Neno la Mungu | "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" (Sehemu ya Kwanza)
Mwenyezi Mungu anasema, "Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu.
Wale wasiofahamu hatua tatu za kazi watakosa kuelewa njia mbalimbali na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu; wale wanaoshikilia tu imara mafundisho ya dini yanayosalia kutoka katika hatua moja ya kazi ni watu wanaomwekea Mungu mipaka kwa mafundisho ya dini, na wale ambao imani yao kwa Mungu haina udhahiri na uhakika. Watu kama hao kamwe hawawezi kupokea wokovu wa Mungu."
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu ilianza tu baada ya mwanadamu kupotoshwa, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu pia ilianza tu punde mwanadamu alipopotoshwa. Kwa maneno mengine, usimamizi wa Mungu wa mwanadamu ulianza kutokana na kazi ya kumwokoa mwanadamu, na wala haukutokana na kazi ya kuiumba dunia. Hakungekuwa na kazi ya kumsimamia mwanadamu pasipo kuwepo na tabia potovu ya mwanadamu, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu ina sehemu tatu, badala ya hatua nne, au enzi nne. Hii tu ndio njia sahihi ya kutaja kazi ya Mungu ya usimamizi wa mwanadamu. Enzi ya mwisho itakapofikia kikomo, kazi ya kusimamia mwanadamu itakuwa imekamilika. Hitimisho la kazi ya usimamizi lina maana kuwa kazi ya kuwaokoa wanadamu wote imemalizika kabisa, na kwamba mwanadamu amefika mwisho wa safari yake. Pasipo kazi ya kuwaokoa wanadamu wote, kazi ya usimamizi wa wanadamu haingekuwapo, wala hakungekuwa na hatua tatu za kazi. Ilikuwa ni hasa kwa ajili ya upotovu wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu alihitaji wokovu kwa dharura, ndipo Yehova alikamilisha uumbaji wa dunia na kuanza kazi ya Enzi ya Sheria. Hapo tu ndipo kazi ya kumsimamia mwanadamu ilipoanza, kumaanisha kwamba hapo tu ndipo kazi ya kumwokoa mwanadamu ilipoanza. “Kumsimamia mwanadamu” haimaanishi kuongoza maisha ya mwanadamu aliyeumbwa upya duniani (ambapo ni kusema, mwanadamu ambaye bado hakuwa amepotoshwa). Badala yake, ni wokovu wa ubinadamu ambao umepotoshwa na Shetani, ambapo ni kusema kwamba, ni kubadilishwa kwa mwanadamu aliyepotoshwa. Hii ndiyo maana ya kumsimamia mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu haihusishi kazi ya kuiumba dunia, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu haijumuishi kazi ya kuumba ulimwengu, na inahusisha tu hatua tatu za kazi zilizo tofauti na uumbaji wa ulimwengu. Ili kuelewa kazi ya kumsimamia mwanadamu, ni muhimu kuwa na ufahamu wa historia ya hatua tatu za kazi—hili ndilo kila mtu anapaswa kulifahamu ili kuokolewa. Kama viumbe wa Mungu, mnapaswa kutambua kuwa mwanadamu aliumbwa na Mungu, na kufahamu chanzo cha upotovu wa mwanadamu, na, vilevile, kufahamu mchakato wa wokovu wa mwanadamu. Iwapo mnafahamu tu jinsi ya kutenda kulingana na mafundisho ili kupata neema ya Mungu, lakini hamna fununu jinsi Mungu anavyomwokoa mwanadamu, au ya chanzo cha upotovu wa mwanadamu, basi hili ndilo mnalokosa kama viumbe wa Mungu. Hupaswi kutoshelezwa tu na kuelewa kwa ukweli unaoweza kuwekwa katika vitendo, huku ukibakia kutojua upeo mpana wa kazi ya usimamizi ya Mungu—kama hivi ndivyo ilivyo, basi wewe ni mwenye kulazimisha kauli sana. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo hadithi ya ndani ya usimamizi wa Mungu wa mwanadamu, ujio wa injili ya dunia nzima, fumbo kubwa zaidi kati ya wanadamu, na pia ni msingi wa kueneza injili. Ukizingatia tu kuelewa ukweli sahili unaohusiana na maisha yako, na usijue lolote kuhusu hili, maajabu makuu zaidi na maono, basi maisha yako si ni sawa na bidhaa yenye kasoro, yasio na maana isipokuwa kuangaliwa?
Ikiwa mwanadamu huzingatia tu matendo, na kuona kazi ya Mungu na hekima ya mwanadamu kama za upili, basi si ni sawa na kuwa mwerevu kwa kiasi kidogo cha pesa na mjinga kwa kiasi kikubwa cha pesa? Lile ambalo sharti ulijue, lazima ulijue, na kile unachostahili kuonyesha kwa vitendo, lazima ukionyeshe kwa vitendo. Ni hapo tu ndipo utakapokuwa mtu anayejua kufuata ukweli. Siku yako ya kueneza injili itakapowadia, ikiwa utaweza kusema tu kuwa Mungu ni Mkuu na Mwenye haki, kuwa ni Mungu Mkuu, Mungu ambaye hapana mwanadamu yeyote mkuu anayeweza kujilinganisha naye, na kuwa hakuna aliye juu zaidi wa kumpiku..., kama waweza tu kusema maneno haya yasiyofaa na ovyo, na kabisa huwezi kunena maneno yenye umuhimu zaidi, na yaliyo na kiini, kama huna lolote la kusema kuhusu kumjua Mungu, ama kazi ya Mungu, na zaidi ya hapo, huwezi kuelezea ukweli, au kutoa kile ambacho kinakosekana kwa mwanadamu, basi mtu kama wewe hana uwezo wa kutekeleza wajibu wake vyema. Kumshuhudia Mungu na kueneza injili ya ufalme si jambo rahisi. Lazima kwanza uwe na ukweli, na maono yatakayoeleweka. Unapokuwa na uwazi wa maono na ukweli wa masuala tofauti tofauti ya kazi ya Mungu, moyoni mwako unapata kujua kazi ya Mungu, na bila kujali anayoyafanya Mungu—iwe ni hukumu ya haki ama kusafishwa kwa mwanadamu—unamiliki maono makuu kama msingi wako, na unamiliki ukweli sahihi wa kuonyesha kwa matendo, basi utaweza kumfuata Mungu hadi mwisho. Lazima ujue kuwa bila kujali kazi ambayo Yeye anatenda, lengo la kazi ya Mungu halibadiliki, kiini cha kazi Yake hakibadiliki, na mapenzi Yake kwa mwanadamu hayabadiliki. Bila kujali maneno Yake ni makali namna gani, haijalishi mazingira ni mabaya kiasi gani, kanuni za kazi Yake, na nia Yake ya kumwokoa mwanadamu hayatabadilika. Mradi tu si ufunuo wa mwisho wa mwadhamu au hatima ya mwanadamu, na si kazi ya awamu ya mwisho, au kazi ya kutamatisha mpango wote wa usimamizi, na mradi tu ni wakati Anapomfinyanga mwanadamu, basi kiini cha kazi Yake hakitabadilika: Daima kitakuwa wokovu wa mwanadamu. Hili linapaswa kuwa msingi wa imani yenu katika Mungu. Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu. Punde unapofahamu lengo la hatua hizi tatu za kazi, basi utafahamu jinsi ya kuthamini umuhimu wa kila hatua ya kazi, na utatambua jinsi ya kutenda ili kutosheleza shauku ya Mungu. Iwapo utaweza kufikia hatua hii, basi hili, ono kubwa kuliko yote, litakuwa msingi wako. Unapaswa kufuata sio tu njia rahisi za matendo, ama ukweli wenye undani, lakini unapaswa kuunganisha maono na matendo, ili kwamba kuwe na ukweli unaoweza kuwekwa kwenye vitendo, na maarifa yaliyo na msingi wa maono. Ni hapo tu ndipo utakapokuwa mtu anayefuatilia ukweli.
kutoka kwa : Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni