nilitambua kwamba aina hii ya matendo haikunipa tu ufahamu kamili zaidi mzima wa ukweli, pia ulinileta karibu na ndugu zangu wa kiume na wa kike na ulituruhusu kushiriki waziwazi zaidi. Na nikiwa na aina hizi za matunda kuonyesha, hatimaye nilielewa jinsi inavyoweza kuwa vizuri kufanya huduma ya mshirika kulingana na matakwa ya Mungu!
Ninashukuru kwa kupata nuru kutoka kwa Mungu, ambako hakukunisaidia tu kuelewa ubia wa kweli wenye kuridhisha, lakini hata zaidi kulinisaidia kuona hatari zilizofichika katika huduma yangu mwenyewe na mshirika wangu, na kulinionyesha kuwa wakati wanadamu wapotovu wanapotwaa mamlaka, matokeo yake ni sawa na joka kubwa jekundu. Natumaini ninaweza kuondosha sumu ya joka kubwa jekundu ndani yangu, kuingia katika huduma ya kweli ya ubia, na hatimaye kuwa mtu anayemtumikia Mungu ambaye analingana na moyo wa Mungu. Mwenyezi Mungu alisema,
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni