Jumapili, 4 Februari 2018

Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 94. Wale Ambao Hawawezi Kuishi Mbele Ya Mungu Daima Ni Wasioamini
Mwenyezi Mungu alisema, Nguzo inapopandishwa kidogo, mnaweza kupiga hatua kidogo. Si jambo baya kuwa na mahitaji ya juu kutoka kwenu na wala si jambo baya kuwauliza maswali magumu. Lengo ni kuwafanya muwe na ufahamu zaidi juu ya elimu na maarifa ya kawaida ya kipengele cha weledi cha wajibu wenu.[a] Huenda labda nyinyi bado hulalamika katika nyoyo zenu, mkisema: "Tumejifunza mambo mengi mazuri lakini Mungu huwa hayataji kamwe au kuturuhusu kuyatumia. Kwa hiyo hatuthubutu kuyataja au kuyatumia. Je, na kama yakikanushwa mara tu tunapoyatumia? Na je, tukikosolewa? "Sasa Nawaambieni kwamba mnaweza kuyatumia mambo haya kwa ujasiri. Lakini ni lazima mpitie ukaguzi wa ndugu zenu wa kiume na wa kike. Usiwe wa kujidai, na kusema: "Mungu amesema wakati huu tunaweza kutumia mambo haya kwa ujasiri, kwa hiyo tutatumia mambo haya kwa ujasiri." Kuwa na ujasiri sio kuenea pote au kuwa wenye dharau. Lazima kuwe na mipaka ya kuwa na ujasiri, ni lazima kukubaliane na kanuni, na ndugu wa kiume na wa kike wanapaswa kulifikiria kuwa linafaa. Mtu fulani akisema, "Hili halikubaliki," basi si unahitaji kulibadilisha? Je, watu wakaidi ni watu wema? (Hapana.) Haishauriwi kuwa hivyo. Ni lazima usikilize maoni ya wengine, na unapowasikia wakisema hivi, unasema, "Uko sawa. Ni lazima nilibadilishe." Baada ya kulibadilisha, watu wengine husema: "Uko karibu hapo, nahisi vyema kuhusu hili. Liko sawa, limefaulu." Safi sana! Kwa kufanya mambo kwa njia hii, kipengele kimoja ni kwamba mnaweza kuingia kwa kina katika kipengele cha weledi, na muwe wakomavu na wenye uzoefu; kipengele kingine ni kwamba nyinyi pia mna uwezo wa kujifunza mambo mengi; na bado kipengele kingine ni kwamba mmejifunza somo. Unapokabiliwa na masuala, hupaswi kujidai, ukifikiri, "Nina kauli ya mwisho. Hamna sifa ya kuzungumza. Ninaelewa kanuni, nyinyi mnaelewa nini? Hamuelewi, ninaelewa!" Huku ni kujidai. Kuwa wa kujidai ni tabia potovu ya kishetani; si kitu kilicho ndani ya ubinadamu wa kawaida. Kwa hiyo, ni nini maana ya kutokuwa wa kujidai? (Kupata mapendekezo kutoka kwa kila mtu, na kila mtu kuyapima pamoja.) Wakati kila mtu anapoliidhinisha, na kila mtu anapokubaliana nalo, basi mmefanya kazi nzuri. Mradi baadhi ya watu au kikundi cha watu hudakiza kipingamizi, basi ni lazima muwe mahsusi zaidi kuhusu kipengele cha weledi. Ni lazima msijifanye kutotambua na kusema: "Nani? Aliyedakiza nini? Ni nini kinachoendelea? Je, wewe ndiye unayelielewa hili au ni mimi? Je, unaelewa hili vyema kuniliko? Unaelewa nini? Huelewi!" Hii ni tabia mbaya, sivyo? Ijapokuwa aliyedakiza kipingamizi huenda asielewe vizuri sana na anaweza kuwa mlei, na unaweza kuwa na haki na kile ulichokifanya kinaweza kuwa sahihi, tatizo hapa ni tabia yako. Kwa hiyo ni nini maonyesho na vitendo sahihi vinavyokubaliana na kanuni na kukubaliana na ukweli? Unasema: "Tatizo ni nini? Acha niangalie. Sio mimi tu, lakini kila mtu anaangalia. Wale ambao wana mapendekezo fulani kuhusu kipengele hiki au utambuzi fulani ndani yake, au ambao wana uzoefu fulani katika kipengele hiki, hebu sote tuangalie pamoja na tuweze kuzungumza juu yake. "Ikiwa kila mtu huamini kweli kuwa kufanya kitu kwa njia hii ni vibaya, kwamba kuna shida kidogo hapa, na unatazama mara moja na huwezi kuona tatizo, unatazama mara mbili na bado huwezi kuliona, kisha unaangalia mara tatu au mara nne na unavyozidi kuangalia ndivyo unavyozidi kuona kuna shida, basi hili kwa kweli ni tatizo. Na lazima ulisahihishe, lifanye liwe zuri na uombe mawazo ya kila mtu. Je, hili ni jambo jema au jambo baya? (Ni jambo jema.) Unaomba mawazo ya kila mtu, kila mtu analizungumzia, unashirikiana pamoja na Roho Mtakatifu anakupa nuru; unafuata hilo, na tatizo linarekebishwa ipasavyo. Kila mtu huangalia na kusema, "Hilo ni sawa, na ni bora zaidi kuliko hapo awali!" Je, si huu ni mwongozo wa Mungu? Hili ni jambo kubwa! Unapofanya mambo kwa njia hii, kama wewe hujidai, unapoacha mawazo yako mwenyewe na fikira zako mwenyewe, na unapotenda ukweli, unanyenyekea na kusikiliza mawazo ya wengine, kisha ni nini hutokea? Wewe hupata fursa ya Roho Mtakatifu kufanya kazi kwako na Roho Mtakatifu hukupatia nuru. Nini hutokea wakati Roho Mtakatifu anapokupatia nuru? Umejifunza kitu kingine cha weledi. Je, si hiki ni kitu chema?
Mara unapokuwa umepitia hili, wewe hufikiri, "Ninapokabiliwa na masuala, ni lazima nisijidai. Kila mtu hunichukia ninapojidai." Wakati kila mtu anapomchukia mtu fulani, Mungu humchukia? (Ndiyo, Yeye humchukia.) Unajifunza somo, kweli? Unapotenda kwa njia hii daima, kipengele kimoja ni kwamba utaona maendeleo katika hali ya weledi ya wajibu wako, na Mungu atakupa nuru na kukubariki; kipengele kingine ni kwamba utakuwa na njia ya kufuata katika kutenda ukweli, utajua jinsi ya kutenda ukweli, hatua kwa hatua utakuja kuelewa kanuni na kupata njia, utajua jinsi ya kufanya mambo kwa namna ambayo itasababisha kupata nuru ya Mungu na uongozi, ni njia zipi za kufanya mambo ambazo humsababisha Mungu kukupuuza au kukuchukia, na jinsi ya kufanya mambo kwa njia ambayo inaweza kubarikiwa na Mungu. Watu wanapopata baraka za Mungu na nuru, kuna furaha au huzuni ndani ya mioyo yao? Kuna furaha. Unapokuja kuwajibika kwa kile ambacho umekifanya mbele ya Mungu, utapata furaha na utafikiri, "Nilikifanya vizuri." Ndani yako utajisikia mwenye amani na furaha. Hisia hii ya amani na furaha hutolewa kwako na Mungu, na ni kuchochea ulikopewa na Roho Mtakatifu. Ikiwa hutendi hili lakini daima huhimili kwa njia zako mwenyewe, ukisema, "Sitamsikiliza mtu yeyote. Hata nikisikiliza, nitaonekana tu kusikiliza na sitabadilika. Nitafanya mambo kwa njia hii, ninahisi niko sawa na nahisi nimethibitishwa kabisa, "ni nini kitakachotokea? Huenda kuwa umethibitishwa na huenda kusiwe na kosa katika kile ufanyacho, huenda hujafanya makosa yoyote na huenda ukaelewa kipengele cha weledi vyema zaidi kuliko wengine, lakini mara unapofanya aina hizi za maonyesho na kutenda kwa njia hii, wengine wataona na watasema: "Tabia ya mtu huyu si nzuri. Unapokabiliwa na masuala, huwa hawakubali lakini hupinga kitu chochote mtu mwingine yeyote anachosema, kama kiko sahihi au la. Mtu huyu huwa hakubali ukweli." Watu wanaposema wewe hukubali ukweli, Mungu atafikiri nini? Je, Mungu anaweza kuona maonyesho haya yako? Bila shaka, Mungu anaweza kuyaona. Mungu hachunguzi tu chokomeani mwa moyo wa mwanadamu, Yeye pia huangalia kila kitu usemacho na kufanya wakati wote na mahali pote. Na Anapoona mambo haya, Yeye hufanya nini? Yeye husema: "Wewe umefanywa mgumu. Uko jinsi hii katika hali ambapo wewe uko sawa, na uko jinsi hii pia katika hali ambapo umekosea. Bila kujali uko katika hali gani, kila kitu unachofichua na kuonyesha ni kupingana na upinzani. Hukubali hata kidogo mawazo au mapendekezo ya mtu yeyote mwingine. Moyo wako unapingana kabisa, kukataa na kutokubali mawazo ya wengine. Wewe ni mgumu sana!" Ni kwa njia gani unakuwa mgumu? Kuwa kwako mgumu ni kwamba maonyesho yako sio njia mbaya ya kufanya mambo au tabia mbaya, lakini kwa usahihi zaidi ni ufichuzi wa tabia yako. Je, tabia yako imefichua nini? Unauchukia ukweli na una uhasama mintarafu ya ukweli. Na wakati umefafanuliwa kama mtu ambaye ana uhasama mintarafu ya ukweli, machoni mwa Mungu uko katika shida. Si zaidi ya haya, kila mtu atasema, "Mtu huyu ana tabia mbaya, yeye ni mkaidi na mwenye kiburi. Mtu huyu ni vigumu kukubaliana naye, hana matendo ya ukweli na hapendi ukweli. Hajawahi kuukubali ukweli." Si zaidi ya haya, kila mtu atakutathmini kwa njia hii; lakini tathmini hii inaweza kuamua jaala yako? Watu hufanya tathmini yako, lakini hili haliwezi kuamua jaala yako. Lakini kuna jambo moja ambalo hupaswi kulisahau: Mungu huuchunguza moyo wa mwanadamu, na wakati huo huo Yeye huangalia kila kitu ambacho mtu husema na kufanya. Mungu akimfafanua mtu kwa kusema, "Una uhasama mintarafu ya ukweli," Yeye hamfafanui tu kwa kusema, "Mtu huyu ana tabia potovu kidogo na kwa kiasi kidogo si mtiifu," bali kwa usahihi zaidi Yeye anasema, "Una uhasama mintarafu ya ukweli," hii ni hoja kubwa au hoja ndogo? (Ni hoja kubwa.) Na hili husababisha shida? (Ndiyo.) Je, hili huleta shida gani? Shida hii haiko katika jinsi watu wengine hukuona au jinsi wanavyokutathmini, lakini liko katika jinsi Mungu anavyoona tabia yako potovu ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli. Hivyo ni vipi basi Mungu huona tabia yako ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli? Je, unajua? Mungu husema, "Ana uhasama mintarafu ya ukweli na hapendi ukweli." Je, Mungu huliona kwa jinsi gani? Ukweli hutoka wapi? Ukweli humwakilisha nani? (Humwakilisha Mungu.) Hivyo fikiria hili: Mungu anapaswa kuonaje tabia ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli? Je, Yeye atalionaje? (Mungu huliona kuwa na uhasama kwelekea Kwake na kama adui Yake.) Na hili ni jambo zito? Mtu aliye na uhasama mintarafu ya ukweli ana uhasama mintarafu ya Mungu. Kwa nini Ninasema kuwa ana uhasama mintarafu ya Mungu? Je, huwa anamtukana Mungu? La. Huwa anampinga Mungu bayana? La. Je, huwa anamshushia Yeye hadhi kisiri? La. Hivyo kufichua tabia ya jinsi hii huwaje uhasama mintarafu ya Mungu? Je, si huu wote ni msukosuko wa bure? Kuna kitu ndani yake, sivyo? Unajua ni kitu gani? Mtu fulani ana tabia hii na hufichua aina hii ya tabia wakati wote na katika maeneo yote na, zaidi ya hayo, yeye huitegemea ili kuishi na haachi kamwe njia hii ambayo kwayo yeye huishi na kufanya mambo, na haitupi kamwe. Wewe hutegemea mambo na tabia hii ili kuishi, na wakati hakuna kitu kinachotokea, ikiwa mtu atasema kuwa una uhasama mintarafu ya Mungu, unaweza kukubaliana naye? Huwezi kukubaliana naye. Hata hivyo, matatizo yanapochipuka, unapokuwa na aina hii ya tabia, wewe huifichua wakati wote na mahali pote? Kwa hiyo hii ni tabia gani? Ni tabia ambayo ni uhasama mintarafu ya Mungu na uhasama mintarafu ya ukweli. Unayasaili maneno ya Mungu, unayachangua, unayachambua na kuyatilia shaka. Inamaanisha nini unapofanya mambo haya? Inamaanisha kwamba unaposikia maneno ya Mungu, wewe hufikiria, "Je, haya ni maneno ya Mungu? Sifikiri huu ni ukweli na sifikiri yote ni lazima yawe ni sahihi." Tabia yako imefichuliwa, ni kweli? Je, una uwezo wa kutii wakati unapofikiria jinsi hii? Hakika huna uwezo. Na kama huna uwezo wa kutii, Mungu bado ni Mungu wako? Hapana, Yeye si Mungu wako. Je, wewe basi humuona Mungu kama nini? Kama chombo cha kujifunza na cha shaka, na hata kama tu mtu wa kawaida, kama mtu mwenye tabia potovu kama tu mtu. Je, si hili linaletwa na tabia potovu ya mtu?
Wakati mtu amekwenda mbali hivyo na wakati ana uhusiano wa aina hii na Mungu, ni uhusiano gani uliopo kati ya mtu huyu na Mungu? Ni wa uhasama na yeye amekuwa mpinzani wa Mungu, sivyo? Ikiwa unamwamini Mungu lakini huwezi kuupata ukweli au kuukubali ukweli, Mungu si Mungu wako. Mungu hakuoni kama adui lakini wewe unamwona Mungu kama mpinzani wako na huwezi kukubali kwamba Yeye ni ukweli wako na njia yako, basi tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa jinsi gani? Unapokabiliwa na maswala unapaswa kwanza kufikiria, "Hali ni ipi hapa? Siielewi vizuri sana, na haiko dhahiri kwangu. "Bila kujali suala ni nini, hufafanui suala hilo kwanza, badala yake kwanza ni lazima uone kile maneno ya Mungu yanachosema juu yake. Unaweza kushindwa kupata maneno husika ya Mungu, na huenda pia usijue ni ukweli gani suala hili linahusisha, lakini unang'amua kanuni—ni kutii, kwanza kabisa. Kwanza kabisa, endelea kutii, tuliza moyo wako na usubiri, usiwe na mawazo au fikira za binafsi, subiri kwa muda na uone jinsi Mungu anavyopanga kukabiliana nalo na kile ambacho Mungu atafanya. Hili ni katika hali ambapo huelewi kabisa. Na je, wakati ambapo huelewi? Kwa mfano, mtu anatoa maoni; unashughulikiaje suala hili? Je, unalishughulikiaje kwa njia inayopatana na ukweli? Kwanza unalikubali; unasikiliza na kusema, "Haya yote ni nini? Aa, kuna shida kwangu kulifanya kwa njia hii? Ikiwa kuna shida, basi hebu tuangalie." Usiichukulie hoja hiyo kwa wepesi; inahusisha mambo katika upeo wa wajibu wako, kwa hiyo unapaswa kulitazama kwa uangalifu. Huu ndio mtazamo sahihi wa kuchukua na hali sahihi ya kuwemo. Unapokuwa katika hali sahihi, wewe hufichua tabia ambayo imechoshwa na ukweli? (Hapana.) Hufichui tabia ambayo ina uhasama mintarafu ya ukweli, na unapotenda kwa njia hii tabia yako ya upotovu inabadilishwa; unatenda ukweli. Unapotenda ukweli kwa njia hii, ni matokeo gani yanayofanikishwa? (Roho Mtakatifu hutuongoza.) Mwongozo wa Roho Mtakatifu ni kipengele kimoja. Kwa Mungu, unatenda ukweli. Wakati mwingine una mwongozo wa Roho Mtakatifu na tatizo linarekebishwa; wakati mwingine baada ya kusikia juu ya suala hili, unalielewa kwa urahisi, na unaliona likiwa rahisi sana. Hicho ni kitu ambacho akili ya mwanadamu inaweza kufanikisha na unahitaji tu kukirekebisha. Hii ni hoja ndogo. Na hoja kubwa ni ipi? Unapotenda kwa njia hii, Mungu hukuona kama mtu anayetenda ukweli na kama mtu anayependa ukweli, na Yeye huona kwamba wewe si mtu anayeuchukia ukweli au ana uhasama mintarafu ya ukweli. Wakati huo huo Mungu anapoona moyo wako, Yeye pia huona tabia yako. Hii ni hoja kubwa. Yaani, unalolifanya mbele za Mungu, unaloishi kwa kudhihirisha mbele ya Mungu na unachokifichua mbele ya Mungu, na vilevile mtazamo unaouchukua, mawazo uliyo nayo na hali uliyomo katika kila kitu unachokifanya—maonyesho haya yote unayo mbele ya Mungu—haya ndiyo mambo muhimu zaidi.
Watu daima wanalalamika juu ya watu na masuala, na hili ni tatizo kubwa. Je, wao daima hufikiri nini? Wanafikiri kuwa ni watu wengine ambao ni wakatili kwao, au kwamba wengine huyafanya mambo kuwa magumu kwa makusudi, au huyapata makosa tu na watu wengine. Je, mtazamo huu ni sahihi? (Hapana, si sahihi.) Kwa nini unasema hapana? Ni kosa kabisa kulalamika daima juu ya masuala na watu. Hawafanyi jitihada na ukweli, na wao wanajaribu daima kuepuka aibu na kutafuta uthibitisho mbele ya wengine au miongoni mwa watu wengine, na wao daima hutaka kutumia njia za kibinadamu kuzitatua hoja hizi zote. Hiki ndicho kikwazo kikubwa mno kwa kuingia kwa maisha. Kwa kufanya kwa njia hii, kutenda kwa njia hii na kumwamini Mungu kwa njia hii, hutaweza kamwe kupata ukweli, kwa kuwa kamwe huji mbele ya Mungu. Huji kamwe mbele ya Mungu kukubali vitu vyote ambavyo Mungu hupanga kwa ajili yako, hutumii kamwe ukweli ili kutatua mambo haya yote, na daima wewe hutaka kutumia mbinu za kibinadamu kuyatatua. Hivyo machoni pa Mungu, umeenda mbali sana na Yeye na sio tu kwamba moyo wako umekwenda mbali sana na Mungu, lakini mawazo yako yote, nia zako zote na hali yako yote havijawahi kuwa mbele ya Mungu. Hivi ndivyo Mungu huwaona wale ambao hulalamika juu ya masuala na watu. Kwa hiyo, watu wengine ambao wana kipaji cha kuzungumza na ni wepesi kung'amua, hufikiria, "Nina ufasaha, na wakati ninapokuwa na watu wengine, wote hunihusudu na kunipenda. Wao hunitukuza, na watu wengi sana huridhishwa nami. "Je, hili ni la manufaa yoyote? Sifa yako njema miongoni mwa watu wengine imeanzishwa, lakini mbele ya Mungu, Amekupuuza daima, na anasema kuwa wewe ni mtu asiyemwamini Mungu na kwamba una uhasama mintarafu ya ukweli. Miongoni mwa wengine wewe hutenda kwa njia ambayo ni laini na ya hila, unaweza kumshughulikia mtu yeyote, una uwezo mkubwa wa kushughulikia hoja, na unaweza kukubaliana na mtu yeyote. Lakini mwishowe, kwa tathmini moja kutoka kwa Mungu utakwisha, utafika mwisho mbaya, na jaala yako itapangwa. Mungu atasema: "Huyu ni mtu asiyeamini, akipeperusha bendera ya imani katika Mungu ili kupata baraka. Huyu mtu ana uhasama mintarafu ya ukweli, hajawahi kamwe kufanya jitihada na ukweli, na hajawahi kuukubali ukweli." Mnafikiria nini juu ya aina hii ya tathmini? Je, hii ndiyo tathmini mnayoitaka? (Hapana.) Bila shaka sicho kile mnachokitaka. Labda watu wengine hawajali, na wao husema, "Sijali. Hatuwezi kumwona Mungu kwa njia yoyote. Suala la kweli zaidi ambalo tunalo ni kuwa tunapaswa kukubaliana na watu walio nasi. Ikiwa hatuwezi kufanya mahusiano haya yafaulu basi tunawezaje kuishi miongoni mwa watu hawa? Maisha yetu yangekuwa magumu sana. Angalau sana tunapaswa kukubaliana na watu hawa na kushughulikia mahusiano vizuri. Chochote kingine kinaweza kusubiri." Ni watu wa aina gani hawa? Je, hawa bado ni watu ambao wanamwamini Mungu? (Hapana.) Mtu ni lazima aishi mbele ya Mungu nyakati zote na ni lazima aje mbele ya Mungu na kutafuta ukweli nyakati zote na kwa hoja zote, ili mwishowe Mungu atasema: "Wewe ni mtu anayeupenda ukweli na Mungu anafurahishwa nawe, Mungu anakukubali. Mungu huuona moyo wako na huiona tabia yako. "Unafikiria nini kuhusu tathmini hii? Hii ina maana kwamba wewe ni salama, sivyo?
Je, nyinyi kwa kawaida huzingatia hoja hizi? Hebu niwaambie, mnapomwamini Mungu, bila kujali kama unafanya wajibu wa nje, au unafanya wajibu unaohusiana na kazi yoyote au kipengele chochote cha kazi ya weledi ndani ya familia ya Mungu—bila kujali ni wajibu gani unaoufanya—ikiwa huwezi daima kuja mbele ya Mungu, ikiwa huwezi kuishi mbele ya Mungu, basi wewe si muumini na hakuna tofauti kati yako na mtu asiyeamini. Je, hili linasikika sahihi kwako? Je, mnaweza kufahamu jambo hili? Labda kuna baadhi ya watu sasa ambao hawawezi kufanya wajibu wao kwa sababu ya mazingira yasiyofaa, na wanaishi miongoni mwa wasioamini, lakini daima wanaweza kupata nuru na mwongozo wa Mungu—hivyo hali ni ipi hapa? Mnajua? (Ni kwa sababu daima wao huja mbele ya Mungu.) Ndiyo, hili huamua jinsi hali ya kiroho ya mtu ilivyo. Ikiwa, ndani yako mwenyewe, daima huwezi kumhisi Mungu, ikiwa daima u mdhaifu, daima u hasi, au wewe daima ni mwasherati, au daima hubebi mzigo katika wajibu wako na moyo wako siku zote unaboronga bila lengo lolote, basi hii ni hali nzuri au hali mbaya kuwemo? Je, ni hali ambapo unaishi mbele ya Mungu? Au ni hali ambapo huishi kamwe mbele ya Mungu? (Ni hali ambapo hatuishi mbele ya Mungu.) Basi fikirieni hili kwa makini—katika hali nyingi, huwa mnaishi mbele ya Mungu au hamuishi mbele ya Mungu? Je, mnafahamu vyema juu ya hili ndani ya mioyo yenu? Je, nyinyi huishi mbele ya Mungu wakati mwingi, au ni kwa nyakati chache tu? (Ni kwa nyakati chache tu.) Hili ni sumbufu kwenu. Kama mtu ni mchezaji, mwimbaji, mwandishi au mtengenezaji filamu, ikiwa moyo wake haujishughulishi kamwe na kufanya wajibu wowote unaofaa, ikiwa yeye ni mpotovu na hastahimiliki, ikiwa huwa daima anavurugika anapokabiliwa na masuala, hana wazo lolote ni hoja ipi inayohusisha kipengele kipi cha ukweli, wala hana wazo lolote kama kile anachokifanya kina athari yoyote, ikiwa hajui mambo gani anayoyafanya kila siku yanayomchukiza Mungu, ni mambo gani ambayo Mungu anaweza kuyakubali au ni mambo gani Mungu huyachukia, na wao huendelea tu siku baada ya siku katika kiwewe, basi ni hali aina gani hii ya kuwemo? Je, wale wanaoishi katika hali hii wana moyo wa kumuogopa Mungu ndani yao? Je, wana uwezo wa kutenda na kanuni? Je, wana uwezo wa kufanya chochote cha maana? (Hapana.) Wanapofanya wajibu wao, wanaweza kusema, "Ni lazima nivumilie vikwazo fulani, ni lazima nifanye kazi kwa bidii, kwa moyo wangu wote na kwa nguvu zangu zote, na kuwa mwaminifu"? Je, ana uwezo wa kuwa na uaminifu wowote? (Hapana.) Basi mnafanya nini hapa kwa kweli mnapofanya wajibu wenu? (Mkitumia nguvu.) Mko sawa; Mnatumia nguvu. Nyinyi ni wenye uwezo wa kazi, sivyo? Chakula chenu na nyumba zenu zote zimeshughulikwa, na halafu nyinyi hufanya kazi hapa. Ingawa hamchumi fedha hapa, mnahisi ni sawa mnapopata chakula, kinywaji na mahali pa kuishi. Lakini nyinyi huchuma ukweli? (Hapana.) Basi nyinyi hupoteza sana. Nyinyi ni wapumbavu mno! Mmemwamini Mungu kwa miaka mingi sasa, hazijakuwa siku chache tu. Mmesikia ukweli mwingi sana na hamjui mnamwamini Mungu kwa minajili gani, mnachohitaji kufanya, mnachopaswa kupata, au ni kitu gani cha muhimu zaidi kupata. Mnajua kidogo sasa? (Ndiyo.) Mnajua nini? Niambieni. (Kwa kumwamini Mungu, kupata ukweli ndilo jambo muhimu zaidi.) Kupata ukweli ndilo jambo muhimu zaidi? Kweli au uongo? (Kweli.) Bila shaka ni kweli. Lakini labda huenda msiwe na maarifa halisi ndani ya mioyo yenu hivi sasa, na huenda hamjalitambua kwa kiwango hiki.
Je, mmekisoma Kitabu cha Ayubu? (Ndiyo.) Na mlipokisoma Kitabu cha Ayubu, mioyo yenu ilisisimka? (Ndiyo.) Hivyo mlipata fikira za shauku, na kutaka kuwa mtu kama Ayubu? (Ndiyo.) Ni kwa muda gani mliweza kuendeleza hali hiyo na hisia hiyo? Nusu siku, siku mbili, juma moja? Au kwa mwezi mmoja au miwili, au mwaka mmoja au miwili? (Labda siku mbili hadi tatu.) Hisia hiyo iliondoka baada ya siku tatu? Wakati hisia hiyo inapoondoka, wewe huendelea kusoma, na unapoendelea kusoma unaweza kuiendeleza kwa siku zingine tatu. Lakini hivyo sivyo ilivyo, au ndivyo? Unaposoma kitabu hicho na unahisi msisimko, unapaswa kuomba, kindani fanya uamuzi wako kuwa unataka kuwa kama Ayubu, mtu ambaye anaweza kumjua Mungu, ambaye anaweza kupata ukweli, na anayeweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, na unasali kwa Mungu afanye vivyo hivyo kwako, na kwamba Mungu akuongoze na kukupangia mazingira, kukutolea nguvu, kukukinga katika mazingira yoyote ambayo unaweza kukabiliana nayo ili uweze kusimama imara, ili usimuasi Mungu, na unaweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, na unaweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Unahitaji daima kumsihi Mungu kwa lengo hili na kwa kile unachokitamani sana na unachotaka kukipata moyoni mwako, unahitaji kusihi na kuomba kwa ajili yalo, na wakati Mungu anapouona moyo wako wa kweli Yeye atalifanya. Huhitaji kuogopa Mungu akifanya jambo hili, kwa maana Mungu hawezi kuufanya mwili wako kufunikwa na vidonda kama wakati Alipomjaribu Ayubu na kukunyang'anya kila kitu ulicho nacho; Mungu hatakufanyia hivyo. Hatua kwa hatua Atafanya kazi Yake kwako kwa mujibu wa kimo chako. Ni lazima usihi kwa uaminifu; usilisome tu leo, ujihisi kusisimka na kumsihi Mungu, na kisha baada ya siku mbili usifanye chochote, na yawe yameisha mara unapogeuka. Watu husema, "Ayubu ni nani?" "Nani? Ayubu? Ayubu ni nani? Je, nawezaje kutojua? Huenda nimesikia kumhusu." Hili ni sumbufu! Usilisome kwa siku tatu na lote limesahaulika, limetoka moyoni mwako. Ukiwahusudu watu kama Ayubu na ungependa kuwa mtu kama huyo, moyoni mwako unapaswa kuwa na njia ya jinsi ya kuwa mtu kama huyo, lazima uweke moyo wako mbele ya Mungu, kisha ni lazima uombe kuihusu, omba kuihusu mara nyingi, chukua hoja hii kutoka moyoni mwako na kuitafakari mara nyingi, soma vitabu, soma makala kuhusu Ayubu na maneno ya Mungu yanayohusiana na Ayubu, itafakari daima na tena na tena, fanya ushirika pamoja na watu ambao wana aina hii ya maarifa, uzoefu au azimio , na lazima ufanye kazi kwa bidii mintarafu ya lengo hilo. Unapaswa vipi kufanya kazi kwa bidii? Kusoma tu kwa kweli sio kufanya kazi kwa bidii. Unahitaji kufanya jitihada na hoja hii, utoe maombi yako na kuiweka katika matendo, huku wakati huo huo ukiwa na azimio la kuvumilia mateso na kuwa na moyo wa shauku na hamu. Kisha unarairai, utoe maombi yako na kumwomba Mungu afanye hivi. Ikiwa Mungu haifanyi, itakuwa bure bila kujali ni jitihada kiasi gani unayoiweka, na jitihada zako ni za bure. Mungu huifanyaje? Yeye huanza kwa kuweka na kupanga mambo kwa ajili yako kulingana na kimo chako. Kwa mfano, unakaribia kuchukua mtihani wa kuingia chuo cha elimu, na unasema, "Ninataka alama ili kuingia katika Chuo Kikuu cha Tsinghua." Unaanza kuweka jitihada ili kufanikisha hili, unapitia upya masomo yako, unatafuta vifaa vya kujifunza juu ya chochote na kila kitu na unatafuta walimu kukufundisha. Kisha unawaambia wazazi wako na wanasema, "Mtoto wetu ana azimio zuri. Yeye huanza jambo kwa dhati, ana azimio na hajakosa ustadi." Kwa hiyo, wazazi wako watafanya nini? Wote wawili wataandaa ada yako ya masomo na kukupatia mwalimu. Watafanya mipango sahihi ya maisha yako, wakati unapopaswa kupumzika, na masomo yako, wakupeleke shuleni na kukuchukua baadaye, na watalifanya ili kwamba, wakati huu, usipate uchovu, au njaa, au kukosa chakula cha kutosha. Watakusaidia kwa kushughulikia na kusimamia mambo katika ulimwengu wa nje ili usichanganyikiwe. Watakufanyia mipango sahihi katika vipengele vyote. Kwa njia hii, utakuwa na wakati wa kutosha wa kupitia upya, kusoma na kufanikisha ndoto yako. Kuhusu kumwamini Mungu, chochote unacholenga au uamuzi wowote ulio nao, unapaswa kuzungumza na Mungu. Unahitaji kuomba juu ya hoja hii na kusihi sana juu yalo; itachukua muda mrefu! Itakuwa bure kuwa na moyo usio mwaminifu. Ikiwa unasali mara kadhaa tu mara kwa mara na kisha unapoona kwamba Mungu hajakufanyia chochote, unasema, "Lisahau. Sijali. Liwe liwalo, nitaacha tu mambo yatokee kama kawaida yake, na nitachukua mambo kama yanavyokuja," basi hili litakuwa bure, na moyo wako si mwaminifu. Je, Mungu atakufanyia chochote ikiwa una dakika kadhaa tu za shauku? Je, Mungu atapanga mazingira kwa ajili yako? Je, hilo linakubalika? Kwa kweli Mungu hafanyi kazi kwa njia hiyo. Mungu anataka kuona uaminifu wako na Anataka kuona ni kwa muda gani uaminifu