Jumatano, 6 Machi 2019

wimbo wa kuabudu | 115. Napaswa Kuufikiria Moyo wa Mungu

Nimebarikiwa kusikia sauti ya Mungu na kuletwa mbele Yake.
Kula na kunywa maneno ya Mungu, nimehudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo na kuona kuonekana kwa Mungu.
Kupitia hukumu na utakaso wa Mungu ni uinuaji Wake.
Ningewezaje, nilivyo mpotovu, kustahili kuona uso Wake?
Nikiwa na wokovu wa Mungu mbele yangu, uso wangu umelowa machozi ya joto.
Kama siwezi kulipiza upendo Wake basi nitakuwa na aibu sana kumtazama.
Kama nina dhamiri na akili kweli, kwa nini basi siwezi kufikiria mapenzi ya Mungu?
Badala yake, nina tamaa ya raha za kimwili na ninaishi chini ya ushawishi wa giza.
II
Mara nyingi mimi husumbuka na kushindwa kutekeleza wajibu wangu.
Tabia za Shetani ni imara sana na kweli ni ngumu sana kuziondoa.
Kutokuwa na ukweli lakini bado mwenye kiburi, mimi nimepungukiwa mantiki sana.
Nangoja kwa hamu hukumu zaidi kali ili nipate kubadili haraka.
Kuona wasiwasi wa Mungu, najitahidi kuwa bora.
Usafishaji wote ni wa kustahili ili kupata ukweli.
Ni kwa sababu tu ya upogoaji na ushughulikiaji Wake ndiyo naishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu.
Nimeonja baraka ambayo ni hukumu na kuadibu kwa Mungu.
III
Mungu amelipa gharama isiyopimika ili kutuokoa:
hukumu na majaribu, watu, matukio, na vitu vingi sana vinavyofanya huduma.
Kuwaokoa watu waliopotoka kama hao si jambo rahisi.
Kwa sababu ya hukumu ya Mungu na kuadibu, nimepata maisha mapya.
Ningewezaje kutomwaga machozi ya shukrani wakati baraka nyingi hivyo zinanijia?
Kufurahia upendo wote wa Mungu, ningewezaje kuishi kwa ajili yangu mwenyewe?
Faraja yangu ya pekee ni kuishi kumtukuza na kumshuhudia Mungu.
Napaswa kutafuta kwa nguvu zangu zote, kupata ukweli na kuwa mtu anayempenda Mungu.
Kuishi kwa kudhihirisha roho ya Petro wa sasa ni kwa kupendeza sana.
Moyo Wangu unafurahia katika kuuridhisha moyo wa Mungu na naishi kwa kudhihirisha maisha ya kweli.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni