Latest Christian Movie Swahili "Imani katika Mungu"
Yu Congguang huhubiri injili kwa niaba ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wakati wa kuhubiri injili, aliandamwa na serikali ya Kikomunisti ya China. Alikimbia milimani, ambapo alipokea msaada kutoka kwa Zheng Xun, mfanyakazi mwenza wa kanisa la nyumba la mahali pale. Walipokutana mara ya kwanza, walihisi kama tayari walikuwa wamejuana kwa muda mrefu. Zheng Xun alimpeleka Yu Congguang kwenye kibanda cha makuti ambapo yeye na wafanyakazi wenzake walikusanyika. Huko, mjadala ulijitokeza miongoni mwa Zheng Xun na wafanyakazi wenzake kuhusu kama muumini katika Mungu anapaswa kutii wale walio madarakani au la.
Yu Congguang alitoa ushirika kwa kuzingatia suala hili na kuondoa kuchanganyikiwa kwao. Ushirika wa Yu Congguang ulikuwa wa manufaa sana kwao, na wote wakaanza kutafuta na kujifunza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Hata hivyo, Mzee Sun kutoka kanisa la mahali pale alipopata habari kwamba Yu Congguang alikuwa shahidi kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu, alifanya kila kitu ambacho angeweza kulizuia kanisa na kuwazuia wafuasi kutafuta njia ya kweli. Sun alikwenda katika nyumba moja hadi nyingine kumtafuta Yu Congguang, na hata kuwahamasisha wafuasi kumripoti Yu kwa polisi na kumkamata …
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni