Ijumaa, 25 Mei 2018

39. Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo

Wu Xia    Mji wa Linyi , Mkoa wa Shandong
Baada ya kuikubali kazi hii na kula na kunywa neno la Mungu, ilikuwa dhahiri kwangu kwamba ni muhimu sana kwamba mimi nijifahamu. Kwa hiyo, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, nilihakikisha nimejithibitisha tena dhidi ya neno ambalo Mungu humfichua mwanadamu. Katika hali nyingi, niliweza kutambua kasoro zangu na upungufu. Nilihisi kwamba ningekuja kujifahamu kweli. Hata hivyo, ilikuwa ni kwa njia ya ufunuo kutoka kwa Mungu tu nilipoweza kuona kwamba kwa hakika sikujifahamu kulingana na neno la Mungu.

Alhamisi, 24 Mei 2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (3) - Umuhimu wa Jina la Mungu

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (3) - Umuhimu wa Jina la Mungu

"Yehova" na "Yesu" yalikuwa ni majina ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, na imetabiriwa katika Ufunuo kuwa Mungu atakuwa na jina jipya katika siku za mwisho. Ni kwa nini Mungu anaitwa kwa majina tofauti katika enzi mbalimbali? Majina haya mawili ya "Yehova" na "Yesu" yana umuhimu gani? Video hii fupi itakusaidia kukutatulia fumbo hili.

46. Maana halisi ya "Uasi dhidi ya Mungu"

Kanisa la Mwenyezi Mungu, ushuhuda, Umeme wa Mashariki

46. Maana halisi ya "Uasi dhidi ya Mungu"


Zhang Jun    Mji wa Shenyang, Mkoa wa Liaoning
Katika siku za nyuma, niliamini kuwa "uasi dhidi ya Mungu" ilimaanisha kumsaliti Mungu, kuacha kanisa, au kuutelekeza wajibu wa mtu. Nilidhani tabia hizi hufanyiza uasi. Kwa hiyo, wakati wowote niliposikia kuhusu watu wakihusika katika tabia hizo, ningejikumbusha kwamba sipaswi kuasi dhidi ya Mungu kama walivyofanya. Aidha, nilikuwa mwangalifu katika jitihada zangu zote na nilishikilia kazi zote nilizopewa na kanisa. Sikurudi nyuma kutoka kwa wajibu wangu wakati niliposhughulikiwa na kupogolewa wala kuondoka kutoka kanisani nilipojaribiwa, bila kujali shida. Kwa hiyo, niliamini kwamba sikuwahi kuasi dhidi ya Mungu kamwe. Nilihisi kuwa nilikuwa nimepata hadhi fulani tayari na nilikuwa na hakika kwamba ningemfuata Mungu mpaka mwisho na hatimaye kufanikisha wokovu.

Jumatano, 23 Mei 2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (2) - Je, ni Kweli kuwa Jina la Mungu Haliwezi Kubadilika?

 "Jina la Mungu Limebadilika?!" (2) - Je, ni Kweli kuwa Jina la Mungu Haliwezi Kubadilika?

Wachungaji na wazee wa ulimwengu wa kidini mara nyingi huhubiri kwa waumini kuwa jina la Bwana Yesu haliwezi kamwe kubadilika na kuwa ni kwa kutegemea tu jina la Bwana Yesu ndio tunaweza kuokolewa. Je, mtazamo wa aina hii unaambatana na kuweli? Yehova Mungu alisema, "kabla yangu hakukuwa na Mungu aliyeumbwa, wala hakutakuwa baada yangu. Mimi, hata mimi, ni BWANA; na isipokuwa mimi hakuna mwokozi" (Isaya 43:10-11). Katika Enzi ya Neema, Mungu mwenye mwili alichukua jina la Yesu. Mungu hawezi kubadilika, hivyo jina Lake linawezaje kubadilia? Zaidi ya hayo, Ufunuo unatabiri kuwa Mungu atakuwa na jina jipya katika siku za mwisho, hivyo haya yote yanahusu nini? Watu wengi hawajui hili, lakini video hii fupi itakufichulia ukweli.

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Sita

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa watu, Mungu ni mkuu mno, mwenye utele mno, wa ajabu mno, Asiyeeleweka mno; machoni pao, maneno ya Mungu hupaa juu, na huonekana kama kazi bora sana ya ulimwengu. Lakini kwa vile watu wana kasoro nyingi sana, na akili zao ni za kawaida sana, na, zaidi ya hayo, kwa kuwa uwezo wao wa kukubali ni haba mno, bila kujali vile Mungu hunena maneno Yake kwa dhahiri, wanabaki palepale bila kutikisika, kana kwamba wana ugonjwa wa akili. Wanapokuwa na njaa, hawaelewi kwamba lazima wale, wanapokuwa na kiu, hawaelewi kwamba lazima wanywe maji; wanaendelea tu kupaaza sauti na kupiga yowe, kana kwamba kuna dhiki isiyoelezeka katika kina cha roho zao, lakini hawawezi kuzungumza kuihusu.

Jumanne, 22 Mei 2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (1) - Je, Kuna Maneno Mengine ya Mungu Kando ya Yale Yaliyo kwenye Biblia?

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (1) - Je, Kuna Maneno Mengine ya Mungu Kando ya Yale Yaliyo kwenye Biblia?

Biblia inasema, "Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kilichofungwa kwa mihuri saba" (Ufunuo 5:1). "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa; Kwa yule ashindaye nitampa mana iliyofichwa aile" (Ufunuo 2:17). Kulingana na Biblia, Bwana atakaporudi katika siku za mwisho Atafungua kitabu, afungue mihuri saba na ampe mwanadamu mana iliyofichwa. Lakini wachungaji na wazee wengine wa ulimwengu wa kidini wanaamini kuwa maneno yote ya Mungu yameandikwa katika Biblia na kuwa hakuna maneno mengine ya Mungu kando ya yale yaliyo kwenye Biblia. Je, mtazamo wa aina hiiunalinganana ukweli? Je, kwa kweli hakuna maneno mengine ya Mungu kando ya yale yaliyo kwenye Biblia? Video hii fupi itakuangazia maswali haya.