Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwendelezo-wa-Neno-Laonekana-katika-Mwili. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwendelezo-wa-Neno-Laonekana-katika-Mwili. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 14 Aprili 2018

2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu.


Matamshi ya Mwenyezi Mungu2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu.

2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu.
(Mwa 9:11-13) Na Nitalithibitisha agano langu nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika kuiharibu nchi. Na Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano Ninalofanya kati yangu na nyinyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, kwa vizazi vyote mpaka milele: Mimi Nauweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.

Baada ya Kuumba Viumbe Vyote, Mamlaka ya Muumba Yanathibitishwa na Kuonyeshwa kwa Mara Nyingine Tena Kwenye “Agano la Upinde wa Mvua”

Ijumaa, 13 Aprili 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Mamlaka ya Mungu (I)

Mwenyezi Mungu alisema, Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho? Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu? Inaweza kusemwa ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? Inaweza kusemwa kwamba maarifa na ufahamu huu wa Mungu ni maarifa ya hali halisi nzima ya Mungu, na kila kitu Anacho na alicho? La, bila shaka haiwezi kusemwa hivyo! Hii ni kwa sababu vikao hivi vya ushirika vilitupa tu ufahamu wa sehemu ya tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho—na wala si kila kitu, au uzima Wake wote. Vikao hivi vya ushirika vilikuwezesha wewe kuelewa sehemu ya kazi iliyowahi kufanywa na Mungu, na kupitia kwa hayo uliweza kuielewa tabia ya Mungu, na kile Anacho, na alicho, pamoja na mtazamo na kufikiria kuliko kila kitu ambacho Amefanya. Hata hivyo huu ni ufahamu tu wa moja kwa moja, wa matamshi, na katika moyo wako, unabakia kutojua ni kiwango kipi haswa ambacho ni kweli.

Jumanne, 10 Aprili 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)

Mwenyezi Mungu alisema, Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Leo Nawapa uchaguzi: Chagua kimoja. Mngependa kusikia kuhusu mada inayouhusu uzoefu wa maisha ya kibinafsi ya watu, au mngependa kusikia inayohusu kumjua Mungu Mwenyewe? Na kwa nini Ninawapa uchaguzi huu? Kwa sababu leo Ninafikiria kufanya ushirika nanyi juu ya mambo mapya kuhusu kumjua Mungu.