Ijumaa, 13 Julai 2018

Tofauti kati ya mtumishi mzuri na mtumishi mwovu ni ipi❓


Tofauti kati ya mtumishi mzuri na mtumishi mwovu ni ipi❓ 📚Mungu alisema, "Wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa marafiki...



Mungu alisema, "Wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa marafiki wema wa Mungu, wanapaswa kupendwa na Mungu, na kuwa na uaminifu wa hali ya juu kwa Mungu. Bila kujali iwapo unatenda bila kuonekana na watu, au mbele ya watu, unaweza kupata furaha ya Mungu mbele za Mungu, unaweza kusimama imara mbele za Mungu, na bila kujali jinsi watu wengine wanavyokutendea, wewe huifuata njia yako mwenyewe kila mara, na kuushughulikia kwa makini mzigo wa Mungu. Mtu wa aina hii pekee ndiye rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu wanaweza kumhudumia Yeye moja kwa moja kwa sababu wamepewa agizo kuu la Mungu, na mzigo wa Mungu, wao wanaweza kuuchukulia moyo wa Mungu kama moyo wao wenyewe, na mzigo wa Mungu kama mzigo wao wenyewe, na hawazingatii iwapo watafaidi au watapoteza matarajio: Hata wasipokuwa na matarajio, na hawatafaidi chochote, watamwamini Mungu daima kwa moyo wa upendo. Kwa hivyo, mtu wa aina hii ni rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu ni wasiri Wake pia; ni wasiri wa Mungu pekee ndio wanaoweza kushiriki katika kutotulia Kwake, matamanio Yake, na ingawa mwili wao una uchungu na ni mdhaifu, wanaweza kuvumilia uchungu na kuacha kile wanachokipenda ili kumridhisha Mungu. Mungu huwapa watu wa aina hii mizigo mingi, na kile ambacho Mungu atafanya hudhihirishwa kupitia kwa watu hawa. Yaani, watu hawa wanapendwa na Mungu, wao ni watumishi wa Mungu wanaoupendeza moyo Wake, na ni watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza kutawala pamoja na Mungu. Ukishakuwa rafiki mwema wa Mungu ndipo utakapoweza kabisa kutawala pamoja na Mungu." kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
"Kumhudumia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe kumhudumia Mungu. Kama tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa na neno la Mungu, basi tabia yako bado inawakilisha Shetani. Hii inatosha kuthibitisha kwamba huduma yako kwa Mungu ni kutokana na nia yako nzuri wewe binafsi. Ni huduma inayotokana na asili yako ya kishetani. Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi , unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi, na kazi yako inaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe. Kwa hakika, utakuwa msumbufu zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hii ni uzoefu na mafunzo ya kibinadamu. Ni filosofia ya maisha ya binadamu. Watu kama hawa wanapatikana miongoni mwa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hatimaye watageuka na kuwa wale Mkristo wa uwongo watakaoonekana siku za mwisho. Watakuwa wadanganyifu. Mkristo wa uwongo na wadanganyifu waliozungumziwa watatokana na aina ya watu kama hawa. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi watakuwa katika hatari isiyoisha ya kutupwa nje. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kusomea na kuwadhibiti watu, kujiinua wao wenyewe—na wale katu hawatubu, katu hawakiri, katu hawakatai nguvu manufaa ya cheo—watu hawa watasambaratika mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu. Watu wanapenda kushikilia vitu vya kale. Wanashikilia fikira za kale, wanashikilia vitu vya kale. Hiki ni kizuizi kikuu katika huduma yao. Kama huwezi kudondosha vitu hivi, vitu hivyo vitayakaba maisha yako yote. Mungu hatakupongeza, hata kwa uchache wowote, hata kama utapoteza miguu yako au kuuvunja mgongo wako ukitia bidii, au hata kuuliwa ukiwa katika “huduma” ya Mungu. Kinyume cha Mambo ni kwamba: Atasema wewe ni mtenda maovu." kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni