Alhamisi, 22 Novemba 2018

Maneno ya Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?"(Official Video)


Neno la Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?"(Official Video)

    Mwenyezi Mungu anasema, "Unapaswa kuona kuwa mapenzi Yake na kazi Yake si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Kwa sababu kazi ya leo ni kubadilisha wale waliopotoshwa, wale waliokufa ganzi, na kutakasa walioumbwa kisha kushughulikiwa na Shetani, si kuumba Adamu na Hawa, ama hata kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake. Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayvodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake."

    Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, umepokea utukufu mkuu na wokovu wa Mungu kabisa. Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu wake kutoka kwa Israeli, watu wake wateule, hadi kwako, ili kufanya kusudio lake lijidhihirishe kwenu kama kundi. Kwa hiyo, ninyi ndinyi mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu. Pengine utayakumbuka maneno haya: “Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.” Zamani, mlisikia msemo huu, lakini hakuna aliyeelewa maana kamili ya maneno yale. Leo, unajua vyema umuhimu wa maneno yale. Maneno haya ndiyo yatakayotimizwa na Mungu katika enzi za mwisho. Yatatimia kwa wale walioteswa na joka kuu jekundu katika sehemu linakoishi. Joka kuu jekundu humtesa Mungu na ni adui wa Mungu, kwa hiyo katika nchi hii, wanaomwamini Mungu wanateswa na kudhihakiwa. Ndiyo sababu maneno haya yatakuja kuwa kweli kwenu nyie kundi la watu. Kazi inapotekelezwa katika nchi inayompinga Mungu, kazi Yake yote inakabiliwa na vizuizi vya kupita kiasi, na mengi ya maneno Yake hayawezi kutimizwa katika wakati ufaao: ndiyo maana, watu husafishwa kwa ajili ya neno la Mungu. Hiki pia ni kipengele cha mateso. Ni vigumu kabisa kwa Mungu kutekeleza kazi yake katika nchi yenye joka kuu jekundu, lakini ni kupitia ugumu huu ndipo Mungu Hupiga hatua katika kazi Yake ili kudhihirisha hekima Yake na matendo Yake ya ajabu. Mungu Huchukua fursa hii kuwakamilisha watu hawa wa kikundi hiki. Kwa ajili ya mateso ya watu, tabia yao na hulka ya kishetani ya watu katika nchi hii najisi, Mungu Anafanya kazi Yake ya kutakasa na ushindi, ili, kutokana na hili, apokee utukufu na kuwapata wale wote wanaoshuhudia matendo Yake. Huu ndio umuhimu wa kujitoa kwa Mungu kwa ajili ya kikundi hiki cha watu. Ina maana kuwa Mungu hufanya kazi ya ushindi kupitia wale wanaompinga. Kwa hiyo, kufanya vile kunadhihirisha nguvu za Mungu. Kwa maneno mengine, ni wale tu walio katika nchi najisi ndiyo wanaostahili kuurithi utukufu wa Mungu na ni hili tu ambalo litafanya nguvu kuu za Mungu kuwa maarufu. Ndiyo maana Nasema kuwa utukufu wa Mungu unapatikana katika nchi najisi na kwa wale wanaoishi humo. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu. Hii ni kama tu ilivyokuwa katika kazi ya Yesu; Angetukuzwa tu kati ya Wafarisayo waliomdhihaki. Isingelikuwa mateso na usaliti wa Yuda, Yesu asingelidhihakiwa na kudharauliwa, na hata zaidi kusulubiwa, na hivyo asingelipokea utukufu. Kila mara Mungu Anapofanya kazi katika wakati fulani na kila mara anapofanya kazi Yake kwa kupitia mwili, huwa Anapokea utukufu na papo hapo huwapata Anaotaka kuwapata. Huu ndio mpango wa kazi ya Mungu na hivi ndivyo anavyosimamia kazi Yake.

Kujua zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni