Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I
Mamlaka ya Mungu (I)
Mwenyezi Mungu alisema, Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho? Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu? Inaweza kusemwa ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? Inaweza kusemwa kwamba maarifa na ufahamu huu wa Mungu ni maarifa ya hali halisi nzima ya Mungu, na kila kitu Anacho na alicho? La, bila shaka haiwezi kusemwa hivyo! Hii ni kwa sababu vikao hivi vya ushirika vilitupa tu ufahamu wa sehemu ya tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho—na wala si kila kitu, au uzima Wake wote. Vikao hivi vya ushirika vilikuwezesha wewe kuelewa sehemu ya kazi iliyowahi kufanywa na Mungu, na kupitia kwa hayo uliweza kuielewa tabia ya Mungu, na kile Anacho, na alicho, pamoja na mtazamo na kufikiria kuliko kila kitu ambacho Amefanya. Hata hivyo huu ni ufahamu tu wa moja kwa moja, wa matamshi, na katika moyo wako, unabakia kutojua ni kiwango kipi haswa ambacho ni kweli.