Ijumaa, 26 Aprili 2019

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | 12. Vigezo vya Mtu Aliye Mwema Kwa Kweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ushuhuda,

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | 12. Vigezo vya Mtu Aliye Mwema Kwa Kweli

Moran Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong

Tangu nilipokuwa mtoto, siku zote nilishikiza umuhimu mkubwa kwa jinsi watu wengine walivyoniona na ukadiriaji wao kwangu. Ili niweze kupata sifa kutoka kwa wengine kwa kila kitu nilichokifanya, sikubishana na yeyote asilani wakati wowote kitu chochote kilichoibuka, ili kuepuka kuharibu picha nzuri watu wengine walikuwa nayo kwangu. Baada ya kuikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, niliendelea kwa njia hii, nikizingatia kwa kila njia iwezekanayo picha nzuri ambayo ndugu zangu wa kiume na wa kike walikuwa nayo kwangu.

Alhamisi, 25 Aprili 2019

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | 9. Kuzing’uta Pingu za Roho

 Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | 9. Kuzing’uta Pingu za Roho

Wu Wen Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Nilikuwa mtu dhaifu na mwenye tabia nyepesi kuhisi. Wakati sikumwamini Mungu, mara kwa mara ningejihisi mwenye huzuni na masikitiko kutokana na mambo yaliyokuja katika maisha. Kulikuwa na nyakati nyingi kama hizi, na siku zote nilihisi kwamba maisha yangu yalikuwa magumu; hapakuwa na furaha, hamkuwa na ridhisho moyoni mwangu ya kuzungumzia. Uchungu huu ulikuwa tu kama pingu zilizonifunga kabisa kila mara, zikinifanya niwe mwenye huzuni. Ilikuwa tu baada kumwamini Mwenyezi Mungu ndipo nilipata kiini cha matatizo ndani ya maneno ya Mungu na nikapata uhuru polepole.

Jumatano, 24 Aprili 2019

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | 8. Ufahamu Kiasi Kuhusu Kuokolewa

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo | 8. Ufahamu Kiasi Kuhusu Kuokolewa

Lin Qing Jijini Qingzhou, Mkoa wa Shandong
Kwa miaka hii mingi ya kumfuata Mungu, nimeacha familia yangu na raha za mwili, na nimekuwa na shughuli nyingi siku nzima nikitimiza wajibu wangu kanisani. Kwa hiyo niliamini: Mradi tu nisiache kazi yangu katika kanisa, nisimsaliti Mungu, nisiache kanisa, na kumfuata Mungu hadi mwisho, nitahurumiwa na kuokolewa na Mungu. Niliamini pia kuwa nilikuwa nikitembea katika njia ya wokovu na Mungu, na yote niliyokuwa niyafanye ni kumfuata Yeye mpaka mwisho.

Jumanne, 23 Aprili 2019

5. Maneno ya Mungu Yaliniongoza Kutoka Katika Matatizo

5. Maneno ya Mungu Yaliniongoza Kutoka Katika Matatizo

Xiao Rui Mji wa Panzhihua, Mkoa wa Sichuan
Nilipokuwa nikihubiri injili nilikutana na viongozi wa dini ambao walisema uongo ili kupinga na kuvuruga, na kuwaita polisi. Hili lilisababisha wale niliokuwa nikihubiria kutothubutu kuwasiliana nasi, na wale ambao walikuwa tu wameikubali injili kutoweza kuwa na imani katika kazi ya Mungu. Nilipofanya kazi kwa bidii sana lakini matokeo yalikuwa duni, nilifikiri: kazi ya Kiinjili ni ngumu sana kutekeleza. Lingekuwa jambo la kustaajabisha sana kama Mungu angeonyesha miujiza kiasi na kuwaadhibu wale ambao husema uongo pamoja na wale ambao kwa uzito kabisa humpinga Mungu kuwaonyesha wale ambao wamedanganywa.

Jumatatu, 22 Aprili 2019

Baraka za Mungu: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ukweli,

Baraka za Mungu: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

                                              Na Bong, Philippines


“Mwalimu mkuu, tafadhali mpe mwanangu fursa na kumruhusu afanye mtihani!” Macho ya mama yangu yalimsihi mwalimu mkuu alipokuwa akizungumza kwa sauti ya kutetemeka kidogo.

Bila kuonyesha hisia, mwalimu mkuu akasema, “Hapana, shule ina kanuni. Mtoto anaweza kufanya mtihani tu wakati ada ya mtihani imelipwa!”

Mama yangu alionekana mwenye kutayahari na kumsihi mwalimu mkuu, akisema, “Mwalimu mkuu, najua hili ni gumu sana kwako shuleni pia, lakini nina watoto wengi na sisi huweza kuishi kwa shida tu.

Jumapili, 21 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 104

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 104

Watu, matukio na vitu vyote nje Yangu vitakufa na kuwakatika hali ya kutokuwepo, ilhali watu, matukio na vitu vyote vilivyo ndani Yangu vitapata kila kitu kutoka Kwangu na kuingia katika utukufu pamoja na Mimi, kuingia katika Mlima Wangu Sayuni, makazi Yangu, na kuishi pamoja kwa amani nami milele. Niliumba vitu vyote mwanzoni na Nitamaliza kazi Yangu mwishowe, na pia Nitatawala milele kama Mfalme. Katikati, pia Ninaongoza na kuutawala ulimwengu mzima.