Mwenyezi Mungu alisema, Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu,
Sura ya 31. Jinsi ya Kufahamu Uenyezi na Utendaji wa Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Kitu hiki kinachoitwa mwanadamu kina uwezo wa kumsaliti Mungu, kwa hivyo unaweza kujua nini kutoka kwa hili? Baadhi ya watu huuliza: "Mungu alimuumba mwanadamu kwa hivyo Mungu hawezi kumzuia mwanadamu kumsaliti Yeye? Ni kwa nini mwanadamu bado ana uwezo wa kumsaliti Mungu? Je, Mungu si mwenyezi?" Hili ni tatizo, sio? Ni tatizo gani unaloweza kuona hapa katika suala hili? Mungu ana upande wa vitendo, lakini pia Ana upande wa uenyezi.