II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu
3. Uhusiano Kati ya Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
Maneno Husika ya Mwenyezi Mungu:
Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu.
Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu.
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mnafaa kuelewa kazi ya Yehova, sheria Alizoweka, na kanuni ambazo kwazo Aliyaongoza maisha ya mwanadamu, yaliyomo kwenye kazi Aliyofanya kwenye Enzi ya Sheria, kusudio lililomfanya Yeye kuweka wazi zile sheria, umuhimu wa kazi Yake katika Enzi ya Neema, na kazi anayofanya Mungu kwenye awamu hii ya mwisho. Hatua ya kwanza ni kazi ya Enzi ya Sheria, hatua ya pili ni kazi ya Enzi ya Neema, na hatua ya tatu ni kazi ya siku za mwisho. Lazima muelewe awamu hizi za kazi ya Mungu. … Kazi ifanywayo katika siku za mwisho haiwezi kuwekwa mbadala wa kazi ya Enzi ya Sheria ama ile ya Enzi ya Neema. Ingawa, hatua zote tatu zinaungana kuwa kitu kimoja na yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kawaida, utekelezaji wa kazi hizi umegawanyishwa katika enzi tofauti. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inaleta kila kitu mpaka tamati; ile iliyofanywa katika Enzi ya Sheria ni ya mwanzo; na ile iliyofanywa katika Enzi ya Neema ni ya ukombozi. … Katika siku za mwisho, kazi ya neno pekee inafanyika ili kuukaribisha Wakati wa Ufalme lakini haiwakilishi enzi zile zingine. Siku za mwisho sio zaidi ya siku za mwisho na sio zaidi ya Enzi ya Ufalme, ambayo haiwakilishi Enzi ya Neema au Enzi ya Sheria. Siku za mwisho ni wakati ambapo kazi zote ndani ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita inafuchuliwa kwenu. …
Kazi katika siku za mwisho ni hatua ya mwisho kati ya hizo tatu. Ni kazi ya enzi nyingine mpya na haiwakilishi kazi ya usimamizi mzima. Mpango wa miaka elfu sita umegawawa katika hatua tatu za kazi. Hakuna hatua moja pekee itakayowakilisha kazi ya enzi hizo tatu ila inaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya yote. Jina Yehova haliwezi kuwakilisha tabia yote ya Mungu. Ukweli kuwa Alitekeleza kazi katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kuwa Mungu Anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria. Yehova alitengeneza sheria kwa mwanadamu na kutoa amri, Akimuuliza mwanadamu ajenge hekalu na madhabahu; kazi Aliyofanya inawakilisha tu Enzi ya Sheria. Kazi Alioyoifanya haidhibitishi kuwa Mungu ni Mungu Anayemwamuru mwanadamu kufuata sheria, Mungu Aliye hekaluni, ama Mungu Aliye mbele ya madhabahu. Haya hayawezi kusemwa. Kazi chini ya sheria inaweza tu kuwakilisha enzi moja. Kwa hivyo, kama Mungu Alifanya kazi katika Enzi ya Sheria pekee, mwanadamu angemfafanua Mungu na kusema, "Mungu ni Mungu Aliye hekaluni. Ili kumtumikia Mungu, lazima tuvae mavazi ya kikuhani na tuingie hekaluni." Iwapo kazi katika Enzi ya Neema haingetekelezwa na Enzi ya Sheria ingeendelea mpaka wakati huu wa sasa, mwanadamu hangefahamu kuwa Mungu pia ni mwenye huruma na upendo. Iwapo kazi katika Enzi ya Sheria haingefanywa, na kwamba tu ile ya Enzi ya Neema ndiyo iliyofanywa, mwanadamu angefahamu tu kwamba Mungu Anakomboa mwanadamu na kumsamehe dhambi zake. Wangefahamu tu kuwa Yeye ni mtakatifu na asiye na hatia, kwamba Anaweza kujitoa kafara na kusulubishwa kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu angejua tu kuhusu haya na asiwe na ufahamu wa mambo mengine yoyote. Kwa hivyo kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu. Enzi ya Sheria inawakilisha vipengelele vingine, Enzi ya Neema vipengele vingine na enzi hii vipengele vingine. Tabia ya Mungu inaweza tu kuonekana kwa mchanganyiko wa hatua zote tatu. Ni wakati tu mwanadamu anajua hatua hizi tatu ndipo anaweza kuipokea kikamilifu. Hakuna hatua kati ya hizo tatu ambayo inaweza kuachwa. Utaiona tu tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake mara tu utakapozijua hatua hizi tatu za kazi. Mungu kukamilisha kazi yake katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kwamba Yeye ni Mungu chini ya sheria, na kukamilika kwa kazi Yake ya ukombozi haionyeshi kuwa Mungu Atamkomboa mwanadamu milele. Hizi zote ni hitimisho zilizofanywa na mwanadamu kuhusu jambo hilo. Enzi ya Neema imefika mwisho, lakini huwezi kusema kuwa Mungu ni wa msalaba tu na kuwa msalaba unawakilisha wokovu wa Mungu. Ukifanya hivyo, basi utakuwa unamfasili Mungu. Katika hatua hii, Mungu Anafanya zaidi kazi ya Neno, lakini huwezi kusema kuwa Mungu hajawahi kuwa Mwenye huruma kwa mwanadamu na kwamba yote Aliyoleta ni kuadibu na hukumu. Kazi katika siku za mwisho inaonyesha wazi kazi ya Yehova na ile ya Yesu na mafumbo yote yasioeleweka na mwanadamu. Hii inafanywa ili kuonyesha hatima na mwisho wa binadamu na kukamilisha kazi yote ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Hatua hii ya kazi katika siku za mwisho huleta kila kitu kufika mwisho. Mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu lazima yaelezwe ili kumpa mwanadamu ufahamu na kuweza kuelewa kwa kina katika mioyo yao. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kugawanywa kulinga na aina zao. Baada tu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilishwa ndipo mwanadamu atapata kuelewa tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake, kwani usimamizi Wake utakuwa umefika mwisho.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imekoma, kazi ya Mungu imeendelea sana. Kwa nini Ninazungumza mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajenga juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya wakati huu ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na kuinua kazi ile iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata. Kwa nini pia Ninasema kwamba hatua hii ya kazi inajenga juu ya kile kilichofanywa na Yesu? Tuseme kwamba hatua hii haingeongezea juu ya kazi iliyofanywa na Yesu, ingebidi Asulubiwe tena katika hatua hii, na kazi ya ukombozi ya hatua iliyopita ingelazimika kufanywa upya tena. Hii isingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo, sio kwamba kazi imekamilika kabisa, bali ni kwamba enzi imesonga mbele, na kazi imekuwa ya juu kabisa kuliko ilivyokuwa kabla. Inaweza kusemwa kwamba hatua hii ya kazi imejengwa juu ya msingi wa Enzi ya Sheria na katika mwamba wa kazi ya Yesu. Kazi hii imejengwa hatua kwa hatua, na hatua hii sio mwanzo mpya. Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita.
kutoka kwa "Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Hatua ya kazi ya mwisho haisimami peke yake, ila ni sehemu ya yote iliyounganishwa pamoja na hatua mbili za awali, ambayo ni kusema kwamba haiwezekani kukamilisha kazi nzima ya wokovu kwa kufanya kazi ya hatua moja pekee. Ingawa hatua ya mwisho ya kazi inaweza kumwokoa mwanadamu kabisa, hii haimaanishi kwamba ni muhimu tu kutekeleza hatua hii pekee, na kwamba hatua mbili za hapo awali hazihitajiki kumwokoa mwanadamu kutokana na ushawishi wa Shetani. Hakuna hatua moja kati ya zote tatu inayoweza kuwekwa kama maono ya kipekee ambayo lazima yajulishwe mwanadamu, kwa kuwa ukamilifu wa kazi ya wokovu ni hatua tatu za kazi, wala si hatua moja kati ya tatu. Ilimradi kazi ya wokovu bado haijakamilishwa, usimamizi wa Mungu utashindwa kufikia kikomo. Nafsi ya Mungu, tabia, na hekima zimeonyeshwa katika ukamilifu wa kazi ya wokovu, wala hazikufichuliwa kwa mwanadamu hapo mwanzo, lakini zimeonyeshwa hatua kwa hatua katika kazi ya wokovu. Kila hatua ya kazi ya wokovu huonyesha sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya nafsi Yake: si kila hatua ya kazi inayoweza moja kwa moja kuonyesha kabisa na kwa ukamilifu nafsi ya Mungu. Kwa hivyo, kazi ya wokovu inaweza tu kuhitimishwa hatua tatu za kazi zitakapokamilika, na kwa hivyo, maarifa ya mwanadamu ya ukamilifu wa Mungu hayawezi kutenganishwa na hatua tatu za kazi ya Mungu. Kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa hatua moja ya kazi ni tabia ya Mungu inayoonyeshwa katika sehemu moja ya kazi yake tu. Haiwezi kuwakilisha tabia na nafsi inayoonyeshwa katika hatua ya awali na ijayo. Hii ni kwa sababu kazi ya kumwokoa mwanadamu haiwezi kumalizika mara moja katika kipindi kimoja, ama katika eneo moja, lakini hukuwa kwa kina hatua kwa hatua kulingana na kiwango cha kukua kwa mwanadamu katika wakati na maeneo tofauti. Ni kazi inayofanywa hatua kwa hatua, na haikamilishwi katika hatua moja. Na kwa hiyo, hekima yote ya Mungu imejumuishwa katika hatua tatu, badala ya hatua moja. Nafsi yake yote na hekima yake yote zimewekwa wazi katika hatua hizi tatu, na kila hatua ina nafsi Yake, na ni rekodi ya hekima ya kazi Yake. … Kila moja ya hatua tatu za kazi huendelea juu ya msingi wa hatua iliyopita; haitekelezwi peke yake, tofauti na kazi ya wokovu. Ingawa kuna tofauti kubwa katika enzi na aina ya kazi ambayo inafanywa, katika kiini chake bado ni wokovu wa mwanadamu, na kila hatua ya kazi ya wokovu ina kina kuliko iliyopita.
kutoka kwa "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Usimamizi mzima wa Mungu umegawika kwa hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayopatana yanatokana na mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu huongezeka hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa "kuonekana kwa Neno katika mwili," na hivyo mahitaji ya mwanadamu huongezeka hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huongezeka hata zaidi. … Wakati wa kale, mwanadamu alihitajika kuzingatia sheria na amri, na alihitajika kuwa mpole na mnyenyekevu. Leo, mwanadamu anahitajika kutii mipango yote ya Mungu na awe na upendo mkuu wa Mungu, na zaidi bado anahitajika kumpenda Mungu katika mateso. Hatua hizi tatu ndizo Mungu anazozitazamia toka kwa mwanadamu, hatua kwa hatua, katika usimamizi Wake wote. Kila hatua ya kazi ya Mungu huzidisha kina kuliko iliyopita, na katika kila hatua, mahitaji ya mwanadamu ni makubwa kuliko yaliyopita, na kwa hali hii, umbo la usimamizi mzima wa Mungu huonekana. Ni hasa kwa sababu mahitaji ya mwanadamu kila mara huwa juu kuliko tabia yake inavyoweza kufikia viwango anavyovihitaji Mungu, na ni hapo ambapo wanadamu wataanza kujiondoa polepole kutoka kwa ushawishi wa Shetani, ndipo kazi ya Mungu itafikia kikomo, wanadamu wote watakuwa wameokolewa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Wakati huo utakapowadia, kazi ya Mungu itakuwa imefika mwisho, na ushirikiano wa mwanadamu na Mungu ili abadilishe tabia zake hautakuwepo, na wanadamu wote wataishi kwenye nuru ya Mungu, na kuanzia hapo kuendelea, hapatakuwa na uasi au upinzani wowote kwa Mungu. Aidha Mungu hatamwekea matakwa mwanadamu, na patakuwepo na ushirikiano mwema zaidi kati ya mwanadamu na Mungu, mojawapo ikiwa maisha ya mwanadamu na Mungu pamoja, maisha ambayo yatafuatia baada ya usimamizi wa Mungu kukamilishwa, na baada ya mwanadamu kuokolewa toka katika mafumbato ya Shetani.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi mzima ya mpangilio wa usimamizi wa Mungu inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe. Awamu ya kwanza—uumbaji wa ulimwengu—ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na kama haikuwa hivyo, basi hakuna yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kumuumba mwanadamu; awamu ya pili ilikuwa ukombozi wa wanadamu wote, na pia ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, awamu ya tatu inaenda bila kusemwa: Kuna haja kuu zaidi ya mwisho wa kazi ya Mungu kufanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya ukombozi, ushindi, kumpata, na kumkamilisha wanadamu wote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kama hangefanya kazi hii Yeye binafsi, basi utambulisho wake hauwezi kuwakilishwa na mwanadamu, au kazi kufanywa na mwanadamu. Ili kumshinda Shetani, ili kumpata mwanadamu, na ili kumpa mwanadamu maisha ya kawaida duniani, Yeye binafsi humwongoza mwanadamu na hufanya kazi binafsi miongoni mwa wanadamu; kwa ajili ya mpangilio mzima wa usimamizi, na kwa kazi yake yote, ni lazima Yeye binafsi afanye kazi hii.
kutoka kwa "Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Hatua tatu za kazi ambazo zilifanywa tangu mwanzo hadi leo zote zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe, na zilitekelezwa na Mungu mmoja. Ukweli wa hatua tatu za kazi ni ukweli wa uongozi wa Mungu kwa wanadamu wote, ukweli ambao hakuna anayeweza kuupinga. Mwishoni mwa hatua tatu za kazi, vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina na kurejea chini ya utawala wa Mungu, kwa kuwa duniani kote kuna Mungu mmoja tu, na hakuna dini nyingine.
kutoka kwa "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama una maarifa wazi ya hatua tatu za kazi—ambapo ni kusema kwamba, ya mpango mzima wa usimamizi wa Mungu—na ikiwa utaweza kupatanisha hatua mbili za awali na hatua ya sasa, na unaweza kuona kwamba ni kazi iliyofanywa na Mungu Mmoja, basi utakuwa na msingi imara zaidi. Hatua tatu za kazi zilifanywa na Mungu mmoja; haya ndiyo maono makubwa zaidi, na ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Hatua tatu za kazi zingefanywa tu na Mungu Mwenyewe, na hapana mwanadamu yeyote ambaye angeweza kufanya kazi kama hii kwa niaba Yake—ambayo ni kusema kuwa ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye angeifanya kazi Yake toka mwanzo hadi leo.
kutoka kwa "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni