Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kuhusu Majina na Utambulisho" (Sehemu ya Kwanza)
Mwenyezi Mungu anasema, "Yesu aliwakilisha Roho wa Mungu, na Alikuwa Roho wa Mungu Akifanya kazi moja kwa moja. Alifanya kazi ya enzi mpya, kazi ambayo hakuna aliyekuwa amefanya mbeleni. Yeye Alifungua njia mpya, Alimwakilisha Yehova, na Alimwakilisha Mungu Mwenyewe.
Sura ya 5 Lazima Uujue Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili
5. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili.
Maneno Husika ya Mungu:
Umuhimu wa kupata mwili ni kwamba mtu wa kawaida Anatekeleza kazi ya Mungu Mwenyewe; yaani, kwamba Mungu Anatekeleza kazi Yake ya uungu kwa wanadamu na hivyo kumshinda Shetani. Kupata mwili kunamaanisha kwamba Roho wa Mungu Anakuwa Mwili, yaani, Mungu Anakuwa mwili; kazi Anayoifanya katika mwili ni kazi ya Roho, inayothibitika katika mwili, na kuonyeshwa kwa mwili.