wako na bidii ya moyo wako vinaweza kudumishwa, na kama moyo wako ni kweli au uongo. Mungu atangoja; Yeye husikiliza sala zako na kile unachorairai, na Yeye husikia maazimio yako na shauku zako, lakini Yeye bado hajaona maazimio yako ya kuvumilia mateso, kwa hivyo Yeye hatakufanyia chochote. Ikiwa wewe husema maneno machache na kisha kwenda, Mungu atakufanyia chochote? Hakika hapana. Lazima uendelee kurairai, endelea kuomba, jitahidi na kulitafakari, kisha uonje mazingira ambayo Mungu hukupangia—yatakujia kidogo kidogo, na Mungu ataanza kutenda. Bila moyo wa kweli, ni bure. Wewe husema, "kwa kweli mimi humhusudu Ayubu na kwa kweli mimi humhusudu Petro." Ni haja gani kuwahusudu? Huwezi kuwa wao bila kujali ni kiasi gani wewe huwahusudu, na bila kujali ni kiasi gani wewe huwahusudu, Mungu hatakufanyia kazi sawa na ile Aliwafanyia. Kwa nini hivyo? Kwa sababu wewe si aina moja ya mtu kama walivyokuwa. Humiliki azimio lao, au ubinadamu wao, na humiliki moyo wao wa shauku uliotafuta ukweli. Wakati utakapokuja utakapomiliki vitu hivi, ni hapo tu ndipo Mungu atakapokufanyia zaidi. Unaelewa?
Je, wengi wenu sasa wana azimio la kuelewa ukweli, kupata ukweli na kukamilishwa mwishowe? (Ndiyo.) Azimio lako ni kubwa kiasi gani? Je, unaweza kufanya liendelee kwa muda gani? Unajua? (Nina azimio hili wakati niko katika hali nzuri. Wakati mambo yanapotokea ambayo hayakubaliani na mwili wangu au kupatana na dhana zangu, na ninapopatwa na usafishaji au matatizo ndani yangu, basi imani yangu hupotea, mimi hukwama kwa namna ya hali hasi, na azimio nililokuwa nalo mwanzo hupungua hatua kwa hatua.) Hili halitaweza. Huku ni kuwa dhaifu sana. Lazima ufikie hatua ambapo azimio lako halibadiliki bila kujali ni mazingira gani unayoyakabili; huku tu ndiko kuwa mwaminifu, na huo ndio upendo halisi wa ukweli na shauku halisi ya kuwa aina hii ya mtu. Itakuwa bure kujikunyata wakati hoja fulani ndogo au shida inapotokea, au kuwa hasi, kusononeka na kuacha azimio lako mwenyewe wakati unapokabiliwa na shida ndogo. Unahitaji kuwa na nguvu ya mtu anayechagua kuhatarisha maisha yake, na kusema, "Bila kujali kinachotokea, hata kama ni lazima nife sitaacha azimio langu au kuachana na lengo hili." Halafu hakutakuwa na shida ambayo inaweza kukuzuia, na Mungu atakufanyia jambo hili. Aidha, lazima uwe na mtazamo wa aina hii na ufahamu jambo linapotokea, na kusema, "Bila kujali kinachofanyika, yote ni sehemu ya kufanikisha lengo langu, na ni shughuli ya Mungu. Kuna udhaifu ndani yangu, lakini mimi si hasi. Ninamshukuru Mungu kwa upendo Anaonipa na kwa kunipangia aina hii ya mazingira. Ni lazima nisisalimu amri. Kusalimu amri kwangu kungekuwa sawa na kufanya masikilizano na Shetani, na ni sawa na kujiangamiza. Kusalimu amri juu ya shauku na azimio langu kutakuwa sawa na kumsaliti Mungu. "Hii ni aina ya moyo ambao ni lazima uwe nao. Suala lolote dogo unalokabiliana nalo ni pumziko dogo katika mfanyiko tendani wa kufanya maendeleo katika maisha, na ni sharti usiruhusu lizuie kwendelea kwako au kuzuia mwelekeo wako wa mbele. Ni vyema kwako kuchukua pumziko dogo au upumzike kwa muda, lakini mwelekeo wako haupaswi kubadilika, na ni lazima usikome kabisa kwa hali yoyote; hii ndiyo aina ya azimio na uamuzi unayopaswa kuwa nayo. Bila kujali wengine wanavyosema au jinsi walivyo, na bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, azimio lako halipaswi kubadilika. Mungu asema, "Sikutaki tena," nawe unasema, "Mungu hanitaki tena, kwa hivyo nitasahau tu kulihusu." Je, si huku ni kuwa mtu bure? Au Mungu asema, "Wewe umepotoka sana, na Ninakuchukia," nawe unasema, "Mungu ananichukia, nitaishi kwa sababu gani tena? Nitatafuta kamba ili kujinyonga." Je, si huku ni kuwa mtu bure? Hutafanikisha lengo lako jinsi hii. Kwa mintarafu ya hadhi yenu ya sasa, hakuna hata mmoja wenu ambaye ameweza kujaribiwa na Mungu bado, na kusema, "Mungu, tafadhali nijaribu." Huna hadhi hii. Je, mna uwezo wa kufanya nini tu? Ni lazima muombe: "Ee Mungu, tafadhali niongoze, nipe nuru, nipe bidii ya kuendelea na unipe bidii ili niweze kuitembea njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu kwa mujibu wa shauku zangu. Bila kujali namna gani ya mateso ninayoyapitia, Wewe hunipa nguvu na Wewe hunilinda. Ingawa ninaweza kuwa dhaifu na ingawa kimo changu ni kichanga, ninakuomba Unipe nguvu, kunilinda na kunionyesha wema. Sitasalimu amri." Hivi ndivyo mnavyopaswa kuomba, na ni lazima daima mje mbele ya Mungu kuomba. Wakati wengine wanacheka na kufanya mzaha na kujiendekeza, ombea hili; wakati wengine wanapojifurahisha, ombea hili; wakati wengine ni hasi, ombea hili; wakati wengine wanalala fofofo, au kuchelewa kuamka, wewe tayari unaliombea hili; wakati wengine wanatembea njia ya ulimwengu na kwa ulafi kufurahia anasa za kimwili, au kufuata mienendo ya kidunia, ombea hili. Wakati unapoweza kuishi mbele ya Mungu katika mambo yote na unaweza kujiweka katika mipaka fulani, wakati unapoweza kujiweka ukiishi mbele ya Mungu na kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi Mungu anaweza kuliona hili. Wakati Mungu anapouona moyo wa mtu, Yeye hayatumii tu macho Yake; Yeye hupanga mazingira kwa ajili yako na Yeye hugusa moyo wako kwa mikono Yake. Kwa nini Nasema hili? Wakati Mungu anapokupangia mazingira, Yeye hutazama kuona kama moyo wako unachafuliwa nayo, unayachukia, unayapenda au ni mtiifu, au kama husubiri kwa utulivu, au hutafuta ukweli—Yeye huona jinsi moyo wako unavyobadilika na ni katika mwelekeo gani huenda. Mabadiliko katika moyo wako, kila badiliko la fikira na mawazo ndani ya moyo wako kuhusu watu, hoja, na mambo ambayo Mungu hupanga kwa ajili yenu, na kila badiliko ya hali ya moyo uliyo nayo—Mungu anaweza kuyahisi yote. Ingawa huenda hujamwambia yeyote na huenda hujaomba, badala yake kufikiria tu mawazo haya kwa moyo wako mwenyewe au katika ulimwengu wako mwenyewe, lakini kwa Mungu ni wazi kabisa na Yeye huliona wazi kwa tazamo moja. Watu hutumia macho yao kukuona, na Mungu hutumia moyo Wake kuugusa moyo wako—Yeye yu karibu hivi nawe. Na kama unaweza kuuhisi uchunguzi wa Mungu, basi unaishi mbele ya Mungu. Kama huwezi kuuhisi kabisa na unaishi ndani ya ulimwengu wako, basi uko katika shida. Wewe huishi mbele ya Mungu, wewe uko mbali na Mungu na mbali sana kutoka Kwake, huendi karibu Yake kwa moyo wako au moyo wako uukaribie moyo Wake, na hukubali uchunguzi wa Mungu. Na Mungu anajua hili! Mungu anaweza kabisa kuhisi yote haya. Kwa hivyo, wakati una azimio na lengo la kukamilishwa na Mungu, kuwa mtu anayetekeleza mapenzi ya Mungu, mtu anayemcha Mungu na aepukanaye na maovu, unapoweza kuomba mara nyingi juu ya hoja hii na kusihi kwa ajili yalo, unapoweza kuishi mbele ya Mungu, kutokwenda mbali na Mungu au kumwacha Mungu, basi wewe unalielewa hili, na Mungu anajua kuhusu hilo pia. Watu wengine wanasema: "Mimi ni dhahiri kulihusu, lakini sijui kama Mungu anajua kulihusu." Hili si jambo la busara. Kwa hiyo hali ni gani hapa? Kama wewe mwenyewe u dhahiri kulihusu, na hujui kama Mungu anajua kulihusu, basi huna uhusiano na Mungu. Umeelewa? Kwa nini Nasema wewe huna uhusiano na Mungu? Wewe huishi mbele ya Mungu, kwa hivyo unashindwa kuhisi kama Mungu yu pamoja nawe, kama Mungu anakuongoza au kukulinda, na kama Mungu anakushutumu wakati unapofanya jambo baya. Huwezi kuhisi jambo lolote kati ya haya, kwa hiyo hili linamaanisha kwamba huishi mbele ya Mungu. Wewe hufikiria tu mwenyewe na kuleweshwa na mawazo yako mwenyewe; huko ni kuishi katika ulimwengu wako mwenyewe na sio kuishi mbele ya Mungu, na hakuna uhusiano kati yako na Mungu.
Mtu anawezaje kuudumisha uhusiano wake na Mungu? Ni kwa njia gani anaweza kuudumisha? Kwa njia ya kusihi, kuomba na kuwa na ushirikiano na Mungu katika moyo wake. Aina hii ya uhusiano itakuwezesha kuishi daima mbele ya Mungu, na kwa hiyo utakuwa mtu mwenye amani sana. Watu wengine daima hufanya mambo ya nje na hujihusisha na mashauri ya nje. Baada ya siku moja au mbili bila kushiriki katika maisha ya kiroho, moyo wao hauna utambuzi, na baada ya siku tatu, au siku tano, bado hauna utambuzi, au bado hauna utambuzi baada ya mwezi mmoja au miwili. Hili lina maana kwamba hawaombi au kurairai chochote, na hawajishughulishi na ushirikiano wa kiroho. Kusihi ni wakati unapokabiliwa na masuala, unamwomba Mungu akusaidie, akuongoze, akukimu, akupe nuru, akuruhusu ujue mapenzi ya Mungu na kujua ukweli ni nini. Kuomba kuna mawanda mapana kiasi. Wakati mwingine ni kusema maneno ndani ya moyo wako, kuzungumza na Mungu wakati unapokabiliwa na shida na kusema maneno yaliyo moyoni mwako kwa Mungu wakati unapokuwa hasi na dhaifu. Unaweza pia kumwomba Mungu unapokuwa mwasi, au unasema na Mungu juu ya masuala yanayokukabili kila siku, yote kuhusu yale ambayo unaweza kuyabaini na yale ambayo huwezi kuyabaini. Huku ni kuomba. Mawanda ya kuomba kimsingi ni kuwa na mazungumzo na Mungu, wakati mwingine kwa nyakati zilizopangwa na wakati mwingine kwa nyakati zisizoratibiwa, na yanaweza kufanyika wakati wowote na mahali popote. Ushirikiano wa kiroho kwa kweli haushikilii muundo fulani. Labda kuna suala, labda hakuna; wakati mwingine kutakuwa na kitu cha kusema, na wakati mwingine hakutakuwa. Huu ni ushirikiano wa kiroho. Wakati kuna suala maalum la kuzungumzia na Mungu, basi unaweza kuomba. Wakati hakuna suala lolote, unafikiri tu juu ya Mungu, "Mungu humpendaje mwanadamu? Mungu anamtunzaje mwanadamu? Mungu humshutumuje mwanadamu?" "Ee Mungu, ninahisi nimefanya jambo hili vibaya. Kama kwa kweli nimefanya jambo hili vibaya, basi nishutumu na unifanye nifahamu." Huu ni ushirika wa kiroho, na unaweza kufanyika wakati wowote na mahali popote. Wakati mwingine uko barabarani na unafikiria kuhusu kitu ambacho huufanya moyo wako uhisi huzuni kweli. Huna haja ya kupiga magoti au kuyafunga macho yako, lakini badala yake unasema mara moja kwa Mungu moyoni mwako: "Ee Mungu, naomba Uniongoze na suala hili. Mimi ni dhaifu na siwezi kulishinda. "Moyo wako umesisimuliwa, na kwa maneno haya machache rahisi Mungu anajua yote kulihusu. Wakati mwingine unafikiria kuhusu familia yako, na unaweza kusema: "Ee Mungu, kwa kweli nimeikosa familia yangu …." Humkosi mtu yeyote hasa, unahisi tu vibaya, hivyo unaongea na Mungu. Usizungumze na watu wengine kulihusu, kwa kuwa hilo halina maana. Unapozungumza na mtu mwingine kulihusu, huenda ikawa kwamba anaikosa familia yake hata zaidi ya wewe, basi hili linakuathiri na unaishia kuikosa yako hata zaidi, na hili halikuletei faida yoyote kamwe. Unapozungumza na Mungu kulihusu, basi Mungu atakufariji, Akufurahishe tena na kukupisha katika wakati huu mgumu na kupita hali hii ndogo. Hali hii, jiwe hili dogo njiani mwako halitakukwaa, halitakuzuia au kuathiri utekelezaji wa wajibu wako. Wakati mwingine, unapozungumza au kufanya ushirika na wengine, moyo wako unaweza ghafla kuwa na hisia ya kuvunjika kidogo au kujisikia mwenye wasiwasi sana, hivyo unafanya haraka kumwomba Mungu, na unaweza kufanya hivi wakati wowote na katika mahali popote. Kunaweza kuwa hakuna chochote unachokisihi, au chochote unachotaka Mungu akufanyie au akunurishie, unaongea tu na Mungu na kuzungumza Naye wakati wowote na katika mahali popote. Ni hisia gani unayopaswa uwe nayo wakati wote? Ni hii: Mungu huwa hatoki kandoni mwangu kamwe, Yeye yu pamoja nami kandoni mwangu wakati wote, Yeye hajawahi kuniacha, na ninaweza kuhisi hili. Bila kujali ni mahali gani nipo, bila kujali ninafanya nini, kama ninapumzika au kulala, kula chakula, au kwa mkutano, au kama sisemi chochote mchana kutwa ninapotekeleza wajibu wangu, najua moyoni mwangu kwamba Mungu ananiongoza kwa mkono, na kwamba Yeye hajawahi kuniacha. Wakati mwingine, wewe hufikiria jinsi umefaulu kwa miaka hii michache iliyopita, mwezi baada ya mwezi, na unahisi moyoni mwako kwamba kimo chako kimekomaa na kwamba ni Mungu anayekuongoza, na kwamba ni upendo wa Mungu ambao unakulinda daima. Unapofikiri hivi, unaomba moyoni mwako: "Nakushukuru Wewe, Mungu!" Na wewe unatoa shukrani zako, na kusema: "Mimi ni dhaifu sana, mwenye woga sana, na mpotovu kwa kina sana. Kama Hukuniongoza kwa njia hii, mimi mwenyewe singeweza kufanikiwa hadi leo. Asante Mungu!" Je, si huu ni ushirika wa kiroho? Kama ungekuwa jinsi hii, basi si ungekuwa na mengi ya kumwambia Mungu? Hungeishi siku baada ya siku bila kuwa na kitu cha kumwambia Mungu. Ikiwa huna chochote cha kumwambia Mungu, basi inamaanisha kwamba Mungu hayuko ndani ya moyo wako. Kama una Mungu ndani ya moyo wako, basi unaweza kumwambia Mungu mambo unayoweza kusema kwa wandani wako—Mungu ni msiri wako wa karibu zaidi. Unapomruhusu Mungu kuwa msiri wako wa karibu zaidi, rafiki yako wa karibu zaidi, familia unayoweza kuitegemea zaidi, kuiegemea zaidi, na Aliye mwaminifu zaidi, Aliye mwandani sana na wa karibu, basi itakuwa vigumu kutokuwa na mambo ya kusema Kwake. Wakati daima una mambo ya kumwambia Mungu, si basi utaweza kuishi daima mbele ya Mungu? Unapoweza kuishi mbele ya Mungu daima, basi wakati wote utaweza kutambua jinsi Mungu anavyokuongoza, jinsi Mungu anavyokulinda, jinsi Anavyokutunza, jinsi Anavyokuwa amani yako na furaha, Anavyokupa baraka na nuru, jinsi Mungu anavyokushutumu, kukufundisha nidhamu, kukuadhibu, kukuhukumu na kukuadibu. Wakati unapoishi mbele ya Mungu daima, moyo wako utajua kwa dhahiri sana kile Mungu anachofanya ndani yako. Hutakuwa na siku ambapo utakuwa mpumbavu kabisa na kutojua chochote, ukisema tu maneno "Ninamwamini Mungu, mimi hutekeleza wajibu wangu, mimi huhudhuria mikutano, mimi husoma kila siku na huomba kila siku." Huwezi tu kupitia mifanyiko tendani hii yote au kuwa tu na aina hii ya tabia ya nje.
Mnapaswa kujua sasa, kwa hiyo ni nini kitu muhimu zaidi katika kumwamini Mungu? Unapomwamini Mungu, kama Mungu hayuko ndani ya moyo wako na Yeye hakuhusu, na kama humwoni Mungu kama mwandani wako sana, wako wa karibu sana, familia na msiri mwaminifu sana na wa kutegemewa sana, basi Mungu si Mungu wako. Sawa, kwa hiyo sasa nendeni na mtende kwa muda kwa mujibu wa yale ambayo Nimeyasema, na muone kama hali yenu ya ndani itabadilika au la. Tenda kwa mujibu wa yale ambayo Nimeyasema na hakika utaishi mbele ya Mungu, utaishi katika tabia ya kawaida na kuwa katika hali ya kawaida. Wakati hali ya mtu ni ya kawaida, ni hapo tu ambapo mambo anayoyaonyesha na kuyafichua kwa kila hatua, au miongoni mwa watu tofauti, masuala, na mambo, au katika mazingira tofauti, yatakuwa ya kawaida. Ni kwa njia hii tu ambapo maisha yake yanaweza kukomaa na anaweza kuingia katika uhalisi wa ukweli kidogo kidogo. Unaelewa? (Ndiyo.)
Tanbihi:
a. Nakala ya awali imetoa "cha wajibu wenu."

kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni