Mwenyezi Mungu alisema, Kwa watu,
Mungu ni mkuu mno, mwenye utele mno, wa ajabu mno, Asiyeeleweka mno; machoni pao, maneno ya Mungu hupaa juu, na huonekana kama kazi bora sana ya ulimwengu. Lakini kwa vile watu wana kasoro nyingi sana, na akili zao ni za kawaida sana, na, zaidi ya hayo, kwa kuwa uwezo wao wa kukubali ni haba mno, bila kujali vile Mungu hunena maneno Yake kwa dhahiri, wanabaki palepale bila kutikisika, kana kwamba wana ugonjwa wa akili. Wanapokuwa na njaa, hawaelewi kwamba lazima wale, wanapokuwa na kiu, hawaelewi kwamba lazima wanywe maji; wanaendelea tu kupaaza sauti na kupiga yowe, kana kwamba kuna dhiki isiyoelezeka katika kina cha roho zao, lakini hawawezi kuzungumza kuihusu.