Jumatano, 23 Mei 2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (2) - Je, ni Kweli kuwa Jina la Mungu Haliwezi Kubadilika?

 "Jina la Mungu Limebadilika?!" (2) - Je, ni Kweli kuwa Jina la Mungu Haliwezi Kubadilika?

Wachungaji na wazee wa ulimwengu wa kidini mara nyingi huhubiri kwa waumini kuwa jina la Bwana Yesu haliwezi kamwe kubadilika na kuwa ni kwa kutegemea tu jina la Bwana Yesu ndio tunaweza kuokolewa. Je, mtazamo wa aina hii unaambatana na kuweli? Yehova Mungu alisema, "kabla yangu hakukuwa na Mungu aliyeumbwa, wala hakutakuwa baada yangu. Mimi, hata mimi, ni BWANA; na isipokuwa mimi hakuna mwokozi" (Isaya 43:10-11). Katika Enzi ya Neema, Mungu mwenye mwili alichukua jina la Yesu. Mungu hawezi kubadilika, hivyo jina Lake linawezaje kubadilia? Zaidi ya hayo, Ufunuo unatabiri kuwa Mungu atakuwa na jina jipya katika siku za mwisho, hivyo haya yote yanahusu nini? Watu wengi hawajui hili, lakini video hii fupi itakufichulia ukweli.

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Sita

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa watu, Mungu ni mkuu mno, mwenye utele mno, wa ajabu mno, Asiyeeleweka mno; machoni pao, maneno ya Mungu hupaa juu, na huonekana kama kazi bora sana ya ulimwengu. Lakini kwa vile watu wana kasoro nyingi sana, na akili zao ni za kawaida sana, na, zaidi ya hayo, kwa kuwa uwezo wao wa kukubali ni haba mno, bila kujali vile Mungu hunena maneno Yake kwa dhahiri, wanabaki palepale bila kutikisika, kana kwamba wana ugonjwa wa akili. Wanapokuwa na njaa, hawaelewi kwamba lazima wale, wanapokuwa na kiu, hawaelewi kwamba lazima wanywe maji; wanaendelea tu kupaaza sauti na kupiga yowe, kana kwamba kuna dhiki isiyoelezeka katika kina cha roho zao, lakini hawawezi kuzungumza kuihusu.

Jumanne, 22 Mei 2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (1) - Je, Kuna Maneno Mengine ya Mungu Kando ya Yale Yaliyo kwenye Biblia?

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (1) - Je, Kuna Maneno Mengine ya Mungu Kando ya Yale Yaliyo kwenye Biblia?

Biblia inasema, "Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kilichofungwa kwa mihuri saba" (Ufunuo 5:1). "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa; Kwa yule ashindaye nitampa mana iliyofichwa aile" (Ufunuo 2:17). Kulingana na Biblia, Bwana atakaporudi katika siku za mwisho Atafungua kitabu, afungue mihuri saba na ampe mwanadamu mana iliyofichwa. Lakini wachungaji na wazee wengine wa ulimwengu wa kidini wanaamini kuwa maneno yote ya Mungu yameandikwa katika Biblia na kuwa hakuna maneno mengine ya Mungu kando ya yale yaliyo kwenye Biblia. Je, mtazamo wa aina hiiunalinganana ukweli? Je, kwa kweli hakuna maneno mengine ya Mungu kando ya yale yaliyo kwenye Biblia? Video hii fupi itakuangazia maswali haya.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sisitiza Zaidi Kwa Uhalisia

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mtu ana uwezekano wa kukamilishwa na Mungu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuelewa ni huduma gani kwa Mungu itakayofaa zaidi makusudi ya Mungu. Watu wengi hawajui kumwamini Mungu humaanisha nini na hawajui chochote kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu. Yaani, watu wengi sana hawana ufahamu wa kazi ya Mungu au lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu. Hadi leo, watu wengi sana bado wanadhani kumwamini Mungu kunahusu kwenda mbinguni na roho zao kuokolewa. Bado hawajui chochote kuhusu umuhimu mahususi wa kumwamini Mungu, na aidha hawana ufahamu wowote wa kazi muhimu kabisa ya Mungu katika mpango Wake wa usimamizi. Kwa aina zote za sababu zao binafsi, watu hawavutiwi na kazi ya Mungu na hawatafakari juu ya makusudi ya Mungu au mpango wa Mungu wa usimamizi.

Jumatatu, 21 Mei 2018

Wimbo wa Sifa "Upendo wa Kweli wa Mungu" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitle)

Wimbo wa Sifa "Upendo wa Kweli wa Mungu" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitle)


Leo naja mbele ya Mungu tena,
naona uso Wake wa kupendeza.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
nimeacha siku zangu za zamani za kuzurura nyuma yangu.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
kufurahia neno Lake kunanijaza na furaha.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
moyo wangu una mengi ya kusema.
Ni maneno Yake mororo yanayoninyunyizia
na kunirutubisha ili nikue.

Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu


Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu



Mwenyezi Mungu alisema, Kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni mojawapo ya hatua muhimu sana za kuingia katika maneno ya Mungu, na ni funzo ambalo watu wote sasa wana haja ya haraka kuingia ndani. Njia za kuingia za kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni:
1. Ondoa moyo wako kwa mambo ya nje, tulia mbele ya Mungu, na uombe Mungu kwa moyo uliolenga.
2. Moyo wako ukiwa umetulia mbele ya Mungu, kula, kunywa, na kufurahia maneno ya Mungu.
3. Yafanye mazoea ya kawaida kutafakari na kuzingatia maneno ya Mungu na kufikiri kazi ya Mungu na moyo wako.