Mwenyezi Mungu anasema, "
Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Nilichunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani.
Mwenyezi Mungu anasema, " Ufunuo Wangu unapofika kilele chake, na hukumu Yangu inapomalizika, utakuwa wakati ambapo watu Wangu wote wanafichuliwa na kufanywa wakamilifu. Nyayo Zangu hukanyaga kila pembe ya ulimwengu dunia katika hali ya kutafuta kwa kudumu wale wenye kupendeza moyo Wangu na wanafaa kwa matumizi Yangu.
Maonyesho yaMungu| "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu"
Mwenyezi Mungu anasema, "Sababu mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana!
Mwenyezi Mungu anasema, "
Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu; hii ni kwa kuwa asili potovu ya mwanadamu inatokana kabisa na Shetani na asili ya mwanadamu imemilikiwa na kupotoshwa na Shetani. Yaani, mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa uovu na ubaya wake. Mwanadamu hakui katika ulimwengu wa ukweli au mazingira matakatifu, na aidha haishi katika mwanga.