Sura ya 30. Kumtumikia Mungu Mtu Anapaswa Kutembea Njia ya Petro |
Sura ya 30. Kumtumikia Mungu Mtu Anapaswa Kutembea Njia ya Petro
Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi hawawezi kuainisha ni watu gani wana ukweli, watu gani hawana ukweli na watu gani husema mambo yaliyo na ukweli. Unapoulizwa kueleza ni nini maana ya "ukweli," huwezi kueleza kwa wazi. Lakini mara tu mtu anaposema kitu, unasema: “Mtazamo wake ni wa kweli. Maneno ayasemayo yanaonyesha ufahamu wa utendaji uliopatikana kupitia kwa uzoefu.”
Unaelewa mara tu unapowasikia wakizungumza. Kwa ninyi hapa mlio wapya, Nikiwauliza ni nini maana ya 'uhalisi,' hamtaweza tu kunijibu, lakini pia hamtaweza kueleza tofauti kati ya mtu anayezungumza uhalisi na mtu anayezungumza mafundisho ya dini. Hili halisemwi kuwadunisha ninyi, ni tu kwamba hamna uzoefu. Tazama wale wakongwe wa kanisa; ingawa washawishi wengine wa kufanya mengi huenda wakawakanganya na vitu wasivyoweza haswa kutambua sababu sahihi, bado wanajua kwamba wanachosema watu hao si sahihi. Wanaweza kutambua ni watu gani wanazungumza mafundisho ya dini, na watu gani wanazungumza uhalisi. Ninyi, kwa hali yoyote, hata bado hamjababia. Hili halisemwi kuwashushia hadhi, kwa hivyo msione vibaya kwa sababu ya hili. Hii ni njia ya kawaida ya uzoefu ambayo kila mtu ni lazima apitie. Kila mtu ni lazima apitie miaka mingi ya kunyunyiziwa maji, kufanyiwa uchunguji, kusikiliza, kuhisi, kutambua na kupitia kabla ya kufahamu polepole lakini kwa kina uzoefu wa maisha, kabla ya kuvuka lango na kufungua macho yao. Ukizungumza tu mafundisho ya dini na kusikia mafundisho ya dini, ikiwa huwezi kutambua masuala yanayohusu uhalisi na usiwe na utambuzi, basi macho yako hayajafunguliwa; bado tu hayajafunguliwa. Ni nini maana ya "macho yako hayajafunguliwa"? Inamaanisha bado hujavuka lango, na huo ni ukweli. Inamaanisha kwamba hujavuka lango panapohusiana na ukweli. Jitazameni sasa. Labda unaweza kufanya kazi ya uchungaji, kuwasaidia wengine, kutoa msaada na kutumia, au kufanya mambo mengine ya desturi katika familia ya Mungu. Lakini wewe hasa huna uhalisi, wala hutakuwa hasa na utambuzi wowote wa kufikia uhalisi au kufikia nyaraka na mafundisho ya dini. Labda hamjaridhishwa na hili, mpaka siku moja mtu fulani aje anayezungumza mafundisho ya dini, aliye na maneno ya kushawishi, na kisha huenda mtamkweza. Na wakati mtu yule aliye na uhalisi wa kweli ajapo, aliye kimya, asiyetoa sauti, basi huenda mtamdharau. Mara mnapofanya hivi, wakati huo mtajua kimo chenu wenyewe kiko wapi. Ndio, kimo cha mwanadamu, ufahamu wa mtu kuhusu uhalisi na wa mtu mwenyewe, uzoefu wa mtu kuhusu kweli, ufahamu wa mtu kuhusu Mungu—mambo haya yote hutokana na uzoefu, hutokana na kuishi siku baada ya siku, hili ni wazi na dhahiri. Vitu hivi bila shaka havitokani na kusoma wala kutoka kwa mambo mangapi uliyoyasikia. "Nina mambo haya, nimeyasikia na ninayakumbuka. Kiwango changu cha maarifa kiko juu sana, mimi ni mwanafunzi wa chuo, ninafanya kazi fulani, ninachunguza jambo fulani, na mimi huyajua mambo mara tu niyasikiapo." Unaweza kutumia maarifa uliyojifunza kusikia falsafa, siasa au fasihi. Lakini huwezi kuyatumia hapa, hayana maana! Tuna nini hapa, basi? Maarifa uliyojifunza huenda yakakusaidia kujua maneno yaliyoandikwa ya ukweli au kuhusu vile yameelezwa vizuri zaidi kuliko wengine, lakini wewe si bora kuliko wengine inapohusu wewe kuupitia ukweli; huna heri kuhusiano na hilo. Mnalikubali hili, sivyo? Hamchunguzi masuala ya uzoefu wa maisha na mnakosa mambo mengi sana. Lakini kwa ninyi ambao mna maarifa fulani, ambao sasa mko katika nafasi ya heri ya kuwa kiongozi juu ya watu wengine, ambao mko kazini mara kwa mara na ambao hukutana na wakongwe wa kanisa walio katika viwango vya juu, na ambao hufanya kazi fulani maalum, mnaweza kuendelea haraka zaidi. Mnaweza kuendelea haraka sana kuliko vile wale wakongwe wa kanisa wangeweza hapo awali, haraka na ufahamu wenu wa uhalisi, na hali yoyote ya ukweli na kwa kujifahamu wenyewe. Labda hamtatembea katika njia inayopinda au labda ninyi pia mtahitajika kupatwa na vipingamizi fulani. Hali ya kila mtu ni tofauti, hali zao ni tofauti. Watu wengine wanahitajika kupatwa na vipingamizi fulani kabla ya kuweza kupitia mabadiliko makuu. Na kisha kuna watu wengine ambao hawahitaji kupatwa na vipingamizi vikubwa, lakini hugundua njia wanayopaswa kutembea na upotovu wao wenyewe katika mambo yanayotendeka kandokando yao, na wao hupata ujuzi fulani katika watu, mambo na vitu vilivyo kandokando yao—huyu ni mtu anayeendelea upesi sana kwa kulinganisha.
Hivyo mnapaswa kuzingatia nini sasa? Ikiwa mtazingatia tu kuyafanyia kazi na kujishughulisha na mambo ya ukingoni, basi maendeleo yenu yatacheleweshwa. Mnapoamini katika Mungu, maendeleo yenu binafsi maishani ni muhimu zaidi na ni ya maana zaidi. Huenda ukajiandaa tu na mafundisho ya dini, au na uwezo wa kufanya kazi, au huenda ukafanya jambo fulani kwa kutumia mbinu fulani nzuri sana, au kwa hekima; mambo haya yote ni ya kufuata, ingawa bado huwezi kuendelea bila hayo. Suala kuu la imani yako kwa Mungu ni kwamba lazima uujue ukweli kabisa, upitie ukweli na uwe na ufahamu fulani wa ukweli, na uweze kuwa na moyo mtiifu na kutosheleza mapenzi ya Mungu mbele Yake. Iwapo unaamini katika Mungu lakini kadri unavyoamini, ndivyo uhusiano wako na Mungu unaenda mrama, ndivyo unavyosonga mbali zaidi na Mungu na ndivyo unavyokuwa na sehemu nyingi ndani yako zinazopingana na ukweli, basi hilo linathibitisha kwamba imani yako haikuongozi kuendelea, kwamba Roho Mtakatifu hajakushughulikia, na kwamba umepotea na umevuka mipaka. Iwapo unaamini kwa kipindi fulani na kisha unakuwa na ufahamu fulani wa uhalisi, kujifahamu kwa kiasi fulani, na ufikirie umeelewa mambo fulani ya uhalisi, basi hili linathibitisha kwamba unafahamu mambo ya kiroho, macho yako yamefunguka na unatembea katika njia sahihi. Kuna wakongwe wengine sasa ambao wamefuata kwa miaka miwili au mitatu, ambao hata hawajababia, ambao ni waasi na wasiozuiwa na ambao hujitayarisha kupokea baraka, ambao wanajitayarisha kufurahia utajiri wao mzuri baada ya kazi kukamilishwa. Hata bado hawajababia kulingana na uzoefu wa maisha, na hawana uhusiano wenye upatanifu na Mungu hata kidogo. Ni vyema kuwa nao kwa kipindi kifupi, na watatii shingo upande, na hawatathubutu kutoa sauti ikiwa wana dhana. Lakini baada ya muda fulani kupita, mara tu wanapoanza kupinga, wanakuwa vyombo vya kuangamia. Kila mtu yuko juu ya ardhi hatari, na hili ni jambo la kuogofya. Ikiwa unamwamini Mungu na unatembea kwenye njia sahihi, basi imani yako ni muafaka na utapata baraka. Ikiwa utaenda kombo, ukitembea kwenye njia isiyo sahihi au njia isiyonyooka, usipoendelea mbele, usipoendelea mbele kwa uwezo wako wote, basi utaangamia na utapata adhabu.
Watu wana njia mbili za imani katika Mungu: Moja ni kuweza kumwamini Mungu kabisa; na nyengine ni kumuasi Mungu na kumpinga Yeye. Hizi ndizo njia mbili pekee. Haiwezekani kwamba humpingi Mungu lakini pia humtii Yeye; hili haliwezekani. Ikiwa humtii Mungu na huna ufahamu halisi, basi unaweza tu kuwa mkaidi na muasi. Huenda usionyeshe uasi kwa mambo unayosema, na huenda usimpinge Yeye waziwazi kwa silaha zilizochukuliwa, lakini bado moyo wako ni mkaidi. Au iwapo huulizwi kufanya jambo, huenda ukahisi umejawa na upendo kwa Mungu na kuhisi uko karibu sana na Mungu. Lakini mara tu unapoulizwa kufanya jambo, basi ukaidi wako, kiburi chako, kujidai kwako na mambo yako ya Shetani hufichuliwa; mara tu yanapofichuliwa, basi ukaidi wako unakuwa wa kweli. Je, si hivyo? Huenda ukaichukulia imani yako kwa Mungu kama tu "Mimi nimebarikiwa kwa kuamini katika Mungu na baadaye nitakuwa chombo cha baraka Zake. Mimi ni mshirika wa familia ya Mungu na mimi nimeinuliwa na Mungu; mimi ni mtu aliyekwezwa na Mungu. Nimebarikiwa na Mungu ni mwema kwangu." Lakini ikiwa unliona kwa njia hii, kuna maana gani? Kuna maana gani kupiga makelele kwa maneno haya matupu yanayorudiwarudiwa? Jambo kuu sasa ni iwapo unaweza kuokolewa au la, iwapo unatembea kwa njia sahihi ya maisha au la, iwapo Mungu anakusifu katika imani yako au la, iwapo Mungu anakubali kuwa kwako mshirika wa familia ya Mungu au la, na iwapo Mungu anakukubali au la; ni hayo tu ndiyo yanaweza kuchukuliwa kama kuwa makini katika imani yako kwa Mungu. Imani ya kipumbavu, kama vile "Ah, Mungu ni mwema kwangu, Mungu hunifadhili, nimebarikiwa na mimi hufanikiwa kila mahali. Tazama, Mungu ameniinua na kunifanya kuwa kiongozi katika familia Yake. Nimekuwa na bahati sana na nyota yangu imekuwa ikiinuka tangu nilipokuja katika familia ya Mungu." Kuringia tu jambo la aina hii hakuna maana. Ni tupu; lisilo na maana! Ikiwa umepewa nafasi lakini huishikilii upesi, basi ilitolewa bure, na hakutakuwa na maana hata ukipewa nafasi nyingi kiasi gani. Shikilia upesi mambo fulani ya kweli, na halisi. Baadhi ya waumini wakongwe husema: "Ah, nimebarikiwa! Mimi nimebarikiwa na mimi ni mtu aliyebarikiwa zaidi katika dunia yote, katika ulimwengu wote!" Haingekusaidia hata ungekuwa malaika; huwezi tu kusema mambo ya aina hii, ni lazima ushikilie upesi mambo ya kweli. Hasa ninyi ambao mumeamini katika Mungu kwa muda mfupi tu na mmepata uzoefu kidogo kutokana na kufanya mambo, ambao hamkupitia zile hatua za kazi hapa mwanzo, na ambao mlikuja mwisho kabisa—je, uko tayari kuwa na uhakika kabisa ili baadaye uweze kuokolewa? Je, uko tayari? Huko tayari, sivyo? Ikiwa huko tayari kuwa na uhakika kabisa kuhusu jambo hilo, basi uko katika nafasi hatari!
Ikiwa huelewi ni nini maana ya kumhudumia Mungu au nini maana ya kutii Mungu, na unaelewa kidogo sana namna ya kumwabudu Mungu au jinsi watu wanapaswa kuamini katika Mungu; iwapo hujashikilia mambo haya na huyafahamu katika moyo wako, basi utaenda mrama kwa urahisi sana na utamuasi Mungu kwa urahisi sana. Kama wale walioanguka hapa awali waliosema: "Roho Mtakatifu na atufunulie mambo haya!" Ninyi nyote sasa mnaona jambo hili kwa dhahiri. Wakati huo hawakuwa na nia yoyote ya kufanya chochote kibaya na kumuasi Mungu, na walijua kwmba Mungu alikuwa amewainua na kwamba ni lazima wafanye kazi kwa bidii. Ilhali hawakutembea kwenye njia sahihi, wakifikiria tu kwamba Mungu alikuwa amewainua, kwamba walitaka kufanya kazi kwa bidii, na kufanya kazi nzuri ya kuwa wachungaji wa wale waliokuwa chini yao kanisani; walidhani chochote kile ambacho waliokuwa juu yao waliwataka wafanye, wangefanya. Hawakuwa wameshika mambo ya utendaji na hakika walikuwa wanafanya mambo bila kutambua, wakitegemea ushupavu wao wenyewe. Walipokuwa hawatumiwi tena, walikasirika sana na kusema: "Mungu ni mwenye haki. Roho na afichue hili! Imani yangu haiko katika mwanadamu, iko katika Mungu." Hawakupanga awali kusema maneno haya, hivyo yalisemwa bila hiari? Sababu yake ilikuwa gani? Ilikuwa ni kwa sababu mwanadamu hamchi Mungu na hamfahamu Yeye. Unaona kwamba watu wengine husema mambo mengine ambayo ni ya upumbavu na ujinga, na wao husamehewa. Wao husamehewa kwa ajili ya ujinga wao na kile ambacho wajibu wao ulikuwa hakichunguzwi. Mbona hali si hiyo kwa watu wengine? Kwa sababu walisema mambo yaliyokuwa mazito sana: "Wewe ni Mungu, lakini bado sitakutii Wewe." Watu hawa ni wapinga Kristo; wao humuasi Mungu na hawakubali ukweli. Watu wengine ni wapumbavu na wajinga. Ni sawa kuonyesha upumbavu wako na ujinga mara moja au mara mbili; lakini ukikosea amri za Mungu za usimamizi au ukikosea tabia ya Mungu, basi utakuwa matatani. Tazama njia ambayo Petro alitembea. Alipata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu hapo mwanzo na alizungumza na Yesu, akisema: "Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu aishiye." Mara tu Roho Mtakatifu alipokuwa amempa nuru, wakati huo alipata ujuzi fulani na moyo wake ulijazwa nuru. Hata kama wakati huo hakuwa na ufahamu wa kina, lakini alitafuta kumfahamu Mungu, na akatembea kwenye njia sahihi ya kumhudumia Mungu. Kumhudumia Mungu ni jambo la hatari zaidi, na pia ni jambo la utukufu zaidi. Kwa sababu wanadamu ni wakaidi na wapotovu, mara tu wanapopotea, wao humalizika. Watu humhudumia Mungu, sio watu wengine; kumhudumia Mungu ni jambo la hatari. Petro alitembea katika njia hiyo na alikuwa na imani hii. Na je, kuhusu Paulo? Hakukubali kwamba Yesu alikuwa Kristo. Alimuwinda bila kukoma na, baada ya kuangushwa chini, bado Paulo hakutambua kwamba Mungu alikuwa Bwana wa vitu vyote, wala vile wanadamu wanapaswa kumtii Yeye. Hakuwa na akili ya kawaida ya kufikiria, lakini kuanzia mwanzo hadi mwisho alihodhi fikira za kiburi: "Ninakupa Wewe kiasi hiki kwa hivyo unapaswa kunipa kiasi hicho; ninatumia rasilimali kiashi hiki, kwa hivyo Wewe unapaswa kunituza kiasi hicho na kunipa kiasi hicho cha mshahara." Kazi yake ilikuwa chini ya utawala wa fikira za aina hii wakati huo wote. Hivyo hakuwahi kuwa na moyo wa kumheshimu Mungu, hakuwahi kuwa na moyo wa kumcha Mungu. Angalia toni ya maneno yake: "Nimepigana vita"—Nimepigana vita Ulivyonifanya nipigane; "Nimemaliza kazi yangu"—Nimekimbia kwenye njia uliyoniambia nikimbie; "Nimeidumisha imani"—je, hukunifanya niidumishe?" Nimeidumisha, kwa hivyo taji ya utukufu haipaswi kuhifadhiwa kwa ajili yangu? Je, hakunena na toni ya aina hii? Bila shaka hangeweza kuzungumza waziwazi namna hii katika waraka. Alizungumza kitasifida na kimafumbo, lakini maneno yake yalianza kutoka kwa dhana hizi. Ni nini kilifanyika mwishowe? Yeye bado aliadhibiwa, au sivyo? Mnatakiwa kuona dhahiri vile wanadamu wanapaswa kuchagua kwenye njia ya kumhudumia Mungu, kwenye njia ya kuamini katika Mungu. Ni njia zipi za kumhudumia Mungu ni za njia za Paulo? Ni njia zipi za kuamini ni za njia ya Paulo? Ni jinsi gani njia ya kumcha Mungu ya kumhudumia Mungu kama ya Petro inawez
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni