46. Maana halisi ya "Uasi dhidi ya Mungu"
Zhang Jun Mji wa Shenyang, Mkoa wa Liaoning
Katika siku za nyuma, niliamini kuwa "uasi dhidi ya Mungu" ilimaanisha kumsaliti Mungu, kuacha kanisa, au kuutelekeza wajibu wa mtu. Nilidhani tabia hizi hufanyiza uasi. Kwa hiyo, wakati wowote niliposikia kuhusu watu wakihusika katika tabia hizo, ningejikumbusha kwamba sipaswi kuasi dhidi ya Mungu kama walivyofanya. Aidha, nilikuwa mwangalifu katika jitihada zangu zote na nilishikilia kazi zote nilizopewa na kanisa. Sikurudi nyuma kutoka kwa wajibu wangu wakati niliposhughulikiwa na kupogolewa wala kuondoka kutoka kanisani nilipojaribiwa, bila kujali shida. Kwa hiyo, niliamini kwamba sikuwahi kuasi dhidi ya Mungu kamwe. Nilihisi kuwa nilikuwa nimepata hadhi fulani tayari na nilikuwa na hakika kwamba ningemfuata Mungu mpaka mwisho na hatimaye kufanikisha wokovu.