Jumanne, 5 Machi 2019

Nyimbo za kuabudu | 53. Jinsi ya Kutafuta Nyayo za Mungu

Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu,
lazima tutafute, tutafute mapenzi ya Mungu,
tutafute maneno ya Mungu na matamshi ya Mungu,
tutafute maneno ya Mungu na matamshi ya Mungu.
Kwani palipo na maneno mapya ya Mungu,
pana sauti ya Mungu, sauti ya Mungu;
palipo na nyayo za Mungu,
pana matendo ya Mungu, pana matendo ya Mungu.
Palipo na maonyesho ya Mungu,
pana sura, sura ya Mungu,
na palipo na sura ya Mungu,
pana ukweli, njia, na uzima.
Mlipokuwa mkitafuta nyayo za Mungu,
nyote mlipuuza maneno kuwa “Mungu ni ukweli, njia, na uzima.”
Hivyo watu wengi wanapopokea ukweli,
hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu
na hata kukosa kutambua kuonekana kwa Mungu.
Ni kosa kubwa sana! Ni kosa kubwa sana!
Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulingana na dhana za mwanadamu,
sembuse Mungu kuonekana kwa ombi la mwanadamu.
Yeye anapofanya kazi Yake,
Yeye anafanya chaguo Lake, Yeye anafanya chaguo Lake, ana mipango Yake.
Zaidi ya hayo, ana malengo Yake mwenyewe, na mbinu Zake mwenyewe, mbinu Zake mwenyewe.
Anapofanya kazi Yake, hahitaji kujadiliana kazi Yake na mwanadamu,
kutafuta ushauri wa mwanadamu, sembuse kumuarifu kila mtu.
Hii ni tabia ya Mungu,
hii inafaa kujulikana na kila mtu.
Kama una hamu ya kushuhudia kuonekana wa Mungu,
kama uko tayari kufuata nyayo za Mungu,
basi kwanza lazima uvuke dhana zako mwenyewe.
Sharti usimfanyie Mungu madai ya kufanya hili ama lile,
wala hufai kumzuia Yeye katika mipaka yako mwenyewe
na kumwekea mipaka katika dhana zako mwenyewe.
Badala yake, unafaa kuuliza jinsi ya kutafuta nyayo za Mungu,
kukubali kuonekana kwa Mungu,
na jinsi unavyopaswa kutii kazi mpya ya Mungu;
hilo ndilo linapaswa kufanywa na mwanadamu, linapaswa kufanywa na mwanadamu.
Kwa kuwa hakuna mwingine, hakuna mwingine aliye ukweli,
na hakuna aliye na, aliye na ukweli,
mwanadamu anapaswa kutafuta, kukubali na kutii.
Kwa kuwa hakuna aliye ukweli, hakuna aliye ukweli,
na hakuna aliye na, aliye na ukweli,
mwanadamu anapaswa kutafuta, kukubali na kutii.
mwanadamu anapaswa kutafuta, kukubali na kutii.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni