Jumamosi, 6 Aprili 2019

Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”

Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja

Mwenyezi Mungu anasema, “Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Kuzaliwa na kufa kwa nani kulitokana na kuchagua kwao? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake?

Ijumaa, 5 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sisitiza Uhalisi Zaidi

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sisitiza Uhalisi Zaidi

Kila mtu ana uwezekano wa kukamilishwa na Mungu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuelewa ni huduma gani kwa Mungu inayofaa zaidi makusudi ya Mungu. Watu wengi hawajui kumwamini Mungu humaanisha nini na hawajui kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu. Yaani, watu wengi zaidi hawana ufahamu wa kazi ya Mungu au lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu. Hadi leo, watu wengi zaidi bado wanadhani kumwamini Mungu kunahusu kwenda mbinguni na roho zao kuokolewa.

Alhamisi, 4 Aprili 2019

“Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele”

Matamshi ya Mungu | “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele”

Mwenyezi Mungu anasema, “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia.

Jumatano, 3 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Tabia ya Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Tabia ya Haki ya Mungu
Kwa vile sasa mmesikiliza ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Ninao ujasiri kwamba mmejihami vilivyo na mseto wa maneno kuhusu suala hili. Kiwango unachoweza kukubali, kufahamu, na kuelewa vyote hivi vinategemea na jitihada zipi utakazotumia. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kutazamia suala hili kwa dhati; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia shingo upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kujua Mungu kwa uzima wake?

Jumanne, 2 Aprili 2019

Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance

Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance
Safi na mwaminifu, kama mtoto bila hatia, mchangamfu na mwenye nguvu za ujana, wao ni kama malaika wanaokuja ulimwenguni. Bila udanganyifu, na mioyo iliyo wazi tu, wao ni waadilifu. Wanatoa mioyo yao kwa Mungu na kupata imani Yake. Wao ni watu waaminifu ambao Mungu anapenda. Kuacha maneno ya Mungu yatuongoze kila siku, tumebarikiwa na Roho Mtakatifu anatuongoza. Tunakubali uchunguzi wa Mungu, tunaishi mbele Yake. Kumpenda Mungu kweli ni kuwa na furaha.

Jumatatu, 1 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumfuata Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Utakatifu wa Mungu (II)

Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu “Upendo Safi Bila dosari.”)
1. “Upendo” unarejelea hisia ambayo ni safi na bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali.