Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Sita
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
4. Njoo Chini ya Utawala wa Muumba na Ukabiliane na Kifo kwa Utulivu
5. Bidii na Faida za Ayubu katika Maisha Zamruhusu Kukabiliana na Kifo kwa Utulivu
6. Ni kwa Kukubali tu Ukuu wa Muumba Ndipo Mtu Anaweza Kurejea Upande Wake
Soma Zaidi:
Mwenyezi Mungu anasema, "
Wakati mtu hana maarifa yaliyo wazi na hajapitia ukuu wa Mungu na mipangilio Yake, maarifa ya mtu kuhusu hatima na yale ya kifo yatakuwa yale yasiyoeleweka. Watu hawawezi kuona waziwazi kwamba haya yote yamo kwenye kiganja cha mkono wa Mungu, hawatambui kwamba Mungu ameushika usukani na Anashikilia ukuu juu yao, hawatambui kwamba binadamu hawezi kutupa nje au kutoroka ukuu kama huo; na kwa hivyo wakati wanapokabiliwa na kifo hakuna mwisho wowote katika maneno yao ya mwisho, wasiwasi wao, na hata majuto. Wanalemewa sana na mambo mengi, wanajivuta ajabu, kunakuwa na mkanganyo mkubwa, na haya yote yanawafanya kuogopa kifo. Kwani mtu yeyote aliyezaliwa ulimwenguni humu, kuzaliwa kwake kunahitajika, na kuaga kwake hakuwezi kuepukika, na hakuna mtu anayeweza kuupiga chenga mkondo huu. Kama mtu atataka kuondoka ulimwenguni humu bila maumivu, kama mtu atataka kukabiliana na awamu ya mwisho ya maisha bila kusitasita au wasiwasi, njia pekee ni kutokuwa na majuto. Na njia pekee ya kuondoka bila majuto ni kujua ukuu wa Muumba, kujua mamlaka yake, na kunyenyekea mbele zake. Ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuwa mbali na mahangaiko ya binadamu, maovu, utumwa wa Shetani; ni kwa njia hii ndipo mtu anaweza kuishi maisha kama ya Ayubu, akiongozwa na akibarikiwa na Muumba, maisha yaliyo huru na yaliyokombolewa, maisha yenye thamani na maana, maisha yenye uaminifu na moyo wazi; ni kupitia kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kunyenyekea, kama Ayubu, kujaribiwa na kunyang’anywa na Muumba, kunyenyekeza katika mipango na mipangilio ya Muumba; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kumwabudu Muumba maisha yake yote na kuweza kupata pongezi Lake, kama Ayubu alivyopata, na kusikia sauti Yake, kumwona akionekana; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi na kufa kwa furaha, kama Ayubu, bila ya maumivu, bila wasiwasi, bila majuto; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi kwa nuru, kama Ayubu, kupita kila mojawapo ya awamu ya maisha kwa nuru, na kukamilisha vizuri safari yake kwa nuru, kutimiza kwa ufanisi kazi yake maalum—kupitia, kujifunza, na kujua ukuu wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa—na kuiaga dunia kwa nuru, na milele hadi milele kusimama upande wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa, kilichopongezwa na Yeye.
Usikose Fursa ya Kujua Ukuu wa Muumba
Awamu sita zilizofafanuliwa hapo juu ni awamu muhimu zilizowekwa wazi na Muumba ambazo kila mtu wa kawaida lazima apitie katika maisha yake. Kila mojawapo ya awamu hizi ni za kweli; hakuna mojawapo kati yazo ambayo inaweza kuepukwa, na zote zinasheheni uhusiano na kuamuliwa kabla kwa Muumba na ukuu Wake. Hivyo basi kwa binadamu, kila mojawapo ya awamu hizi ni sehemu muhimu ya kujikagua, na namna ya kupitia kila mojawapo vizuri ni suala muhimu sana ambalo nyinyi nyote mnakabiliwa nalo.
Mkusanyiko wa miongo ambayo inaunda maisha ya binadamu si mirefu sana wala mifupi sana. Miaka ishirini na-kitu iliyopo katikati ya kuzaliwa na kukomaa hupita kwa muda mfupi tu wa kupepesa jicho, na ingawaje wakati huu katika maisha mtu anachukuliwa kuwa mtu mzima, watu katika kundi hili la umri wanajua machache sana kuhusu maisha ya binadamu na hatima ya binadamu. Wanapozidi kupata uzoefu zaidi, ndipo wanapopiga hatua kwa utaratibu hadi kwenye umri wa miaka ya kati. Watu katika miaka yao ya thelathini na arubaini huanza kuupata uzoefu unaoanza kuota wa maisha na hatima yake, lakini fikira zao kuhusu mambo haya zingali na ukungu mwingi sana akilini mwao. Si mpaka umri wa arubaini ndipo baadhi ya watu huanza kumwelewa binadamu na ulimwengu, vilivyoumbwa na Mungu, na kung’amua kwamba maisha ya binadamu yanahusu tu, kile ambacho hatima ya binadamu inahusu. Baadhi ya watu, ingawaje wamekuwa wafuasi wa muda mrefu wa Mungu na sasa wanao umri wa kati, bado hawamiliki maarifa na ufafanuzi sahihi wa ukuu wa Mungu, sikwambii hata unyenyekevu wa kweli. Baadhi ya watu hawajali chochote isipokuwa namna ya kupokea baraka, na ingawaje wameishi kwa miaka mingi, hawajui au hawaelewi hata kidogo hoja ya ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu, na kwa hivyo bado hawajaingia hata kwenye kipindi cha matendo halisi cha kunyenyekea katika mipango na mipangilio ya Mungu. Watu kama hao ni wajinga kabisa; watu kama hao wanaishi maisha yao bure bilashi.
Kama maisha ya binadamu yangegawanywa kulingana na kiwango cha mtu cha kile alichopitia maishani na maarifa yake kuhusu hatima ya binadamu, basi yangegawanywa kwa sura tatu. Sura ya kwanza ni ujana, miaka ile ya kati ya kuzaliwa na umri wa kati, au kuanzia kuzaliwa hadi kugonga miaka thelathini. Sura ya pili ni ya ukomavu, kuanzia umri wa miaka ya kati hadi umri wa uzee, au kuanzia thelathini hadi sitini. Na sura ya tatu ni kile kipindi cha uzee wa mtu, kuanzia umri wa uzee, kuanzia miaka sitini hivi, mpaka pale mtu anapoondoka ulimwenguni. Kwa maneno mengine, kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka ya kati, maarifa ya watu wengi kuhusu hatima na maisha ni finyu na ni yale ya kuiga tu kama kasuku, fikira za wengine yanayokosa hali halisi iliyo ya kweli na ya matendo. Kwenye kipindi hiki, mtazamo wa mtu kuhusu maisha, na namna ambavyo mtu anapojipanga katika ulimwengu vyote ni vya juujuu na vinyonge sana. Hiki ndicho kipindi cha mtu cha utoto. Baada tu ya mtu kuonja furaha na huzuni zote za maisha ndipo anapofaidi na kupata ufahamu halisi wa hatima, ndipo mtu—kwa kufichika akilini, na ndani kabisa ya moyo wake—huanza kwa utaratibu kushukuru kutoweza kurudishwa nyuma kwa hatima, na kuanza kutambua polepole kwamba ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu kwa kweli upo. Kwa kweli hiki ndicho kipindi cha kuanza kukomaa kwa mtu. Baada ya mtu kusita kupambana dhidi ya hatima, na pale ambapo mtu hayuko radhi tena kuvutwa kwenye mabishano, lakini anajua msimamo wake, anajinyenyekeza kwa mapenzi ya Mbinguni, na kujumlisha mafanikio na makosa ya maisha ya mtu huyo, na anasubiria hukumu ya Muumba kwa maisha ya mtu—hiki ni kipindi cha ukomavu. Tukitilia maanani aina hizi tofauti za kile mtu amepitia na kufaidi ambako watu hupata kwenye vipindi hivi vitatu, katika hali za kawaida fursa ya mtu ya kujua ukuu wa Muumba si kubwa sana. Kama mtu ataishi kufikisha umri wa miaka sitini, mtu anayo miaka thelathini tu au karibu na hapo kuujua ukuu wa Mungu; kama mtu atataka kipindi kirefu zaidi cha muda, hilo linawezekana tu kama maisha ya mtu yatakuwa marefu zaidi, tuseme kama mtu ataweza kuishi karne moja. Kwa hivyo Ninasema, kulingana na kanuni za sheria za kawaida za uwepo wa binadamu, ingawaje ni mchakato mrefu sana kuanzia wakati ule mtu anakumbana na mada ya kujua ukuu wa Muumba hadi pale ambapo mtu anaweza kutambua hoja ya ukuu wa Muumba, na kutoka hapo mpaka pale ambapo mtu anaweza kujinyenyekeza kwa utawala huo, kama kwa hakika mtu atahesabu miaka hiyo, miaka hiyo haizidi thelathini au arubaini hivi ambapo mtu anayo fursa ya kufaidi haya yote. Na mara nyingi, watu hujisahau kutokana na matamanio yao na malengo yao ya kupokea baraka; hawawezi kutambua ni wapi ambapo kiini halisi cha maisha ya binadamu kipo, hawang’amui umuhimu wa kujua ukuu wa Muumba, na kwa hivyo hawafurahii fursa hii yenye thamani ya kuingia kwenye ulimwengu wa binadamu kuhusiana na maisha ya binadamu na kile alichopitia, kupitia ukuu wa Muumba, na hawatambui namna lilivyo jambo la thamani kwa kiumbe chochote kilichoumbwa kupokea mwongozo wa kibinafsi kutoka kwa Muumba. Kwa hivyo Ninasema, watu wale wanaotaka kazi ya Mungu kuisha haraka, wanaopenda Mungu angepangilia mwisho wa binadamu haraka iwezekanavyo, ili waweze mara moja kutazama hali Yake halisi na muda si muda kubarikiwa, wanayo hatia ya aina mbaya zaidi ya kutotii na ujinga wa kupindukia. Na kwa wale wanaotamani, kwenye muda wao finyu, kung’amua fursa hii ya kipekee ili kuujua ukuu wa Muumba, hao ni watu werevu, wenye akili zao. Matamanio haya mawili tofauti yanafichua mitazamo miwili tofauti na shughuli za kufuatilia: Wale wanaotafuta baraka ni wachoyo na waovu; hawatilii maanani mapenzi yoyote ya Mungu, wala hawatafuti kujua ukuu wa Mungu, wasiwahi kutamani kujinyenyekeza katika utawala huo, wanataka kuishi tu wanavyopenda. Wao ni watovu wa wema; wao ndio wanaofaa kuangamizwa. Wale wanaotafuta kumjua Mungu wanaweza kuweka pembeni matamanio yao, wako radhi kujinyenyekeza kwa ukuu wa Mungu na mipangilio ya Mungu; wanajaribu kuwa aina ya watu ambao wananyenyekea katika mamlaka ya Mungu na kutimiza tamanio la Mungu. Watu kama hao huishi kwa nuru, huishi katikati ya baraka za Mungu; kwa hakika wataweza kupongezwa na Mungu. Haijalishi ni nini, chaguo la binadamu halina manufaa, binadamu hawana kauli yoyote kuhusiana na muda gani ambao kazi ya Mungu itachukua. Ni bora zaidi kwa watu kujiweka katika udhibiti wa Mungu, kunyenyekea katika ukuu Wake. Usipojiweka katika huruma Yake, ni nini utakachofanya? Je, Mungu atakuwa na hasara yoyote? Usipojiweka katika huruma Yake, ukijaribu kuushika usukani, unafanya chaguo la kijinga, na wewe tu ndiwe utakayepata hasara hatimaye. Endapo tu watu watashirikiana na Mungu haraka iwezekanavyo, endapo tu watafanya hima kukubali mipango Yake, kujua mamlaka Yake, na kutambua yote ambayo Amewafanyia, ndipo watakuwa na tumaini, ndipo maisha yao yatapata maana na kuepuka kuwa hapo tu, ndipo watakapopata wokovu.
Hakuna Anayeweza Kubadilisha Hoja Kwamba Mungu Anashikilia Ukuu juu ya Hatima ya Binadamu
Baada ya kusikiliza kila kitu Nilichomaliza kusema, je, fikira yenu ya hatima imebadilika? Mnaelewa vipi hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Ili kuiweka kwa urahisi, katika mamlaka ya Mungu kila mtu anakubali waziwazi au kimyakimya ukuu Wake na mipangilio Yake, na haijalishi ni vipi ambavyo mtu anashughulika katika mkondo wa maisha yake, haijalishi ni njia ngapi mbovu ambazo mtu ametembelea, mwishowe atarudi tu kwenye mzingo wa hatima ambayo Muumba amempangia yeye. Hii ndiyo hali isiyoshindika ya mamlaka ya Muumba, namna ambavyo mamlaka Yake yanavyodhibiti na kutawala ulimwengu. Ni hii hali ya kutoshindika, mfumo huu wa kudhibiti na kutawala, ambao unawajibikia sheria zinazoamuru maisha ya mambo yote, zinazoruhusu binadamu kuweza kuhama hadi kwenye mwili tofauti baada ya kifo tena na tena bila uingiliaji kati, zinazofanya ulimwengu kugeuka mara kwa mara na kusonga mbele, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka. Mmeshuhudia hoja hizi zote na unazielewa, haijalishi kama ni za juujuu ama ni za kina; kina cha ufahamu wako kinategemea kile unachopitia na maarifa ya ukweli, na maarifa yako kuhusu Mungu. Kujua kwako vyema uhalisia wa ukweli, ni kiwango kipi ambacho umepitia matamshi ya Mungu, ni vipi unajua vyema hali halisi ya Mungu na tabia yake—hii inawakilisha kina cha ufahamu wako wa ukuu na mipangilio ya Mungu. Je, uwepo wa ukuu wa Mungu na mipangilio unategemea kama binadamu wanainyenyekea? Je, hoja kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya inaamuliwa na kama binadamu watayanyenyekea? Mamlaka ya Mungu yapo licha ya hali mbalimbali; katika hali zote, Mungu anaamuru na kupangilia hatima ya kila binadamu na mambo yote kulingana na fikira Zake, mapenzi Yake. Hali hii haitabadilika kwa sababu binadamu hubadilika, na iko huru wala haitegemei mapenzi ya binadamu, haiwezi kubadilishwa na mabadiliko yoyote ya muda, anga, na jiografia, kwani mamlaka ya Mungu ndiyo hali yake halisi kabisa. Kama binadamu anaweza kujua na kuukubali ukuu wa Mungu, na kama binadamu anaweza kuunyenyekea, haiwezi kwa vyovyote vile kubadilisha hoja kwamba ukuu wa Mungu upo juu ya hatima ya binadamu. Hivi ni kusema kwamba, haijalishi ni mtazamo gani ambao binadamu atachukua kwa ukuu wa Mungu, hauwezi tu kubadilisha hoja kwamba Mungu anashikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote. Hata kama hutanyenyekea katika ukuu wa Mungu, angali Anaamuru hatima yako; hata kama huwezi kujua ukuu Wake, mamlaka Yake yangali yapo. Mamlaka ya Mungu na hoja ya ukuu wa Mungu dhidi ya hatima ya binadamu viko huru dhidi ya mapenzi ya binadamu, havibadiliki kulingana na mapendeleo na machaguo yako ya binadamu. Mamlaka ya Mungu yapo kila mahali, kila saa, kila muda. Kama mbingu na nchi zingepita, mamlaka Yake yasingewahi kupita, kwani Yeye ni Mungu Mwenyewe, Anamiliki mamlaka ya kipekee, na mamlaka Yake hayazuiliwi au kuwekewa mipaka na watu, matukio, au vitu, na anga au na jiografia. Siku zote Mungu hushikilia mamlaka Yake, huonyesha uwezo Wake, huendeleza usimamizi Wake wa kazi kama kawaida; kila wakati Anatawala viumbe wote, hutosheleza viumbe wote, huunda na kupangilia viumbe wote, kama Alivyofanya siku zote. Hakuna anayeweza kubadilisha hili. Hii ni hoja; huu umekuwa ukweli usiobadilika tangu zama za kale!
Mtazamo na Matendo Bora ya Mtu Anayependa Kujinyenyekeza katika Mamlaka ya Mungu
Mwanadamu anatakiwa kuwa na mtazamo gani sasa katika kujua na kujali mamlaka ya Mungu, hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Hili ni tatizo la kweli linalokabili kila mmoja. Wakati wa kukabiliana na matatizo ya kweli ya maisha, unafaa kujua na kuelewa vipi mamlaka ya Mungu na ukuu Wake? Wakati hujui namna ya kuelewa, kushughulikia, na kupitia matatizo haya, ni mtazamo gani unaofaa kutumia ili kuonyesha nia yako, tamanio lako, na uhalisia wako wa kujinyenyekeza katika ukuu na mipangilio ya Mungu? Kwanza lazima ujifunze kusubiri; kisha lazima ujifunze kutafuta; kisha lazima ujifunze kujinyenyekeza. “Kusubiri” kunamaanisha kusubiria muda wa Mungu, kusubiria watu, matukio, na mambo ambayo Amekupangilia wewe, kusubiria mapenzi Yake ili yaweze kwa utaratibu kujifichua kwako. “Kutafuta” kunamaanisha kuangalia na kuelewa nia za Mungu katika fikira Zake kwako wewe kupitia watu, matukio, na mambo ambayo Amekuwekea wazi, kuelewa ukweli kupitia mambo hayo, kuelewa kile ambacho binadamu lazima watimize na njia ambazo lazima waendeleze, kuelewa kile ambacho lazima kitimizwe na njia ambazo lazima wahifadhi, waelewe ni matokeo gani ambayo Mungu analenga kutimiza kwa binadamu na ni utimilifu gani Analenga kutimiza ndani yao. “Kujinyenyekeza,” bila shaka, kunaashiria kukubali watu, matukio, na mambo ambayo Mungu amepanga, kukubali ukuu Wake na, kwa yote, kupata kujua namna ambavyo Muumba anaamuru hatima ya binadamu, namna Anavyomjaliza binadamu na maisha Yake, na namna Anavyofanya kazi ya ukweli katika binadamu. Mambo yote katika mipangilio na ukuu wa Mungu hutii sheria za kimaumbile, na kama utaamua kumwachia Mungu kupangilia na kuamuru kila kitu kwa niaba yako, unafaa kujifunza kusubiri, unafaa kujifunza kutafuta, unafaa kujifunza kujinyenyekeza. Huu ndio mtazamo ambao kila mtu anayetaka kujinyenyekeza katika mamlaka ya Mungu lazima awe nao, ubora wa kimsingi ambao kila mmoja anayetaka kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu lazima aumiliki. Ili kushikilia mtazamo kama huu, kumiliki ubora kama huu, lazima mfanye kazi kwa bidii zaidi; na ndipo mnapoweza kuingia kwenye uhalisi wa kweli.
Kumkubali Mungu kama Bwana Wenu wa Kipekee Ndiyo Hatua ya Kwanza katika Kutimiza Wokovu
Ukweli kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni ukweli ambao kila mmoja lazima atilie maanani kwa umakinifu, lazima apitie na aelewe katika moyo wake; kwani ukweli huu unao mwelekeo katika maisha ya kila mmoja, kwenye maisha ya kale, ya sasa, na ya siku za usoni ya kila mmoja, kwenye awamu muhimu ambazo kila mtu lazima apitie maishani, katika maarifa ya binadamu kuhusu ukuu wa Mungu na mtazamo ambao anafaa kuwa nao katika mamlaka ya Mungu, na kawaida, kwa kila hatima ya mwisho ya kila mmoja. Kwa hivyo inachukua nguvu za maisha yako yote kujua na kuyaelewa. Unapochukua mamlaka ya Mungu kwa umakinifu, unapoukubali ukuu wa Mungu, kwa utaratibu utaanza kutambua na kuelewa kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo. Lakini kama hutawahi kutambua mamlaka ya Mungu, hutawahi kukubali ukuu Wake, basi haijalishi ni miaka mingapi utakayoishi, hutafaidi hata chembe maarifa ya ukuu wa Mungu. Kama hutajua na kuelewa kwa kweli mamlaka ya Mungu, basi utakapofika mwisho wa barabara, hata kama utakuwa umesadiki katika Mungu kwa miongo mingi, hutakuwa na chochote cha kuonyesha katika maisha yako, maarifa yako ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu yatakuwa kwa hakika sufuri bin sufuri. Huoni kuwa jambo hili ni la huzuni mno? Kwa hivyo haijalishi umetembea kwa umbali gani maishani, haijalishi unao umri wa miaka mingapi sasa, haijalishi safari inayosalia itakuwa ya umbali gani, kwanza lazima utambue mamlaka ya Mungu na kuyamakinikia, ukubali hoja kwamba Mungu ni Bwana wako wa kipekee. Kutimiza maarifa yaliyo wazi, sahihi na kuelewa ukweli huu kuhusiana na ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni funzo la lazima kwa kila mmoja, ndio msingi wa kuyajua maisha ya binadamu na kutimiza ukweli, ndiyo maisha ya kila siku na mafunzo ya kimsingi ya kumjua Mungu ambayo kila mmoja anakabiliana nayo, na ambayo hakuna yeyote anayeweza kuyakwepa. Kama mmoja wenu angependa kuchukua njia za mkato ili kufikia shabaha hii, basi Ninakuambia, hilo haliwezekani! Kama mmoja wenu anataka kukwepa ukuu wa Mungu, basi hilo nalo ndilo haliwezekani zaidi! Mungu ndiye Bwana wa pekee wa binadamu, Mungu ndiye Bwana wa pekee wa hatima ya binadamu, na kwa hivyo haiwezekani kwa binadamu kuamuru hatima yake mwenyewe, haiwezekani kwake kuishinda. Haijalishi uwezo wa mtu ni mkubwa kiasi kipi, mtu hawezi kuathiri, sikwambii kuunda, kupangilia, kudhibiti, au kubadilisha hatima za wengine. Yule Mungu Mwenyewe wa kipekee ndiye Anayeweza kuamuru tu mambo yote kwa binadamu, kwani Yeye tu ndiye anayemiliki mamlaka ya kipekee yanayoshikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu; na kwa hivyo Muumba pekee ndiye Bwana wa kipekee wa binadamu. Mamlaka ya Mungu yanashikilia ukuu sio tu juu ya binadamu walioumbwa, lakini juu ya hata viumbe ambavyo havikuumbwa visivyoweza kuonekana na binadamu, juu ya nyota, juu ya ulimwengu mzima. Hii ni hoja isiyopingika, hoja ambayo kweli ipo, ambayo hakuna binadamu au kiumbe chochote kinaweza kubadilisha. Kama mmoja wenu angali hajatosheka na mambo kama yalivyo, akiamini kwamba una ujuzi fulani maalum au uwezo, na bado anafikiria unaweza kubahatika na kubadilisha hali zako za sasa au vinginevyo kuzitoroka; kama utajaribu kubadilisha hatima yako kupitia kwa jitihada za binadamu, na hivyo basi kujitokeza kati ya wengine na kupata umaarufu na utajiri; basi Ninakwambia, unayafanya mambo kuwa magumu kwako, unajitakia taabu tu, unajichimbia kaburi lako mwenyewe! Siku moja, hivi karibuni au baadaye, utagundua kwamba ulifanya chaguo baya, kwamba jitihada zako ziliambulia patupu. Malengo yako, tamanio lako la kupambana dhidi ya hatima, na mwenendo wako binafsi wa kupita kiasi, utakuongoza kwenye barabara isiyoweza kukurudisha kule ulikotoka, na kwa hili utaweza kujutia baadaye. Ingawaje sasa huoni ubaya wa athari hiyo, unapopitia na kushukuru zaidi na zaidi ukweli kwamba Mungu ndiye Bwana wa hatima ya maisha, utaanza kwa utaratibu kutambua kile Ninachozungumzia leo na athari zake za kweli. Haijalishi kama kwa kweli unao moyo na, haijalishi kama wewe ni mtu anayependa ukweli, inategemea tu ni mtazamo aina gani ambao utachukua kuhusiana na ukuu wa Mungu na ule ukweli. Na, hili linaamua kama kweli unaweza kujua na kuelewa mamlaka ya Mungu. Kama hujawahi katika maisha yako kuhisi ukuu wa Mungu na mipangilio yake, na isitoshe hujawahi kutambua na kukubali mamlaka ya Mungu, basi utakosa thamani kabisa, bila shaka utakuwa athari ya chukizo na zao la kukataliwa na Mungu, hayo yote ni kutokana na njia uliyochukua na chaguo ulilofanya. Lakini wale ambao, katika kazi ya Mungu, wanaweza kukubali jaribio Lake, kukubali ukuu Wake, kujinyenyekeza katika mamlaka Yake, na kufaidi kwa utaratibu hali halisi waliyopitia na matamshi Yake, watakuwa wametimiza maarifa halisi ya mamlaka ya Mungu, ufahamu halisi wa ukuu Wake, na watakuwa kwa kweli watakuwa wanatii Muumba. Watu kama hao tu ndio watakaokuwa wameokolewa kwa kweli. Kwa sababu wameujua ukuu wa Mungu, kwa sababu wameukubali, shukrani yao ya na kujinyenyekeza kwao katika hoja ya Mungu juu ya hatima ya binadamu ni ya halisi na sahihi. Wanapokabiliana na kifo wataweza, kama Ayubu, kuwa na akili isiyotishika na kifo, kujinyenyekeza katika mipango na mipangilio ya Mungu katika mambo yote, bila chaguo lolote la kibinafsi, bila tamanio lolote la kibinafsi. Mtu kama huyo tu ndiye atakayeweza kurudi katika upande wa Muumba kama kiumbe cha kweli cha binadamu kilichoumbwa.
kutoka katika: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni