Sura ya 5 Lazima Uujue Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili
5. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili.
Maneno Husika ya Mungu:
Umuhimu wa kupata mwili ni kwamba mtu wa kawaida Anatekeleza kazi ya Mungu Mwenyewe; yaani, kwamba Mungu Anatekeleza kazi Yake ya uungu kwa wanadamu na hivyo kumshinda Shetani. Kupata mwili kunamaanisha kwamba Roho wa Mungu Anakuwa Mwili, yaani, Mungu Anakuwa mwili; kazi Anayoifanya katika mwili ni kazi ya Roho, inayothibitika katika mwili, na kuonyeshwa kwa mwili.
Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo
Mwenyezi Mungu anasema, "
Uzima wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii kumefanyika kulingana na hali zinazozunguka ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji.
Mwenyezi Mungu anasema, "
Siku hizi, binadamu wote, kwa viwango vinavyotofautiana, wameingia katika hali ya kuadibu. Kama tu alivyosema Mungu, “Naenda mbele na binadamu sako kwa bako.” Hii ni kweli kabisa, lakini watu bado hawawezi kulielewa kabisa wazo hili.
Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho.