Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V(2)Sehemu ya Pili |
Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu alisema,Kiini cha Shetani ni ovu, kwa hivyo matokeo ya vitendo vya Shetani bila shaka ni ovu, ama kwa kiwango cha chini kabisa, yanahusiana na uovu wake, tunaweza kusema hayo? (Ndiyo.) Kwa hivyo, je Shetani anampotosha mwanadamu vipi?
Kwanza lazima tuangalie hasa—uovu uliofanywa na Shetani duniani na miongoni mwa ubinadamu ambao unaonekana, tunaoweza kuhisi; mmewahi kuyafikiria haya awali? Pengine hamkuyafikiria sana, kwa hivyo wacha Nitaje pointi kadhaa muhimu ili muweze kuona jinsi Shetani anampotosha mwanadamu. Kuna nadharia inayoitwa mageuko; kila mtu anajua kuihusu, siyo? Mageuko na uyakinifu huu, si sehemu ya maarifa yanayosomwa na mwanadamu? (Ndiyo.) Hivyo, Shetani kwanza anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu, na kisha anatumia sayansi kuamsha mvuto wa wanadamu kwa maarifa, sayansi, na vitu vya ajabu, ama kwa vitu ambavyo watu wanataka kuchunguza; hii ni kusema, Shetani anatumia maarifa ya kisayansi kumpotosha mwanadamu. Vitu vifuatavyo vinavyotumiwa na Shetani kumpotosha mwanadamu ni desturi ya kitamaduni na ushirikina, na baada ya vitu hivyo, anatumia mienendo ya kijamii. Hivi vyote ni vitu ambavyo watu wanapatana navyo katika maisha yao ya kila siku na hivi vyote vinahusiana na vitu vilivyo karibu na watu, vitu wanavyoona, wanavyosikia, wanavyogusa na wanavyopitia. Mtu anaweza kusema kwamba vinazunguka kila mtu, haviwezi kutorokwa na kuepukika. Wanadamu hawana njia ya kuepuka kuathiriwa, kuambukizwa, kudhibitiwa, na kufungwa na vitu hivi; hawana nguvu za kuvisukuma mbali.
Kwanza lazima tuangalie hasa—uovu uliofanywa na Shetani duniani na miongoni mwa ubinadamu ambao unaonekana, tunaoweza kuhisi; mmewahi kuyafikiria haya awali? Pengine hamkuyafikiria sana, kwa hivyo wacha Nitaje pointi kadhaa muhimu ili muweze kuona jinsi Shetani anampotosha mwanadamu. Kuna nadharia inayoitwa mageuko; kila mtu anajua kuihusu, siyo? Mageuko na uyakinifu huu, si sehemu ya maarifa yanayosomwa na mwanadamu? (Ndiyo.) Hivyo, Shetani kwanza anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu, na kisha anatumia sayansi kuamsha mvuto wa wanadamu kwa maarifa, sayansi, na vitu vya ajabu, ama kwa vitu ambavyo watu wanataka kuchunguza; hii ni kusema, Shetani anatumia maarifa ya kisayansi kumpotosha mwanadamu. Vitu vifuatavyo vinavyotumiwa na Shetani kumpotosha mwanadamu ni desturi ya kitamaduni na ushirikina, na baada ya vitu hivyo, anatumia mienendo ya kijamii. Hivi vyote ni vitu ambavyo watu wanapatana navyo katika maisha yao ya kila siku na hivi vyote vinahusiana na vitu vilivyo karibu na watu, vitu wanavyoona, wanavyosikia, wanavyogusa na wanavyopitia. Mtu anaweza kusema kwamba vinazunguka kila mtu, haviwezi kutorokwa na kuepukika. Wanadamu hawana njia ya kuepuka kuathiriwa, kuambukizwa, kudhibitiwa, na kufungwa na vitu hivi; hawana nguvu za kuvisukuma mbali.
Kwanza tutazungumza kuhusu maarifa. Si kila mtu angechukulia maarifa kuwa kitu chema? Ama kwa kiwango cha chini kabisa, watu wanafikiri kwamba kidokezo cha neno “maarifa” ni chema badala ya hasi. Kwa hivyo mbona tunataja hapa kwamba Shetani anatumia maarifa kwanza kumpotosha mwanadamu? Si nadharia ya mageuko ni kipengele cha maarifa? Si sheria za kisayansi za Newton ni sehemu ya maarifa? Si mvuto wa dunia ni sehemu ya maarifa, siyo? (Ndiyo.) Hivyo mbona maarifa yametajwa miongoni mwa maudhui anayoyatumia Shetani kumpotosha mwanadamu? Maoni yenu hapa ni yapi? Je, maarifa yana hata chembe cha ukweli ndani yake? (La.) Kwa hivyo ni nini kiini cha maarifa? (Yanaenda kinyume na ukweli.) Maarifa ambayo mwanadamu anatafiti yanafunzwa kwa msingi upi? Yanalingana na nadharia ya mageuko? Si maarifa ambayo mwanadamu amechunguza, ujumla wake, unatokana na ukanaji Mungu? (Ndiyo.) Hivyo, kuna sehemu yoyote ya maarifa haya ambayo ina uhusiano na Mungu? Je, yanahusiana na kumwabudu Mungu? Yanahusiana na ukweli? (La.) Shetani anatumiaje maarifa kumpotosha mwanadamu? Nimetoka tu kusema kwamba hakuna sehemu yoyote ya maarifa haya inahusiana na kumwabudu Mungu ama na ukweli. Watu wengine wanayafikiria hivi: “Yanaweza kutokuwa na chochote kuhusiana na ukweli, lakini hayawapotoshi watu.” Mnafikiri nini kuhusu haya? Ulifundishwa na maarifa kwamba furaha ya watu ilitegemea kile walichokiumba na mikono yao? Je, maarifa yaliwahi kukufunza kwamba hatima ya mwanadamu ilikuwa mikononi mwake? (Ndiyo.) Haya ni mazungumzo ya aina gani? (Ni upuuzi.) Sahihi! Ni upuuzi! Maarifa yanatatiza kujadili. Unaweza kuiweka kwa urahisi kwamba eneo la maarifa ni maarifa tu. Hili ni eneo la maarifa linalofunzwa kwa msingi wa ukanaji Mungu na kutokuwa na uelewa kwamba Mungu aliumba mambo yote. Watu wanaposoma aina hii ya maarifa, hawaoni Mungu anatawala mambo yote, hawaoni Mungu anaongoza ama anasimamia mambo yote. Badala yake, wanayofanya tu ni kutafiti, kuchunguza, na kutafuta majibu ya kisayansi bila kikomo kwa sehemu hiyo ya maarifa. Hata hivyo, iwapo watu hawamwamini Mungu na badala yake wanatafiti tu, kamwe hawatapata majibu ya kweli, siyo? Maarifa yanakupa tu riziki, yanakupa tu kazi, yanakupa tu mapato ili usiwe na njaa, lakini kamwe hayawezi kukusaidia kumjua Mungu, hayatakusaidia kumwamini Yeye, kumtii Yeye, na maarifa kamwe hayatakuweka mbali na maovu. Kadiri unavyosoma maarifa, ndivyo utatamani zaidi kuasi dhidi ya Mungu, kumtafiti Mungu, kumjaribu Mungu, na kwenda kinyume na Mungu. Hivyo sasa, tunaona yapi ambayo maarifa yanawafunza watu? Yote ni filosofia ya Shetani. Je, filosofia za Shetani na kanuni za kuishi zinazopatikana kwa wanadamu potovu zina uhusiano wowote na ukweli? (La.) Hazina uhusiano wowote na ukweli na, kwa kweli, ni kinyume cha ukweli. Watu mara nyingi husema, “Maisha ni mwendo”; haya ni mazungumzo ya aina gani? (Upuuzi.) Watu pia wanasema, “Mwanadamu ni chuma, mchele ni chuma, mwanadamu huhisi anataabika kwa njaa asipokula mlo”; hii ni nini? (Upuuzi, maneno ya Shetani.) Hata ni uwongo mbaya zaidi na inachukiza kuisikia. Hivyo, maarifa ni kitu ambacho pengine kila mtu anakijua. Kwa yanayoitwa maarifa ya mwanadamu, Shetani amejaza kidogo filosofia yake ya maisha na kufikiria kwake. Na wakati Shetani anafanya haya, Shetani anamruhusu mwanadamu kuomba kufikiria kwake, filosofia, na mtazamo wake ili mwanadamu aweze kukana uwepo wa Mungu, kukana utawala wa Mungu juu ya mambo yote na utawala juu ya hatima ya mwanadamu. Kwa hivyo, masomo ya mwanadamu yanapoendelea, anahisi uwepo wa Mungu kuwa usio yakini anapopata maarifa zaidi, na mwanadamu anaweza hata kuhisi kwamba Mungu hayupo kwa sababu ya mitazamo, dhana, na fikira ambazo Shetani ameongeza kwa akili ya mwanadamu. Shetani anapoweka fikira hizi ndani ya akili ya mwanadamu, si watu wanapotoshwa na mambo haya? (Ndiyo.) Ni nini msingi wa maisha ya mwanadamu sasa? Kweli anategemea maarifa haya? La; msingi wa maisha ya mwanadamu ni fikira, mitazamo na filosofia za Shetani ambazo zimefichwa kwa maarifa haya. Hapa ndipo kiini cha upotovu wa Shetani wa mwanadamu unafanyika, hili ndilo lengo la Shetani na mbinu yake ya kumpotosha mwanadamu.
A. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Maarifa Kumpotosha Mwanadamu
Kwanza tutazungumzia kipengele cha juujuu zaidi cha mada hii. Mlipokuwa mnafunzwa Kiswahili shuleni, je, lugha na maandishi yaliweza kuwapotosha watu? Hayangeweza. Maneno yanaweza kupotosha watu? (La.) Maneno hayapotoshi watu; ni chombo kinachowaruhusu watu kuongea na chombo ambacho watu wanatumia kuwasiliana na Mungu. Zaidi, lugha na maneno ni jinsi ambavyo Mungu anawasiliana na watu sasa, ni vyombo, ni vya umuhimu. Moja ongeza moja ni mbili, haya ni maarifa, siyo? Mbili zidisha kwa mbili ni nne, haya ni maarifa, siyo? Lakini yanaweza kukupotosha? Hii ni akili ya wote na kanuni kwa hivyo haiwezi kupotosha watu. Kwa hivyo ni maarifa gani yanayopotosha watu? Ni maarifa ambayo yamechanganywa mitazamo na fikira za Shetani, Shetani anataka kujaza mitazamo na fikira hizi ndani ya ubinadamu kupitia maarifa. Kwa mfano, katika insha, kuna chochote kibaya na maneno yaliyoandikwa? (La.) Hivyo, shida inaweza kuwa wapi? Mitazamo na nia ya mwandishi alipoandika insha hiyo na pia maudhui ya fikira zake—haya ni mambo ya kiroho—yanaweza kuwapotosha watu. Kwa mfano, iwapo ungekuwa ukitazama kipindi kwa runinga, ni mambo yapi ndani yake yangeweza kubadili mtazamo wako? Je, yale yaliyosemwa na wasanii, maneno yenyewe, yangeweza kuwapotosha watu? (La.) Ni mambo yapi ambayo yangeweza kuwapotosha watu? Ingekuwa fikira na maudhui ya kiini ya kipindi, ambayo yangewakilisha mitazamo ya mwelekezi, na taarifa iliyo kwa mitazamo hii ingeshawishi mioyo na akili za watu. Siyo? (Ndiyo.) Je, mnajua Narejelea nini katika mjadala Wangu wa Shetani kutumia maarifa kuwapotosha watu? (Ndiyo, tunajua.) Hutafahamu vibaya, siyo? Hivyo unaposoma riwaya ama insha tena, unaweza kutathmini iwapo fikira zilizoelezwa katika insha hiyo zinapotosha ama hazipotoshi mwanadamu ama kuchangia kwa ubinadamu? (Tunaweza kufanya hivyo kidogo.) Hiki ni kitu ambacho lazima kisomwe na kupitiwa polepole, si kitu kinachoeleweka kwa urahisi mara moja. Kwa mfano, unapotafiti ama kusoma sehemu ya maarifa, baadhi ya vipengele vyema vya maarifa hayo vinaweza kukusaidia kuelewa baadhi ya akili ya wote kuhusu eneo hilo, na kile ambacho watu wanapaswa kuepukana nacho. Chukua mfano wa “umeme,” hili ni eneo la maarifa, siyo? Ungekuwa mjinga kama hungejua kwamba umeme unaweza kuwatetemesha watu, siyo? Lakini utakapoelewa sehemu hii ya maarifa, hutakuwa na uzembe kuhusu kugusa kitu cha umeme na utajua jinsi ya kutumia umeme. Haya yote ni mambo mema. Unaelewa kile tunachojadili kuhusu jinsi maarifa yanawapotosha watu? (Ndiyo, tunaelewa.) Iwapo unaelewa hatutaendelea kukizungumzia zaidi kwa sababu kuna aina nyingi za maarifa ambazo zinasomwa duniani na lazima mchukue wakati wenu kuzitofautisha wenyewe.
B. Jinsi ambavyo Shetani Anatumia Sayansi Kupotosha Mwanadamu
Sayansi ni nini? Si sayansi imewekwa kwa hadhi ya juu na kuchukuliwa kuwa muhimu katika akili za karibu kila mtu? (Ndiyo, imewekwa kwa hadhi ya juu.) Sayansi inapotajwa, si watu wanahisi, “Hiki ni kitu ambacho watu wa kawaida hawawezi kuelewa, hii ni mada ambayo tu watafiti wa kisayansi ama wataalam wanaweza kugusia. Haina uhusiano wowote na sisi watu wa kawaida”? Je, ina uhusiano lakini? (Ndiyo.) Shetani anatumiaje sayansi kuwapotosha watu? Hatutazungumza kuhusu mambo mengine isipokuwa mambo ambayo watu mara nyingi wanapatana nayo katika maisha yao binafsi. Umesikia kuhusu “jeni,” siyo? (Ndiyo.) Nyote mnalijua neno hili, siyo? Je, jeni ziligunduliwa kupitia sayansi? Jeni zinamaanisha nini hasa kwa watu? Hazifanyi watu kuhisi kwamba mwili ni kitu cha ajabu? Wakati watu wanajulishwa kwa mada hii, si kutakuwa na watu—hasa wenye kutaka kujua—ambao watataka kujua zaidi ama kutaka maelezo zaidi? Hawa watu wanaotaka kujua wataweka nguvu zao zote kwa mada hii na wakati hawana shughuli watatafuta maelezo kwa vitabu na intaneti kujifunza maelezo zaidi kuihusu. Sayansi ni nini? Kuongea waziwazi, sayansi ni fikira na nadharia ya vitu ambavyo mwanadamu anataka kujua, vitu visivyojulikana, na ambavyo hawajaambiwa na Mungu; sayansi ni fikira na nadharia za siri ambazo mwanadamu anataka kuchunguza. Unafikiria wigo wa sayansi ni upi? Unaweza kusema kwamba unajumuisha mambo yote, lakini mwanadamu anafanya vipi kazi ya sayansi? Je, ni kupitia utafiti? Inahusiana na kutafiti maelezo na sheria za vitu hivi na kuweka mbele nadharia zisizoaminika ambazo watu wote wanafikiria, “Wanasayansi hawa ni wakubwa mno! Wanajua mengi na wana maarifa mengi kuelewa mambo haya!” Wanapendezwa sana na watu hao, siyo? Watu wanaotafiti sayansi, wana mitazamo ya aina gani? Hawataki kutafiti ulimwengu, kutafiti mambo ya ajabu ya maeneo ya maslahi yao? Matokeo ya mwisho ya haya ni nini? Baadhi ya sayansi ina watu wanaofikia mahitimisho yao kwa kubahatisha, nyingine ina watu wanaotegemea uzoefu wa binadamu kwa mahitimisho yao na hata eneo lingine la sayansi litakuwa na watu wanaofikia mahitimisho yao kutokana na uzoefu ama uchunguzi wa kihistoria na usuli. Sivyo? (Ndiyo.) Hivyo, sayansi inawafanyia nini watu? Kile sayansi inafanya ni kwamba inawaruhusu tu watu kuona vyombo katika ulimwengu wa maumbile na tu kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu; haimruhusu mwanadamu kuona sheria ambazo Mungu anatumia kutawala mambo yote. Mwanadamu anaonekana kupata majibu kutoka kwa sayansi, lakini majibu hayo yanachanganya na yanaleta tu uradhi wa muda mfupi, uradhi ambao unawekea moyo wa mwanadamu mipaka kwa ulimwengu wa maumbile. Mwanadamu anahisi kwamba tayari amepata majibu kutoka kwa sayansi kwa hivyo licha ya suala litakaloibuka, anaamini kwa dhati mitazamo yao ya kisayansi kulithibitisha ama kulikubali. Moyo wa mwanadamu unamilikiwa na sayansi na kushawishiwa nayo hadi pahali ambapo mwanadamu tena hana akili ya kumjua Mungu, kumwabudu Mungu, na kuamini kwamba mambo yote yanatoka kwa Mungu na mwanadamu anapaswa kumwangalia kupata majibu. Hii si ukweli? Unaweza kuona kwamba kadiri ambavyo mtu anaamini sayansi, anakuwa mjinga zaidi, akiamini kwamba kila kitu kina suluhisho la sayansi, kwamba utafiti unaweza kutatua chochote. Hamtafuti Mungu na haamini kwamba Yupo; hata watu wengine ambao wamemfuata Mungu kwa miaka mingi wataenda na kutafiti vimelea kwa msukumo ama kutafuta baadhi ya maelezo ili kupata majibu. Mtu kama huyo haangalii masuala kwa mtazamo wa ukweli na wakati mwingi anataka kutegemea mitazamo na maarifa ya kisayansi ama majibu ya kisayansi kutatua shida; lakini hamtegemei Mungu na hamtafuti Mungu. Je, watu kama hao wana Mungu katika mioyo yao? (La.) Hata kuna watu wengine wanaotaka kutafiti Mungu kwa njia sawa na vile wanasoma sayansi. Kwa mfano, kuna wataalam wengi wa kidini walioenda mahali safina ilisimama baada ya mafuriko makubwa. Wameiona safina, lakini katika kuonekana kwa safina hawaoni uwepo wa Mungu. Wanaamini tu hadithi na historia na haya ni matokeo ya utafiti wao wa kisayansi na utafiti wa dunia ya maumbile. Ukitafiti vitu yakinifu, viwe mikrobiolojia, falaki, ama jiografia, hutawahi kupata matokeo yanayosema kwamba Mungu yupo ama kwamba anatawala mambo yote, Sivyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo sayansi inamfanyia nini mwanadamu? Si inamweka mbali na Mungu? Si hii inawaruhusu watu kumtafiti Mungu? Si hii inawafanya watu kuwa na shaka zaidi kuhusu uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo Shetani anataka kutumia vipi sayansi kumpotosha mwanadamu? Si Shetani anataka kutumia mahitimisho ya kisayansi kuwadanganya na kuwanyima watu hisia? Shetani anatumia majibu yenye maana nyingi kushikilia mioyo ya watu ili wasitafute ama kuamini uwepo wa Mungu, na hivyo watakuwa wenye tuhuma kwa Mungu, kumkanusha Mungu na kuwa mbali na Yeye. Hivyo, hii ndiyo sababu tunasema ni njia moja Shetani anawapotosha watu.
C. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu
Je, kuna mambo mengi yanayochukuliwa kuwa sehemu ya desturi ya kitamaduni? (Ndiyo.) Hii desturi ya kitamaduni inamaanisha nini? (Inapitishwa kutoka kwa mababu.) Inapitishwa kutoka kwa mababu, hiki ni kipengele kimoja. Familia, vikundi vya makabila, na hata jamii ya binadamu imepitisha njia yao ya maisha kutoka mwanzo, ama imepitisha mila, misemo, na kanuni, ambazo zimeingizwa kwa fikira za watu. Watu wanafikiria nini kuhusu mambo haya? Watu wanayachukulia kuwa yasiyoweza kutengwa na maisha yao. Wanayachukua mambo haya na kuyachukulia kuwa kanuni na uhai wa kutii, na daima hawako tayari kuyabadilisha ama kuyaacha mambo haya kwa sababu yalipitishwa kutoka kwa mababu. Kuna vipengele vingine vya desturi ya kitamaduni, kama kile kilichopitishwa na Confucius ama Mencius, ama mambo waliyofunzwa watu na Udao ama Uconfucius ambayo yamekuwa sehemu ya kila mtu hadi ndani kwa mifupa yao. Sivyo? (Ndiyo.) Desturi ya kitamaduni hii inajumuisha nini? Inajumuisha likizo ambazo watu wanasherehekea? Kwa mfano, hapo juu kuna Tamasha la Majira ya machipuko, Tamasha la Taa, Siku ya Kufagia Kaburi, Tamasha la Mashua ya Joka, na kuna Siku ya Kimataifa ya Leba, Siku ya Watoto, Tamasha ya Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani, na Siku ya Kitaifa. Baadhi za familia hata husherehekea likizo zingine, ama husherehekea wakati wazee wanahitimu umri fulani, ama wakati watoto wanahitimu umri wa mwezi 1 na wakati wako na umri wa siku 100. Hizi zote ni likizo za desturi. Je, si usuli wa likizo hizi unajumuisha desturi ya kitamaduni? Ni nini kiini cha desturi ya kitamaduni? Kina chochote kuhusu kumwabudu Mungu? Kina chochote kuhusu kuwaambia watu kuweka katika vitendo ukweli? (La.) Kuna likizo zozote za watu kutoa sadaka kwa Mungu, kwenda kwa madhabahu ya Mungu na kupokea neno Lake? Kuna likizo kama hizi? (La.) Watu hufanya nini katika likizo hizi zote? (Kumwabudu Shetani. Kula, kunywa na shughuli za burudani.) Katika nyakati za sasa zinaonekana kuwa hafla za kula, kunywa, na kujiburudisha. Basi ni nini chanzo cha desturi ya kitamaduni? Desturi ya kitamaduni imetoka kwa nani? (Shetani.) Imetoka kwa Shetani. Katika usuli wa hizi likizo za desturi, Shetani anaingiza mambo ndani ya mwanadamu, haya ni mambo gani? Kuhakikisha kwamba watu wanakumbuka mababu zao, hili ni mojawapo ya mambo haya? Kwa mfano, wakati wa Tamasha la Kufagia Kaburi watu husafisha makaburi na kutoa sadaka kwa mababu zao. Hivyo watu hawatasahau mababu zao, siyo? Pia, Shetani anahakikisha kwamba watu wanakumbuka kuwa wazalendo, kama katika Tamasha la Mashua ya Joka. Je, Tamasha la Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani? (Kupatana kwa familia.) Ni nini usuli wa kupatana kwa familia? Sababu zake ni nini? (Kuweka familia kwanza, na hisia.) Kuwasiliana na kuunganika kihisia, siyo? Bila shaka, iwapo ni kusherehekea Mkesha wa Mwaka Mpya wa Mwezi ama Tamasha la Taa, kuna njia nyingi za kuelezea sababu za usuli. Haijalishi mtu anaelezea sababu iliyo nyuma yazo, kila moja ni njia ya Shetani ya kuingiza filosofia yake na kufikiria kwake kwa watu, ili waweze kupotea kutoka kwa Mungu na wasijue kwamba kuna Mungu, na kwamba watoe sadaka ama kwa mababu zao au Shetani, ama kwamba ni udhuru wa kula, kunywa na kujifurahisha kwa ajili ya matamanio ya mwili. Kila ya likizo hizi inaposherehekewa, fikira na mitazamo ya Shetani yanapandwa kwa kina ndani ya akili za watu na hata hawajui. Wakati watu wanafika umri wa kati ama zaidi, mambo haya, fikira na mitazamo hii ya Shetani tayari yamekita mizizi ndani sana ya mioyo yao. Zaidi, watu wanafanya juhudi zao kabisa kueneza fikira hizi, ziwe sahihi ama si sahihi, kwa kizazi kifuatacho bila wasiwasi. Sivyo? (Ndiyo.) Hivyo desturi hii ya kitamaduni na likizo hizi zinapotosha vipi watu? (Watu wanawekewa mipaka na kufungwa na kanuni za hizi desturi kana kwamba hawana muda ama nguvu kumtafuta Mungu.) Hiki ni kipengele kimoja. Kwa mfano, kila mtu anasherehekea wakati wa Mwaka Mpya wa Mwezi, usingesherehekea, hungehisi huzuni? Hungehisi, “Haiya, sikusherehekea Mwaka Mpya. Siku hii ya Mwaka Mpya wa Mwezi ilikuwa mbaya sana, na haijasherehekewa; mwaka huu wote utakuwa mbaya”? Si ungehisi kutokuwa na utulivu? (Ndiyo.) Na pengine kuogopa kiasi, siyo? Kuna hata watu wengine ambao hawajatoa sadaka kwa mababu zao kwa miaka mingi na ghafla wamekuwa na ndoto ambapo mtu aliyekufa anawaomba pesa, watahisi nini ndani yao? “Inahuzunisha kwamba huyu mtu aliyekufa anahitaji pesa ya kutumia! Nitawachomea baadhi ya pesa ya karatasi, nisipo hiyo hakika haitakuwa sawa. Sisi tunaoishi tunaweza kupatana na shida kidogo nisipochoma baadhi ya pesa ya karatasi, ni nani anayeweza kusema wakati janga litatokea?” Daima watakuwa na wingu hili ndogo la hofu na wasiwasi katika mioyo yao. Hivyo ni nani anayewapa wasiwasi? (Shetani.) Shetani huleta wasiwasi. Si hii ndiyo njia moja ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? Anatumia mbinu na udhuru mbalimbali ili kukudhibiti, kukutishia, kukufunga, hadi kiasi kwamba unachanganyikiwa na kumkubali na kumnyenyekea; hivi ndivyo Shetani anampotosha mwanadamu. Nyakati nyingi ambapo watu ni wanyonge ama hawaelewi vyema hali ilivyo, wanaweza bila kutaka, kufanya kitu kwa njia iliyochanganyikiwa, yaani, wanaanguka chini ya mshiko wa Shetani bila kusudi na wanaweza kufanya kitu bila kusudi na wasijue wanafanya nini. Hii ni njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu. Hata kuna watu wachache sasa ambao wanasita kuachana na desturi za kitamaduni ambazo zimekita mizizi na hawawezi tu kuziacha. Ni hasa wakati ni wanyonge na wasipoonyesha hisia ndipo wanataka kusherehekea likizo za aina hizi na wanataka kukutana na Shetani na kumridhisha Shetani tena, ambako kupitia huko wanaweza pia kujifariji ndani yao. Si mambo yanaenda hivi? (Ndiyo.) Ni nini usuli wa hizi desturi za kitamaduni? Mkono mweusi wa Shetani unavuta nyuzi nyuma ya pazia? Asili ovu ya Shetani inatawala na kudhibiti vitu? Shetani anadhibiti hivi vitu vyote? (Ndiyo.) Wakati watu wanaishi katika desturi ya kitamaduni na kusherehekea likizo za desturi za aina hizi, tunaweza kusema kwamba haya ni mazingira ambapo wanadanganywa na Shetani na kupotoshwa na Shetani? Si wana furaha kupotoshwa na Shetani? Si hivi ndivyo jinsi ilivyo? (Ndiyo.) Hiki ni kitu ambacho sisi wote tunakiri, siyo? Na kitu ambacho sote tunakijua.
D. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Ushirikina Kumpotosha Mwanadamu
Mnalijua neno “ushirikina,” siyo? Katika ushirikina, watu mara nyingi wanakutana na nini? (Miungu ya uongo) Kuna usawa unaopatana na desturi ya kitamaduni hapa, lakini hatutazungumza kuhusu huo leo, badala yake Nitajadili unaokabiliwa mara nyingi: uganga, uaguzi, kuchoma ubani, na kuabudu Buddha. Watu wengine wanafanya uganga, wengine wanaabudu Buddha na kuchoma ubani, ilhali wengine wanabashiriwa ama wanaambiwa bahati zao kwa kumruhusu mtu kusoma vipengele vya uso yao. Wangapi kati yenu wameambiwa bahati zao ama wamesomwa uso? Hiki ni kitu ambacho watu wengi wanataka, siyo? (Ndiyo.) Mbona hivyo? Watu wanapata faida ya aina gani kutoka kwa uaguzi na uganga? Wanapata uradhi wa aina gani kutoka kwa hayo? (Udadisi.) Ni udadisi tu? Haiwezi kuwa udadisi. Ni nini lengo la ubashiri? Mbona ufanyiwe? Si kwa ajili ya kuona siku za baadaye? Watu wengine wanasomwa nyuso zao ili kutabiri siku za baadaye, wengine wanafanya hivyo ili kuona iwapo watakuwa na bahati nzuri au la. Wengine wanafanya hivyo ili kuona vipi ndoa zao zitakuwa, na bado wengine wanafanya hivyo kuona bahati itakayoletwa na mwaka ulio mbele. Watu wengine wanasomwa nyuso zao kuona matarajio ya wana na binti zao yatakuwa vipi na kuona vipengele vyote vya vitu hivi, na wanabiashara wengine wanafanya hivyo kuona watatengeneza pesa ngapi ili waweze kupata mwongozo kwa kile wanachopaswa kufanya. Watu wengine wanataka tu kujua bahati yao itakuwaje na siku za baadaye zitaleta nini. Je, ni kuridhisha udadisi tu? (La.) Wakati watu wanasomwa nyuso zao ama kufanya vitu vya aina hii, ni kwa faida ya siku zao za baadaye binafsi na wanaamini kwamba haya yote yanahusiana kwa karibu na hatima zao. Je, kuna yoyote katika mambo haya yaliyo ya manufaa? (La.) Mbona si ya manufaa? Si kitu kizuri kujua kidogo kuhusu siku za badaye? Hii inakusaidia kujua wakati shida inaweza kutokea, ili uweze kuiepuka kama ulikuwa unajua kuihusu awali, siyo? Kupigiwa ramli kunaweza kukuruhusu kuongozwa kuhusiana nako, ili mwaka ulio mbele uweze kuwa mzuri na unaweza kuwa tajiri ukifanya biashara. Si hii ni ya manufaa? (La.) Iwapo ina manufaa haituhusu, hatutaishiriki leo; mjadala wetu hauhusishi maudhui na mada hii. Shetani anatumiaje ushirikina kumpotosha mwanadamu? Kile ambacho watu wanajua kuhusu vitu kama ubashiri, kusoma uso, na uaguzi ni ili waweza kujua bahati zao zitakuwa vipi katika siku za baadaye na vile njia iliyo mbele inakaa, lakini mwishowe, ni mikono ya nani inadhibiti vitu hivi? (Mikono ya Mungu.) Viko katika mikono ya Mungu. Kuhusiana na Shetani, kwa kutumia mbinu hizi, anataka watu wajue nini? Shetani anataka kutumia kusoma uso na uaguzi ili kuwaambia watu kwamba anajua bahati zao mbeleni, na Shetani anataka kuwaambia watu kwamba anajua vitu hivi na anavidhibiti. Shetani anataka kutumia fursa hii na kutumia mbinu hizi kudhibiti watu, ili kwamba watu wanamwekea imani isiyoweza kutambua na kutii kila neno lake. Kwa mfano, ukisomwa uso, mwaguzi akifunga macho yake na kukwambia kila kitu ambacho kimekufanyikia katika miongo michache iliyopita kwa uwazi kamili, ungehisi vipi ndani yako? Ghafla ungehisi, “Nimependezwa sana na huyu mwaguzi, yuko sahihi sana! Sijawahi mwambia yeyote maisha yangu ya nyuma, alijuaje kuyahusu?” Haitakuwa vigumu sana kwa Shetani kujua maisha yako ya nyuma, siyo? Mungu amekuongoza hadi leo, na Shetani pia amewapotosha watu wakati huo wote na amekufuata. Shetani ni roho ovu; kupita kwa miongo kwako si chochote kwa Shetani na si vigumu kwake kujua vitu hivi. Wakati unajua kwamba alichosema Shetani ni sahihi, si unampa moyo wako? Siku zako za baadaye na bahati yako, si unategemea udhibiti wake? Papo hapo, moyo wako utahisi heshima ama ustahi kwake, na kwa watu wengine, nafsi zao pengine tayari zimenyakuliwa naye. Na utamwuliza mwaguzi mara moja: “Napaswa kufanya nini baada ya hapa? Napaswa kuepukana na nini mwaka ujao? Ni vitu gani ambavyo sipaswi kufanya? Na kisha atasema: “Hupaswi kwenda pale, hupaswi kufanya hili, usivae nguo za rangi fulani, hupaswi kwenda pahali kama hapo na hapo mara nyingi, na unapaswa kufanya mambo fulani zaidi…” Si utatia vyote anavyosema moyoni mara moja? (Ndiyo.) Ungevikariri haraka kuliko neno la Mungu. Mbona ungevikariri haraka hivyo? (Vina faida kwangu.) Kwa sababu ungetaka kumtegemea Shetani kwa sababu ya bahati njema, si hapa ndipo anaunyakua moyo wako? Unapofanya kile anachosema na maneno yake sasa yanakuwa ukweli kama alivyotabiri, hungetaka kurudi nyuma kwake na kujua ni bahati gani mwaka unaokuja utaleta? (Ndiyo.) Utafanya chochote Shetani anakwambia ufanye na utaepukana na vitu anakwambia uepukane navyo, si unatii vyote anasema? Utaletwa chini ya bawa lake haraka sana, kupotoshwa, na kuwekwa chini ya udhibiti wake. Hii inafanyika kwa sababu unaamini anachosema ni ukweli na kwa sababu unaamini kwamba anajua kuhusu maisha yako ya nyuma, maisha yako ya sasa, na vitu ambavyo siku za badaye zitaleta; hii ni mbinu Shetani anatumia kudhibiti watu. Lakini kwa kweli, ni nani aliye katika udhibiti? Ni Mungu Mwenyewe, si Shetani. Shetani anatumia tu hila zake hapa kudanganya watu wajinga, kuwadanganya watu wanaoona tu ulimwengu wa maumbile kumwamini na kumtegemea. Kisha, wataanguka katika mshiko wa Shetani na kutii kila neno lake. Lakini Shetani wakati wowote hupunguza jitihada watu wanapotaka kumwamini na kumfuata Mungu? Shetani hapunguzi jitihada. Katika hali hii, watu kweli wanaanguka katika mshiko wa Shetani? (Ndiyo.) Tunaweza kusema kwamba tabia ya Shetani hapa haina haya hata kidogo? (Ndiyo.) Mbona tungesema hivyo? (Shetani anatumia hila.) Hmm, kwa sababu hila za Shetani ni za ulaghai na zinadanganya. Shetani hana haya na anawadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti kila kitu chao na kuwadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti hatima zao. Hii inawafanya watu wajinga kuja kumtii kabisa na anawadanganya na sentensi moja ama mbili tu na katika kuchanganyika kwao, watu wanasujudu mbele yake. Si hii ni sahihi? (Ndiyo.) Hivyo, Shetani anatumia mbinu za aina gani, anasema nini kukufanya umwamini? Kwa mfano, pengine hujamwambia Shetani idadi ya watu katika familia yako, lakini anaweza kusema kwamba kuna watatu katika familia yako, akiwemo binti ambaye ana miaka 7, na pia umri wa wazazi wako. Iwapo ulikuwa na tuhuma na shaka zako mwanzoni, hutahisi kwamba anaaminika zaidi kidogo baada ya kusikia hayo? (Ndiyo.) Na kisha Shetani anaweza kusema, “Kazi imekuwa ngumu kwako leo, wakubwa wako hawakupi utambuzi unaostahili na daima wanafanya kazi dhidi yako.” Baada ya kuyasikia hayo, ungefikiri, “Hiyo ni sahihi kabisa! Mambo hayajakuwa yakienda vizuri kazini.” Hivyo ungemwamini Shetani zaidi kidogo. Kisha angesema kitu kingine kukudanganya, kukufanya umwamini hata zaidi, na kidogo kidogo, utajipata huwezi kupinga ama kuwa na tuhuma kwake tena. Shetani anatumia tu hila chache zisizo na maana, hata ndogo zisizojalisha, kukufadhaisha. Unapofadhaishwa, hutaweza kupata njia zako, hutajua kile cha kufanya, na utaanza kufuata kile Shetani anasema. Hii ni mbinu ya “ah nzuri sana” anayotumia Shetani kumpotosha mwanadamu pahali unapoingia katika mtego wake bila kusudi na unashawishiwa naye. Unaona, Shetani anakwambia mambo machache ambayo watu wanafikiria kuwa mambo mazuri, na kisha anakwambia kile cha kufanya na kile cha kuepuka na hivyo ndivyo unaanza kufuata njia hiyo bila kusudi. Punde unapoanza kufuata njia hiyo, haitakuwa chochote ila shida kwako; daima utakuwa ukifikiria kile alichosema Shetani na kile alichokwambia ufanye, na bila kujua utamilikiwa naye. Mbona hivi? Ni kwa sababu wanadamu hawana ukweli na hivyo hawawezi kusimama dhidi ya majaribu na ushawishi wa Shetani. Wanapokabiliwa na uovu, ujanja, usaliti, na kijicho cha Shetani, wanadamu ni wajinga sana, wasiojua na wanyonge, siyo? Si hii ni mojawapo ya njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? (Ndiyo.) Mwanadamu anadanganywa na kulaghaiwa bila kusudi, kidogo kidogo, kupitia mbinu mbalimbali za Shetani, kwa sababu hawana uwezo wa kutofautisha kati ya mema na hasi. Hawana kimo hiki, na uwezo wa kumshinda Shetani.
E. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu
Je, mienendo ya kijamii ni kitu kipya? (La.) Hivyo ilianza lini? Mtu anaweza kusema kwamba mienendo ya kijamii ilianza wakati Shetani alipoanza kuwapotosha watu? (Ndiyo.) Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo. Kuna kingine zaidi? Je, misemo maarufu ambayo watu wanapenda kusema inahesabika pia? Je, pia mitindo ya maisha ambayo watu wanataka inahesabika? Je, nyota wa muziki, watu mashuhuri, majarida, na riwaya ambazo watu hupenda zinahesabika? (Ndiyo.) Katika akili zenu, ni kipengele kipi cha mienendo hii kinaweza kumpotosha mwanadamu? Ni mienendo ipi inawavutia sana? Watu wengine husema: “Sisi sote tumefikia umri fulani, tuko katika miaka ya arobaini, hamsini, sitini, sabini ama themanini ambapo hatuwezi kufaa katika mienendo hii na haituvutii tena.” Je, hii ni sahihi? (La.) Wengine husema: “Hatufuati watu mashuhuri, hicho ni kitu ambacho vijana walio katika umri wa ujana na ishirini wanafanya; pia hatuvai nguo za mitindo ya kisasa, hicho ni kitu ambacho watu wanaojali sura wanafanya.” Kwa hivyo ni ipi kati ya hii inaweza kuwapotosha? (Misemo maarufu.) Je, hii misemo maarufu inaweza kuwapotosha watu? Huu ni msemo mmoja, na mnaweza kuona iwapo unawapotosha watu au la, “Pesa inamfanya farasi jike kwenda”; huu ni mwenendo? Si hiki ni kitu kibaya zaidi kulinganishwa na mienendo ya mavazi na chakula mliyotaja? (Ndiyo.) “Pesa inamfanya farasi jike kwenda” ni filosofia ya Shetani na inaenea katika kila jamii ya binadamu. Mnaweza kusema kwamba ni mwenendo kwa sababu umepatiwa kila mtu na sanasana uko katika mioyo yao. Watu walienda kutoka kutoukubali msemo huu hadi kuuzoea ili wanapokutana na maisha halisi, polepole waliukubali kwa kimya, kukiri uwepo wake na hatimaye, waliupa muhuri wao wa idhini. Sivyo? (Ndiyo.) Je, hii si njia ya Shetani kumpotosha mwanadamu? Pengine nyinyi mlioketi hapa hamwelewi msemo huu kwa kiwango sawa, lakini kila mtu ana viwango tofauti vya tafsiri na kukiri kwa msemo huu kutokana na mambo ambayo yamefanyika karibu nao na uzoefu wao binafsi, siyo? Licha ya kiwango cha uzoefu mtu anao na msemo huu, ni nini athari mbaya unaweza kuwa nao katika moyo wa mtu? (Watu wangeweza kufikiri kwamba pesa inaweza kufanya chochote, na wangeheshimu pesa.) Kitu fulani kinafichuliwa kupitia tabia ya binadamu ya watu katika dunia hii, mkiwemo nyinyi mlioketi hapa. Hiki kinafasiriwa vipi? Ni ibada ya pesa. Ni vigumu kutoa hili kwa moyo wa mtu? Ni vigumu sana! Inaonekana kwamba upotovu wa Shetani wa mwanadamu ni kamili kabisa! Tunaweza kusema hivyo? (Ndiyo.) Hivyo baada ya Shetani kutumia mwenendo huu kuwapotosha watu, unaonyeshwa vipi kwao? Hamhisi kwamba hamtaishi siku moja katika dunia hii bila pesa yoyote, kwamba hata siku moja haiwezekani? (Ndiyo.) Hadhi ya watu inatokana na kiasi cha pesa wakonayo na pia heshima yao. Migongo ya maskini imekunjwa kwa aibu, ilhali matajiri wanafurahia hadhi zao za juu. Wanatenda kwa njia ya kujigamba na wana majivuno, wakiongea kwa sauti kubwa na kuishi kwa kiburi. Msemo na mwenendo huu unaleta nini kwa watu? Si watu wengi wanaona kupata pesa kunastahili gharama yoyote? Si watu wengi hutoa Heshima na uadilifu wao wakitafuta pesa zaidi? Si watu wengi hupoteza fursa ya kufanya wajibu wao na kumfuata Mungu kwa sababu ya pesa? Si hii ni hasara kwa watu? (Ndiyo.) Si Shetani ni mbaya kutumia mbinu hii na msemo huu kumpotosha mwanadamu kwa kiwango kama hicho? Si hii ni hila yenye kijicho? Unaposonga kutoka kuukataa huu msemo maarufu hadi mwishowe kuukubali kama ukweli, moyo wako unaanguka kabisa chini ya mshiko wa Shetani, na hivyo unakuja kuishi naye bila kusudi. Msemo huu umekuathiri kwa kiwango kipi? Unaweza kujua njia ya ukweli, unaweza kujua ukweli, lakini huna nguvu ya kuufuatilia. Unaweza kujua kwa hakika neno la Mungu, lakini huko radhi kulipa gharama, huko radhi kuteseka kulipa gharama. Badala yake, kwako, ni afadhali utoe siku zako za baadaye na kudura yako kwenda kinyuma na Mungu hadi mwisho kabisa. Licha ya kile Mungu anasema, licha ya kile Mungu anafanya, licha ya kiasi unagundua kwamba upendo wa Mungu kwako ni wa kina na mkubwa, bado ungeendelea kwa njia hiyo kwa ukaidi na kulipa gharama ya msemo huu. Hii inamaanisha kwamba huu msemo tayari unadhibiti tabia na fikira zako, na unaona afadhali hatima yako idhibitiwe na msemo huu kuliko kuyatoa yote. Watu wanafanya hivi, wanadhibitiwa na msemo huu na kutawaliwa nao. Hii si athari ya Shetani kumpotosha mwanadamu? Hii si filosofia na tabia potovu ya Shetani ikikita mizizi kwa moyo wako? Ukifanya hivyo, si Shetani amefikia lengo lake? (Ndiyo.) Unaona jinsi Shetani amempotosha mwanadamu kwa njia hii? (La.) Hukumwona. Unaweza kumhisi? (La.) Hukuihisi. Je, unaona uovu wa Shetani hapa? (Ndiyo.) Shetani humpotosha mwanadamu wakati wote na pahali pote. Shetani anaifanya isiwezekane kwa mwanadamu kujilinda dhidi ya upotovu huu na anamfanya mwanadamu mnyonge kwake. Shetani anakufanya ukubali fikira zake, mitazamo yake na mambo maovu yanayotoka kwake katika hali ambapo huna kusudi na huna utambuzi wa kile kinachokufanyikia. Watu wanakubali kikamilifu vitu hivi na hawavibagui. Wanapenda sana vitu hivi na kuvishikilia kama hazina, wanaviacha vitu hivi viwatawale na kuwachezea, na hivi ndivyo upotovu wa Shetani wa mwanadamu unakuwa wa kina na kina zaidi.
Mbinu nyingi zilizojadiliwa awali ambazo Shetani hutumia kuwapotosha watu ni dhahiri na kila mtu amezipitia; Shetani huzitumia na haziwezi kuepukika. Mwanadamu ana maarifa na baadhi ya nadharia za kisayansi, mwanadamu anaishi na ushawishi wa desturi ya kitamaduni, na kila mtu anarithi desturi ya kitamaduni. Mwanadamu ataendeleza desturi ya kitamaduni aliyopewa kutoka kwa Shetani na pia kutenda pamoja na mienendo ya kijamii ambayo Shetani anawapa wanadamu. Licha ya kutoweza kutengana na Shetani, kushiriki na kile ambacho Shetani anafanya wakati wote, kukubali ujanja, kiburi, kijicho, na uovu wake—baada ya kumiliki tabia hizi za Shetani—je, mwanadamu ana furaha ama huzuni katika kuishi miongoni mwa wanadamu hawa na katika dunia hii? (Huzuni.) Mbona unasema hivyo? (Amefungwa na vitu hivi na maisha yake ni mapambano machungu.) Hmm. Unaweza kumwona mtu ambaye ana miwani na anaonekana wa hekima; pengine kamwe hapigi kelele, awe daima na lugha ya kushawishi, wa busara, na zaidi ya hayo, kwa sababu ya umri wake mkubwa, pengine amepitia vitu vingi na kuwa na uzoefu mkubwa; pengine anaweza kuzungumza kwa undani kuhusu masuala makubwa na madogo na kuwa na msingi dhabiti wa kile anachosema; pengine pia ana seti ya nadharia ya kutathmini uhalisi na sababu ya vitu; na watu pengine wanaweza kuangalia tabia yake, sura yake, na kuona jinsi anajibeba na kuona uadilifu wake na hulka yake na kutopata dosari kwake. Watu kama hawa hasa wanashughulika na mienendo ya kijamii ya sasa na hawachukuliwi kuwa wa mtindo wa kizamani; badala yake yeye ni mtu anayevumbua na kujaribu mawazo mapya kabisa yasiyokubalika kwa urahisi na ni mtu wa mitindo. Ingawa mtu huyu anaweza kuwa mzee, kamwe hayuko nyuma ya nyakati na kamwe si mzee sana kufunzwa. Juujuu, hakuna anayeweza kupata dosari kwake, lakini ndani amepotoshwa na Shetani kabisa na kikamilifu. Juujuu hakuna chochote kibaya, yeye ni mpole, ni muungwana, anayo maarifa na maadili fulani; ana uadilifu na vitu anavyojua vinalingana na vile wanavyojua vijana. Hata hivyo, kuhusu asili na kiini chake, mtu huyu ni mfano kamili na unaoishi wa Shetani, ana usawa kabisa na Shetani. Hili ni “tunda” la upotovu wa Shetani wa mwanadamu. Kile Nilichosema kinaweza kuwaumiza, lakini chote ni ukweli. Maarifa ambayo mwanadamu anasoma, sayansi anayoelewa, na njia anayochukua kufaa na mienendo ya jamii, bila ubaguzi, ni vyombo vya upotovu wa Shetani. Huu ni ukweli kabisa. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi miongoni mwa tabia ambayo imepotoshwa kabisa na Shetani na mwanadamu hana njia ya kujua utakatifu wa Mungu ni nini na kiini cha Mungu ni nini. Hii ni kwa sababu juujuu mtu hawezi kupata dosari kwa njia ambazo Shetani anampotosha mwanadamu; hakuna anayeweza kuamua kutoka kwa tabia ya mtu kwamba kuna chochote kibaya. Kila mtu anaendelea na kazi yake kwa kawaida na kuishi maisha ya kawaida; wanasoma vitabu na magazeti kwa kawaida, wanasoma na kuzungumza kwa kawaida; watu wengine hata wamejifunza kuwa na sura ya kinafiki ya maadili ili waweze kusema salamu zao, kuwa na heshima, kuwa na adabu, kuwaelewa wengine, kuwa na urafiki, kuwasaidia wengine, kuwa wenye hisani, na wataepuka kulalamika kwa wengine na kuepuka kutumia watu kwa manufaa yao. Hata hivyo, tabia yao iliyopotoka ya kishetani imekita mizizi ndani yao; kiini hiki hakiwezi kubadilishwa kwa kutegemea juhudi za nje. Mwanadamu hana uwezo wa kujua utakatifu wa Mungu kwa sababu ya kiini hiki, na licha ya kiini cha utakatifu wa Mungu kuwekwa wazi kwa mwanadamu, mwanadamu hakichukulii kwa umakini. Hii ni kwa sababu Shetani tayari amemiliki kabisa hisia, fikira, mitazamo, na mawazo ya mwanadamu kupitia njia mbalimbali. Huu umiliki na upotovu si ya muda mfupi ama ya mara kwa mara; upo kila mahali na kila wakati. Kwa hivyo, watu wengi ambao wamemwamini Mungu kwa miaka mitatu au minne—hata miaka sita na saba—bado wanashikilia mawazo na mitazamo ambayo Shetani amewaekea kana kwamba wanashikilia hazina. Kwa sababu mwanadamu ameukubali uovu, kiburi, na asili ya kijicho ya Shetani, bila kuepukika kwa mahusiano ya ana kwa ana ya mwanadamu mara nyingi kuna migogoro, mara nyingi kuna magombano na kutokuwa na uwiano, mambo ambayo yameumbwa kwa sababu ya asili ya kiburi ya Shetani. Iwapo Shetani angempa mwanadamu vitu vyema—kwa mfano, iwapo Uconfucius na Udao wa desturi ya kitamaduni ambayo mwanadamu alikubali ilichukuliwa kuwa vitu vizuri—watu wa aina sawa wanapaswa kuweza kupatana na wengine baada ya kukubali vitu hivyo, siyo? Hivyo mbona kuna mgawanyiko mkubwa kati ya watu waliokubali vitu sawa? Mbona hivyo? Ni kwa sababu viti hivi vimetoka kwa Shetani na Shetani husababisha mgawanyiko miongoni mwa watu. Vitu ambavyo Shetani anapatiana, bila kujali jinsi vinavyoonekana kuwa vya heshima na vikubwa juujuu, vinamletea mwanadamu na vinaleta katika maisha ya mwanadamu kiburi pekee, na si chochote ila ujanja wa asili ovu ya Shetani. Sivyo? Mtu ambaye angeweza kujificha, kumiliki maarifa mengi, ama kuwa na malezi mazuri angekuwa na wakati mgumu kusitiri tabia yao potovu ya kishetani. Haijalishi mtu huyu atajificha kwa njia ngapi, kama ulimfikiri kuwa mtakatifu, ama kama ulifikiri ni mkamilifu, ama kama ulifikiri ni malaika, haijalishi ulifikiri ni mtu safi vipi, maisha yake yangekuwaje nyuma ya pazia? Utaona asili ipi katika ufunuo wa tabia yake? Bila shaka ungeona asili ovu ya Shetani. Mtu anaweza kusema hivyo? (Ndiyo.) Kwa mfano, tuseme mnamjua mtu wa karibu nanyi ambaye mnafikiri kuwa mtu mzuri, ama ulimfikiri kuwa mtu mzuri, pengine mtu uliyemwabudu kama Mungu. Kwa kimo chako cha sasa, unawafikiri vipi? Kwanza, unaangalia iwapo mtu wa aina hii ana ama hana ubinadamu, iwapo ni mwaminifu, iwapo ana upendo wa kweli kwa watu, iwapo maneno na vitendo vyao vinafaidi na kusaidia wengine. (La.) Yaitwayo wema, upendo na uzuri unaofichuliwa hapa, ni nini kweli? Yote ni sura ya kinafiki, yote ni uongo. Hii sura ya kinafiki ya nyuma ya pazia ina madhumuni maovu ya chinichini: Ni ya kumfanya mtu huyo apendwe na kuabudiwa kama Mungu. Je, mnaona jambo hili kwa dhahiri? (Ndiyo.)
Mbinu ambazo Shetani anatumia kuwapotosha watu zinaletea nini binadamu? Kuna chochote chema kuzihusu? (La.) Kwanza, mwanadamu anaweza kutofautisha kati ya mema na mabaya? (La.) Unaona, katika dunia hii, awe ni mtu fulani mkubwa ama gazeti fulani, ama kituo fulani cha redio, yote yatasema kwamba hiki ama kile ni chema ama kibaya, si hayo ni barabara? (La.) Si hayo ni sahihi? (La.) Tathmini zao za matukio na watu ni za haki? (La.) Kuna ukweli ndani ya tathmini hizi? (La.) Je, dunia hii ama ubinadamu huu unatathmini vitu vyema na hasi kulingana na kiwango cha ukweli? (La.) Mbona watu hawana uwezo huo? Watu wamesoma maarifa mengi na wanajua mengi kuhusu sayansi, uwezo wao si mkubwa kutosha? Mbona hawawezi kutofautisha kati ya vitu vyema na hasi? Mbona hivi? (Kwa sababu watu hawana ukweli; sayansi na maarifa si ukweli.) Kila kitu Shetani anauletea ubinadamu ni uovu na upotovu na hakina ukweli, uhai, na njia. Na uovu na upotovu ambao Shetani anamletea mwanadamu, unaweza kusema kwamba Shetani ana upendo? Unaweza kusema kwamba mwanadamu ana upendo? Watu wengine wanaweza kusema: “Huko sahihi, kuna watu wengi duniani kote wanaosaidia maskini na watu wasio na makazi. Si hao ni watu wazuri? Pia kuna mashirika ya hisani ambayo yanafanya kazi nzuri, si kazi yote wanayofanya ni ya uzuri?” Kwa hivyo tunasema nini kuhusu hayo? Shetani anatumia mbinu na nadharia mbalimbali kumpotosha mwanadamu; huu upotovu wa mwanadamu ni dhana isiyo dhahiri? La, siyo dhahiri. Shetani pia anafanya vitu vingine vya utendaji, vikiwemo baadhi ya vitu vya uongo vinavyojifanya kuwa vitu vizuri, na pia vitendo vya udanganyifu kabisa, ambavyo Shetani anafanya na nia na madhumuni yake mwenyewe. Watu waliopotoshwa na Shetani ni kitu kimoja; pia wako katika dunia hii na katika jamii wakikuza mtazamo ama nadharia. Katika kila nasaba na katika kila kipindi cha historia wanakuza nadharia na kuingiza baadhi ya fikira ndani ya wanadamu. Fikira na nadharia hizi polepole zinakita mizizi katika mioyo ya watu, na kisha watu wanaanza kuishi kwa nadharia na fikira hizi; si wanakuwa Shetani bila kusudi? Si watu wako kitu kimoja na Shetani? Wakati watu wamekuwa kitu kimoja na Shetani, ni nini mtazamo wao kwa Mungu mwishowe? Si ni mtazamo sawa ambao Shetani anao kwa Mungu? Hakuna anayethubutu kukubali haya, siyo? Ni ya kutisha sana! Watu ni Shetani, na asili yao ni ile asili ya Shetani. Mbona Nasema kwamba asili ya Shetani ni ovu? Hii inaamuliwa na kuchambuliwa kulingana na kile Shetani amefanya na vitu ambavyo Shetani amefichua; si bila ustahili kusema kwamba Shetani ni mwovu. Iwapo Ningesema tu kwamba Shetani ni mwovu, mngefikiri nini? Mngefikiri, “Bila shaka Shetani ni mwovu.” Hivyo nitakuuliza: “Ni kipengele kipi cha Shetani ni ovu?” Ukisema: “Shetani kumpinga Mungu ni uovu,” bado hutakuwa ukizungumza kwa uwazi. Sasa tumesema mambo maalum kwa njia hii; je, mna uelewa kuhusu maudhui maalum ya kiini cha uovu wa Shetani? (Ndiyo.) Sasa kwa kuwa mmekuwa na huu uelewa wa asili ovu ya Shetani, ni kiasi gani mnaelewa kuhusu nyinyi wenyewe? Je, mambo haya yanahusiana? (Ndiyo.) Je, uhusiano huu unawaumiza? (La.) Ni wenye msaada kwenu? (Ndiyo.) Ni wenye msaada vipi? (Msaada mkubwa sana!) Hebu tuzungumzie mambo maalum; Sitasikia maneno yenye maana nyingi. Ni kwa kiasi kipi “mkubwa sana” kinarejelea? (Tunajua vitu ambavyo Mungu anachukia, vitu vipi vinaenda kinyume na Mungu; mioyo yetu inaelewa kiasi kuhusu vitu hivi.) Mm, kuna kitu kingine cha kuongezea? Ninaposhiriki kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, ni muhimu Niwe na ushirika kuhusu kiini ovu cha shetani, ni nini maoni yako? (Ndiyo, ni muhimu.) Mbona? (Uovu wa Shetani unauweka utakatifu wa Mungu katika heshima ya juu.) Je, ndivyo ilivyo? Hii ni sahihi kidogo kwa sababu bila uovu wa Shetani, watu hawatajua kuhusu utakatifu wa Mungu; hii ni sahihi. Hata hivyo, ukisema kwamba utakatifu wa Mungu upo tu kwa sababu ya tofauti yake na uovu wa Shetani, hii ni sahihi? Hii hoja si sahihi. Utakatifu wa Mungu ni kiini kiasilia cha Mungu; hata ingawa Mungu anaufichua ama kutenda, Anayo hiki kiini kiasilia na kinafichuliwa kiasili, ni cha Mungu Mwenyewe na daima kimekuwepo, lakini mwanadamu hawezi kukiona. Mwanadamu anaishi miongoni mwa tabia potovu ya Shetani na miongoni mwa kiini chake potovu, na mwanadamu hajui kuhusu utakatifu ama maudhui maalum ya utakatifu wa Mungu. Si hii ni sahihi? Hivyo, unaona ikiwa muhimu kwamba tushiriki kwanza kuhusu kiini ovu cha Shetani? (Ndiyo, ni muhimu.) Unaona, tumeshiriki kuhusu vipengele vingi vya upekee wa Mungu na hatukutaja kiini cha Shetani, siyo? Watu wengine wanaweza kuonyesha baadhi ya shaka kama, “Unashiriki kuhusu Mungu Mwenyewe, mbona Unazungumza daima kuhusu jinsi Shetani anawapotosha watu na jinsi asili ya Shetani ni ovu?” Umeyaweka mapumzikoni mashaka haya? (Ndiyo.) Uliyawekaje mapumzikoni? (Kupitia ushirika wa Mungu, tulitofautisha kile ambacho ni ovu.) Wakati watu wana utambuzi wa uovu na wakati wana ufafanuzi sahihi wa uovu, wakati watu wanaweza kuona wazi maudhui maalum na udhihirisho wa uovu, chanzo na kiini cha uovu—wakati utakatifu wa Mungu unajadiliwa sasa—watu basi watatambua wazi, ama kuufahamu wazi kama utakatifu wa Mungu, kama utakatifu wa kweli. Nisipojadili uovu wa Shetani, watu wengine wataamini kimakosa kwamba kitu fulani ambacho watu wanafanya katika jamii ama miongoni mwa watu—ama kitu fulani katika dunia hii—kinaweza kuhusiana na utakatifu. Si mtazamo huu ni wa makosa? (Ndiyo.) Hivi, Nimeshiriki kuhusu kiini cha Shetani. Mmefikia uelewa upi wa utakatifu wa Mungu kupitia uzoefu wenu wa miaka ya hivi karibuni, kutokana na nyinyi kuona neno la Mungu na kutokana na kupitia kazi Yake? Endelea, na uuzungumzie. Si lazima utumie maneno yanayofurahisha sikio, zungumza tu kutoka kwa uzoefu wako mwenyewe, utakatifu wa Mungu ni upendo Wake tu? Ni upendo wa Mungu tu tunaoelezea kama utakatifu? Huo utakuwa wa upande mmoja sana, siyo? Si huo utakuwa wa upande mmoja? (Ndiyo.) Hivyo, mbali na upendo wa Mungu, kuna vipengele vingine vya kiini cha Mungu ambavyo mmeona? (Ndiyo.) Mmeona nini? (Mungu anachukia tamasha na likizo, mila, na ushirikina; huu ni utakatifu wa Mungu.) Ulisema tu kwamba Mungu anachukia mambo fulani; Mungu ni mtakatifu kwa hivyo Anachukia vitu, inamaanisha hivyo? (Ndiyo.) Katika mizizi ya hayo, ni nini utakatifu wa Mungu? Utakatifu wa Mungu hauna maudhui makubwa, ni kwamba tu Anachukia vitu? Katila akili zenu mnafikiria, “Kwa sababu Mungu anachukia vitu hivi ovu, hivyo mtu anaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu”? Si huu ni uvumi hapa? Si hii ni aina ya dhana na hukumu? Ni nini mwiko mkubwa zaidi inapokuja kwa kuelewa kiini cha Mungu? (Kuacha ukweli nyuma.) Ni wakati tunaacha ukweli nyuma kuzungumza kuhusu mafundisho ya kidini, huu ni mwiko mkubwa sana kufanya. Kitu kingine? (Uvumi na ubunifu.) Uvumi na ubunifu, huu pia ni mwiko wa nguvu sana. Mbona uvumi na ubunifu si wa manufaa? Vitu unavyobashiri kuhusu na kufikiria vitu ambavyo kweli unaweza kuona? (La.) Ni kiini cha kweli cha Mungu? (La.) Nini tena ni mwiko? Ni mwiko kuhesabu tu kifungu cha maneno yanayosikika kuwa mazuri kuhusu kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Si huku ni kujigamba na upuuzi? Hukumu na uvumi ni upuuzi, kama tu kuchukua maneno yanayosikika kuwa mazuri. Kuna kingine tena? Sifa tupu pia ni upuuzi, siyo? (Ndiyo.) Je, Mungu anafurahia kusikiza watu wakisema upuuzi wa aina hii? (La, hafurahii.) Ni nini kisawe cha “kutofurahia” kitu? (Kuhisi kutostareheka.) Anahisi kutostareheka kusikia huu upuuzi! Mungu anaongoza na kuokoa kundi la watu, na baada ya kundi hili la watu kusikia maneno Yake hawaelewi Anachomaanisha. Mtu anaweza kuuliza: “Mungu ni mwema?” na wangejibu, “Mwema!” “Mwema vipi?” “Mwema sana sana!” “Mungu anampenda mwanadamu?” “Ndiyo!” “Kiasi gani?” “Sana, sana zaidi!” “Unaweza kuelezea upendo wa Mungu?” “Ni wa kina zaidi kuliko bahari, wa juu zaidi kuliko anga!” Si huu ni upuuzi? Si huu upuuzi ni sawa na kile mlichotoka kusema kuhusu, “Mungu anachukia tabia potovu ya Shetani, hivyo Mungu ni mtakatifu”? (Ndiyo.) Si kile mlichotoka kusema ni upuuzi? Mengi ya haya mambo ya upuuzi yanayosemwa yanatoka wapi? (Shetani.) Yanatoka kwa Shetani. Mambo ya upuuzi yanayosemwa kimsingi yanatoka kwa kutowajibika kwa watu na kutomheshimu Mungu. Tunaweza kusema hayo? (Ndiyo.) Hukuwa na uelewa wowote lakini bado uliongea upuuzi, si huku ni kutowajibika? Si ni kutomheshimu Mungu? Umesoma kiasi kidogo cha maarifa, umeelewa kiasi kidogo cha kufikiria, na kiasi kidogo cha mantiki, ambayo umetumia hapa na, zaidi, umefanya hivyo ukimjua Mungu. Unafikiri Mungu anahisi kutostareheka kuyasikia hayo? Mnawezaje kumjua Mungu mkitumia mbinu hizi? Je, si hayo yanasikika kuwa ya kufedhehesha? Kwa hivyo, inapokuja kwa maarifa ya Mungu, mtu lazima awe makini sana; mahali unapojua Mungu, zungumza tu kuhusu hayo. Zungumza kwa uaminifu na kivitendo na usipambe maneno yako na pongezi za kawaida na usitumie sifa isiyostahilika; Mungu haihitaji na kitu kama hiki kinatoka kwa Shetani. Tabia ya Shetani ni ya kiburi na Shetani anapenda kupewa sifa isiyostahilika na kusikia maneno mazuri. Shetani ataridhishwa na kufurahia iwapo watu watataja maneno yote mazuri ambayo wamejifunza na kutumia maneno haya kwa Shetani. Lakini Mungu hahitaji hii; Mungu hahitaji kuvishwa kilemba cha ukoka ama sifa isiyostahilika na Hahitaji kwamba watu wazungumze upuuzi na kumsifu kwa upofu. Mungu anachukizwa sana na hata Hatasikiza sifa ambayo haiko sambamba na ukweli. Hivyo, wakati watu wengine wanamsifu Mungu kwa upofu na kile wanachosema hakilingani na kile kiko katika mioyo yao na wanapofanya viapo kwa upofu na kumwomba ovyo ovyo, Mungu hasikizi hata kidogo. Lazima uwajibike kwa kile unachosema. Ikiwa hujui jambo, sema tu; ikiwa unajua jambo, onyesha hivyo kwa njia ya kitendo. Sasa, kwa maudhui halisi ya utakatifu wa Mungu, mna uelewa maalum kuuhusu? Sasa hamtathubutu kusema vitu vya upuuzi, siyo? Hamwongei upuuzi, lakini hamwezi kuwacha kuongea, kwa hivyo mnapaswa kuwa na uelewa fulani, siyo? Mnafikiria jambo hili? Mnalishughulikia kwa makini, siyo? Unaweza kusema mambo machache sasa. (Nilipofichua uasi, nilipokuwa na makosa, nilipokea hukumu na kuadibu kwa Mungu, na hapo niliona utakatifu wa Mungu. Na nilipoanguka katika hali na mazingira ambayo hayakukubaliana na matarajio yangu, niliomba kuhusu mambo haya na kutafuta nia za Mungu na Mungu aliponipa nuru na kuniongoza na maneno Yake, niliona utakatifu wa Mungu.) Hmm, haya yametoka kwa uzoefu wako mwenyewe, siyo? (Wakati Mungu anawaongoza watu katika njia yote, na sababu anatawala watu, kwa hayo naona utakatifu wa Mungu. Kwa kweli, kwa kile ambacho Mungu ametoka kuzungumzia jinsi Shetani anampotosha mwanadamu na mwanadamu amekuwa akiishi chini ya upotovu na mateso ya Shetani, mwanadamu hana mamlaka juu ya haya, kwa kweli naona utakatifu wa Mungu kupitia kazi ya Mungu kwa mwanadamu.) (Nimeona kwa kile Mungu amezungumzia kwamba mwanadamu amepotoshwa na kudhuriwa na Shetani hivi. Hata hivyo, Mungu ametoa yote kutuokoa na kutoka haya naona utakatifu wa Mungu.) Hii ni njia ya kweli ya kuzungumza na ni maarifa ya kweli. Kuna maoni mengine tofauti na haya? (Sijui iwapo uelewa wangu ni sahihi au la. Katika ushirika ambao Mungu alikuwa na sisi hivi karibuni, naona uovu wa Shetani kwa mambo ambayo Shetani anasema na kufanya. Katika ushirika wa kwanza, alisema kwamba Mungu alimwambia mwanadamu kile alichoweza na asichoweza kula, na kwamba maneno ya Mungu yalifichua usafi na uwazi; kutoka kwa haya naona utakatifu wa Mungu. Hiki ni kile naweza kuongezea.) Mm. Kwa kile mmesikia watu hawa wakisema, mnasema Amina zaidi kwa maneno ya nani? Matamshi ya nani, ushirika wa nani ulikuwa karibu zaidi na ushirika wa mada yetu leo, ya nani ilikuwa ya kweli zaidi? Ushirika wa dada wa mwisho ulikuwa vipi? (Mzuri.) Unasema Amina kwa kile alichosema, ni nini alichosema kilichokuwa sahihi kwa lengo? Unaweza kuwa wazi, sema unachotaka kusema na usijali kuhusu kutokuwa sahihi. (Katika maneno ambayo dada alizungumza hivi karibuni, nilisikia kwamba neno la Mungu linaeleweka kwa urahisi na ni wazi sana, si kama maneno ya Shetani yasiyo ya moja kwa moja. Niliona utakatifu wa Mungu kwa haya.) Hmm, hii ni sehemu ya hayo. Je, nyote mlisikia kilichosemwa hivi karibuni? (Ndiyo.) Kilikuwa sahihi? (Ndiyo.) Hebu tumpigie dada makofi. Vizuri sana. Naona kwamba mmepata kitu katika ushirika hizi mbili za hivi karibuni, lakini lazima nyinyi mwendelee kufanya kazi kwa bidii. Ni lazima mfanye kazi kwa sababu kuelewa kiini cha Mungu ni somo kubwa sana; si kitu ambacho mtu anaweza kuelewa mara moja ama anaweza kuzungumza wazi kwa maneno machache tu.
Kila kipengele cha tabia potovu ya Kishetani ya watu, maarifa, filosofia, fikira na mitazamo ya watu, na vipengele binafsi vinawazuia pakubwa kujua kiini cha Mungu; hivyo mnapozisikia mada hizi, mada zingine zinaweza kuwa mbali kwenu kufikia, mada zingine pengine hamtaelewa, ilhali mada zingine pengine kimsingi hamtalingana nazo na hali halisi. Licha ya hayo, Nimesikia kuhusu uelewa wenu wa utakatifu wa Mungu na Najua kwamba katika mioyo yenu mmeanza kukubali kile Nilichosema na kushiriki kuhusu utakatifu wa Mungu. Najua kwamba katika mioyo yenu hamu yenu ya kuelewa kiini cha utakatifu wa Mungu imeanza kuchipuka. Lakini ni nini kinachonifanya kuwa na furaha zaidi? Ni kwamba wengine wenu tayari wanaweza kutumia maneno rahisi sana kuelezea maarifa yenu ya utakatifu wa Mungu. Ingawa hiki ni kitu rahisi kusema na Nimekisema awali, katika mioyo ya wengi wenu hii bado haijakubaliwa ama kuweka alama. Hata hivyo, wengine wenu wameweka maneno haya moyoni na ni vizuri kabisa na huu ni mwanzo mzuri sana. Natumai kwamba kwa mada ambazo mnafikiri kuwa za maana sana—ama kwa mada ambazo ziko mbali kwenu kufikia—mtaendelea kushiriki katika ushirika, na kufanya ushirika zaidi na zaidi. Kwa yale masuala ambayo yako mbali kwenu kufikia kutakuwa na mtu wa kuwapa mwongozo zaidi. Mkishiriki katika ushirika zaidi kuhusu maeneo ambayo mnaweza kufikia sasa, Roho Mtakatifu atafanya kazi Yake na mtakuwa na uelewa mkubwa zaidi. Kuelewa kiini cha Mungu na kujua kiini cha Mungu kinapeana msaada usioweza kupimika kwa kuingia kwa watu katika maisha. Natumai kwamba hamtapuuza haya ama kuyaona kama mchezo; kwa sababu kumjua Mungu ni msingi muhimu na msingi wa imani ya mwanadamu kwa Mungu na ufuatiliaji wa mwanadamu wa ukweli na wokovu na kitu ambacho hakifai kuachiliwa. Iwapo mwanadamu anamwamini Mungu lakini hamjui Mungu, na iwapo mwanadamu anaishi miongoni mwa baadhi ya barua na mafundisho ya kidini, hutawahi kufikia wokovu hata kama utatenda na kuishi kulingana na maneno ya juujuu ya ukweli. Hiyo ni kusema, iwapo imani yako kwa Mungu haitokani na kumjua, basi imani yako haimaanishi chochote. Unaelewa, sivyo? (Ndiyo, tunaelewa.) Ushirika wetu utaishia hapa kwa leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni