Ijumaa, 19 Januari 2018

Sura ya 32. Ni Watu wa Aina Gani Watakaoadhibiwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 32. Ni Watu wa Aina Gani Watakaoadhibiwa | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kukufuru na kashfa dhidi ya Mungu ni dhambi ambayo haitasamehewa kwa enzi hii na enzi ijayo na wale wanaofanya dhambi hii hawatazaliwa upya kamwe. Hili linamaanisha kwamba tabia ya Mungu haiwezi kuvumilia kosa la wanadamu. Watu wengine wanaweza kusema maneno yasiyofaa au maneno mabaya wakati hawaelewi, au wanapodanganywa, kuwekewa vikwazo, kudhibitiwa, au kukandamizwa na wengine. Lakini wanapokubali njia ya ukweli katika siku zijazo watajawa na majuto.

Sura ya 39. Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Kanisa
Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sura ya 39. Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Ni nini mnafahamu kuhusu mabadiliko katika tabia? Asili ya mabadiliko katika tabia na mabadiliko katika mwenendo ni tofauti, na mabadiliko katika matendo pia ni tofauti—yote ni tofauti kwa asili. Watu wengi wanaweka mkazo maalum kwa tabia yao katika imani yao kwa Mungu, matokeo yakiwa mabadiliko yanayofanyika katika mienendo yao. Baada ya kuamini katika Mungu, wanakoma kubishana na wengine, wanakoma kupigana na watu na kuwatukana, wanakoma kuvuta sigara na kunywa, hawaibi mali ya uma—hata iwe msumari ama kipande cha mbao pekee—na hata wanaenda kiasi cha kutoipeleka kotini wanapopata hasara ama wamekosewa.

Alhamisi, 18 Januari 2018

Sura ya 11. Kutatua Asili na Kutenda Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 11. Kutatua Asili na Kutenda Ukweli

Maneno ya Mwenyezi Mungu
1. Uhusiano Kati ya Ubinadamu na Uwezo wa Kutenda Ukweli
Watu husema kuwa kutenda ukweli ni vigumu kabisa. Basi mbona watu wengine wanaweza kutenda ukweli? Watu wengine husema ni kwa sababu kwa asili wanaipokea kazi ya Roho Mtakatifu ikifanya kazi juu yao, na pia kwa sababu ni wazuri kiasili. Hoja hii ina kiwango fulani cha mantiki. Watu wengine ni wazuri kiasili; wana uwezo wa kutenda ukweli. Ubinadamu wa watu wengine ni mnyonge, hivyo ni vigumu kwao kutenda ukweli; hii inamaanisha kuwa watakumbana na matatizo fulani.

Sura ya 10. Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 10. Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata
Maneno ya Mwenyezi Mungu
1. Kama hali ya Watu Ni Ya Kawaida Inategemea na Kama Wanapenda Ukweli au La
Watu wengi wameibua suala lifuatalo: Baada ya ushirika wa juu, wanahisi wazi kabisa, wanakuwa na nguvu zaidi, na hawana hisia hasi—lakini hali kama hiyo inabaki tu kwa karibu siku kumi, ambapo baadaye hawawezi kudumisha hali ya kawaida. Suala ni nini? Je mmewahi kujiuliza kinachosababisha hili? Mbona hali zenu ni nzuri sana katika siku hizo takriban kumi za kwanza? Wengine wanasema kuwa hili ni tokeo la kutolenga ukweli.

Jumatano, 17 Januari 2018

5. Ole Wao Wale Wamsulubishae Mungu Mara Nyingine Tena

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, msalaba

5. Ole Wao Wale Wamsulubishae Mungu Mara Nyingine Tena

Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili katika nchi ya China kufanya kazi, na Ameonyesha mamilioni ya maneno, Akishinda na kuokoa kundi la watu kwa neno Lake na kuikaribisha enzi mpya ya hukumu ikianza na nyumba ya Mungu. Leo, kuenea kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho kumefikia kilele chake katika China Bara. Wengi wa watu katika Kanisa Katoliki na madhehebu yote ya Kikristo na makundi ya kidini ambayo yanafuatilia ukweli wamerudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.

Sura ya 29. Mtu Lazima Ajue Jinsi Ambayo Mungu Hufanya Kazi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Sura ya 29. Mtu Lazima Ajue Jinsi Ambayo Mungu Hufanya Kazi

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Mungu, iwe ni kwa mwili au kwa Roho, yote inafanywa kulingana na mpango wa usimamizi. Kazi Yake haifanywi kulingana na kama ni ya umma au ya kibinafsi, au kulingana na mahitaji ya mwanadamu—inafanywa kikamilifu kulingana na mpango wa usimamizi. Hatua hii ya kazi haiwezi kufanywa kwa njia yoyote ya zamani: Inapaswa kukamilika juu ya msingi wa hatua mbili zilizopita za kazi.