Tamko la Kumi na Nne | Kanisa la Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Katika enzi zote, hakuna mwanadamu ameingia katika ufalme na hivyo hakuna aliyefurahia neema ya Enzi ya Ufalme, hakuna aliyeona Mfalme wa ufalme. Ingawa chini ya nuru ya Roho Wangu watu wengi wametabiri uzuri wa ufalme, wanajua tu nje ya ufalme, sio umuhimu wa ndani. Leo, ufalme ujapo kuwepo rasmi duniani, ubinadamu wote bado hujui kinachopaswa kukamilishwa, ulimwengu ambao binadamu hatimaye ataletwa ndani, wakati wa Enzi ya Ufalme.
Kuhusu haya, Naogopa watu wote wako katika hali ya mkanganyiko. Kwa sababu siku ya utambuzi kamili wa ufalme bado haijafika kabisa, wanadamu wote wamechanganyikiwa, hawawezi kuiona vizuri. Kazi Yangu ya uungu inaanza rasmi na Enzi ya Ufalme. Ni katika mwanzo rasmi wa Enzi ya Ufalme kwamba tabia Yangu inaanza kuendelea kudhihirika kwa mwanadamu. Hivyo kwa muda huu tarumbeta takatifu inaanza rasmi kutoa sauti na kutangaza kwa wote. Nichukuapo kirasmi mamlaka Yangu na kutawala kama Mfalme katika ufalme, watu Wangu wote watakamilishwa na Mimi baada ya muda. Wakati mataifa yote ya dunia yatavurugwa, hapo ndipo hasa ufalme Wangu utaanzishwa na kupata umbo na pia Nitabadilika na kurejea kwa ulimwengu mzima. Wakati huo, watu wote watauona uso Wangu tukufu, watauona uso Wangu wa kweli. Tangu kuumbwa kwa dunia hadi sasa, ubinadamu umepotoshwa na Shetani hadi kiasi kilicho leo. Kwa ufisadi wa mwanadamu, Nimefichwa zaidi na zaidi kutoka kwake na Nikazidi kutoeleweka na wao. Mwanadamu hajawahi kuuona uso Wangu wa kweli, hajawahi kuathiriana na Mimi moja kwa moja. Ni kwa tetesi na hadithi tu ndipo kumekuwa na “Mimi” kwa ubunifu wa mwanadamu. Kwa hivyo Nakubaliana na ubunifu wa binadamu, kwamba, ni dhana za binadamu, kukabiliana na “Mimi” kwa akili za wanadamu, kwamba Naweza kubadilisha hali ya “Mimi” ambayo wameweka kwa miaka mingi. Hii ni kanuni ya kazi Yangu. Hakuna mtu hata mmoja ameweza kuijua vizuri sana. Ingawa wanadamu wamejilaza na kuja mbele Yangu kuniabudu, Sifurahii matendo kama haya ya wanadamu kwa sababu kwa mioyo yao hawajashikilia mfano Wangu, lakini mfano Wangu wa nje. Kwa hivyo, akili zao zinapokosa tabia Yangu, hawajui chochote kuhusu uso Wangu wa kweli. Kwa hivyo, wakati wameamini wamenipinga ama kukosea amri Zangu za kitawala, Nafunga macho. Na hivyo, kwa kumbukumbu zao, Nimi ni Mungu anayeonyesha huruma kwa wanadamu badala ya kuwaadibu, ama Mimi ni Mungu Mwenyewe asiyemaanisha Anachokisema. Haya yote ni mawazo yanayotokana na fikira za wanadamu na sio kwa mujibu na ukweli.
Nasimama juu ya ulimwengu wote siku baada ya siku, nikichunguza, na kujificha Mimi Mwenyewe kwa unyenyekevu katika nyumba Yangu kupata uzoefu wa maisha ya binadamu, Nikichunguza kwa karibu matendo yote ya mwanadamu. Hakuna aliyewahi kujitolea Kwangu kwa kweli. Hakuna aliyewahi kufuata ukweli. Hakuna aliyewahi kuwa mwangalifu Kwangu. Hakuna aliyewahi kufanya maazimio mbele Yangu na kufanya wajibu wake. Hakuna aliyewahi kuniruhusu kuishi ndani yake. Hakuna aliyewahi kunithamini kama afanyavyo maisha yake. Hakuna aliyewahi kuona kwa vitendo vya ukweli uzima wote wa uungu Wangu. Hakuna aliyewahi kutamani kuwasiliana na Mungu wa vitendo Mwenyewe. Wakati maji yanameza wanadamu, Nawaokoa kutokana na maji yaliyotuama na kuwapa nafasi ya kuishi upya. Wanadamu wanapopoteza imani yao ya kuishi, Nawavuta juu kutoka ukingo wa kifo, na kuwapa ujasiri wa kuishi, ili kwamba wananichukua kama msingi wa kuwepo kwao. Wanadamu wanaponiasi, Nawafanya Kunijua kwa kuasi kwao. Kutokana na asili ya zamani ya ubinadamu na kutokana na huruma Yangu, badala ya kuwaua binadamu, Nawaruhusu kutubu na kuanza upya. Wakati wanadamu wanateseka na kiangazi, Nawatoa kifoni kama bado wamesalia na pumzi moja, kuwazuia kudanganywa na Shetani. Watu wameona mikono Yangu mara ngapi; watu wameona uso Wangu karimu mara ngapi, kuuona uso Wangu wa tabasamu; na wameona adhama Yangu mara ngapi, kuona ghadhabu Yangu. Ingawa ubinadamu haujawahi kunijua, Siwakamati juu ya udhaifu wao kufanya matata yasiyohitajika. Kupitia ugumu wa ubinadamu, Nina huruma na udhaifu wake. Ni kwa sababu ya kuasi kwa wanadamu, kutokuwa na shukrani kwao, ndiko Nawaadibu kwa viwango tofauti.
Najificha wakati wanadamu wana kazi nyingi na kujifichua wakati wao wa burudani. Ubinadamu unanidhania kuwa Anayejua yote na kuwa Mungu Mwenyewe anayekubali maombi yote. Wote basi wanakuja mbele Yangu kutafuta tu msaada wa Mungu, bila kuwa na tamaa ya kunijua. Wakiwa katika maumivu ya magonjwa, wanadamu wananiomba msaada. Wakiwa na shida, wananiambia matatizo yao kwa nguvu zao zote ili kumwaga mateso yao. Na bado hakuna mwanadamu hata mmoja ameweza kunipenda pia akiwa na faraja. Hakuna mtu hata mmoja amenitafuta wakati wa amani na furaha ili Nishiriki furaha yake. Wakati familia yao ya karibu ina furaha na iko sawa, wanadamu tayari wananiweka kando ama kunifungia mlango, kunikataza kuingia, na hivyo kufurahia furaha heri ya familia. Akili ya binadamu ni nyembamba sana, nyembamba sana hata kumshikilia Mungu, apendaye, mwenye huruma, na anayegusika kama Mimi. Nimekataliwa mara ngapi na wanadamu wakati wao wa kicheko na furaha, Nimetegemewa kama gongo mara ngapi na wanadamu wakati wanaanguka; Ni mara ngapi Nimelazimishwa kuwa daktari wa wanadamu wanaougua magonjwa. Mwanadamu ni katili jinsi gani! Hawana akili na ni wabaya kabisa. Hawana hata hisia zinazopatikana kwa binadamu. Hawana ubinadamu hata kidogo. Fikiria siku za nyuma na linganisha na sasa. Kuna mabadiliko yanayofanyika ndani zenu? Kuna siku kidogo za zamani sasa? Ama zamani bado haijabadilishwa?
Juu ya mlima na chini ya bonde Nimepitia, na kuwa na uzoefu wa panda shuka za dunia. Nimetembea na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi, lakini bado inaonekana tabia ya mwanadamu imebadilika kidogo. Na ni kama asili ya zamani ya mwanadamu imeeneza mizizi na kuota ndani yao. Hawawezi kamwe kubadili hiyo asili ya zamani, kuiboresha tu kwa msingi wa kwanza. Wasemavyo wanadamu, kiini hakijabadilika, lakini umbo limebadilika sana. Kila mtu, inaonekana, anajaribu kunidanganya, kunipofusha, ili aweze kuingia na kupata shukrani Yangu. Sipendi wala kutia maanani udanganyifu wa watu. Badala ya kukasirika, Nachukua mtazamo wa kuangalia lakini si kuona. Napanga kuupa ubinadamu kiwango fulani cha uhuru, na hivyo, kushughulikia wanadamu wote kama kitu kimoja. Kwa sababu wanadamu wote hawajiheshimu na ni maskini wasio na faida, wasiojithamini, watawezaje kunihitaji kuonyesha huruma na mapenzi mapya? Wanadamu wote hawajijui, na hawajui uzito wao. Wanapaswa kujipima uzito. Ubinadamu haunitambui, hivyo Nami pia siutilii maanani. Wanadamu hawanitambui, kwa hivyo Mimi pia Siweki juhudi kwao. Je, hii ni bora? Je, hii haiwazungumzii, watu Wangu? Nani amefanya maazimio mbele Yangu na kukosa kuyatupilia mbali baadaye? Nani amefanya maazimio ya muda mrefu mbele Yangu badala ya kutatua mara nyingi juu ya hii na hiyo? Daima, wanadamu hufanya maazimio mbele Yangu wakati wa raha na kuyafuta kabisa wakati wa shida. Baadaye, wanachukua uamuzi wao na kuuweka mbele Yangu. Je, Mimi si wa kuheshimika hadi Naweza kubali kwa kawaida taka iliyookotwa na mwanadamu kutoka pipani? Wanadamu wachache hushikilia maazimio yao, wachache ni safi, na wachache wanatoa yenye thamani kubwa zaidi kama sadaka Kwangu. Je, nyinyi wote si sawa kwa njia hii? Iwapo, kama mmoja wa watu Wangu kwenye ufalme, huwezi kufanya wajibu wako, utachukiwa na kukataliwa na Mimi!
Machi 12, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni