Jumatatu, 21 Mei 2018

Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu


Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu



Mwenyezi Mungu alisema, Kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni mojawapo ya hatua muhimu sana za kuingia katika maneno ya Mungu, na ni funzo ambalo watu wote sasa wana haja ya haraka kuingia ndani. Njia za kuingia za kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni:
1. Ondoa moyo wako kwa mambo ya nje, tulia mbele ya Mungu, na uombe Mungu kwa moyo uliolenga.
2. Moyo wako ukiwa umetulia mbele ya Mungu, kula, kunywa, na kufurahia maneno ya Mungu.
3. Yafanye mazoea ya kawaida kutafakari na kuzingatia maneno ya Mungu na kufikiri kazi ya Mungu na moyo wako.

Jumapili, 20 Mei 2018

New Swahili Gospel Movie "Jina la Mungu Limebadilika?!" | Kufunua Siri ya Jina la Mungu

New Swahili Gospel Movie "Jina la Mungu Limebadilika?!" | Kufunua Siri ya Jina la Mungu

Jina lake ni Wang Hua, na ni mhubiri wa kanisa la nyumbani Kusini mwa Uchina. Baada ya kuanza kumwamini Bwana, alipata kwenye Biblia kuwa Mungu aliitwa Yehova katika Agano la Kale, na aliitwa Yesu katika Agano Jipya. Ni kwa nini Mungu ana majina tofauti? Wang Hua alishangazwa sana na hili. Alijaribu kutafuta jibu katika Biblia, lakini akakosa kuelewa fumbo hilo... Lakini alikuwa na imani thabiti kuwa hakuna jina lingine chini ya mbingu lililopewa wanadamu, hivyo Yesu pekee ndiye Mwokozi, na kuwa muradi tushikilie jina la Yesu, bila shaka tutanyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Hata hivyo, siku moja Wang Hua alisikia habari za kushtusha: jina la Mungu limebadilika! Baada ya hapo, moyo wake haungetulia tena …

Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Maono ya Kazi ya Mungu (3)


Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu.

Jumamosi, 19 Mei 2018

Swahili Christian Video "Mtoto, Rudi Nyumbani" | Hakuna Wokovu Ila Kupitia Kwa Bwana


Swahili Christian Video "Mtoto, Rudi Nyumbani" | Hakuna Wokovu Ila Kupitia Kwa Bwana

Li Xinguang ni mwanafunzi wa shule ya upili ya ngazi ya juu. Alikuwa mvulana mwenye busara na mwenye tabia nzuri tangu alipokuwa mdogo. Wazazi wake na walimu wake walimpenda sana. Alipokuwa akienda katika shule ya kati, alipumbazwa na michezo ya kompyuta ya mtandaoni. Angekosa kwenda darasani mara kwa mara ili aende kwenye chumba cha mtandao. Wazazi wake walifanya kila juhudi kumsaidia kuyaondoa mazoea yake ya michezo.

Sura ya 21. Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu


Sura ya 21. Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu


Mwenyezi Mungu alisema, Kama huna uzoefu wa kitu, basi wewe hakika hutajua jinsi ya kukisimamia na utakisimamia vibaya. Hata kama unakisimamia, na ufikiri: “Mimi nimeeleza kiasi haya yote na nikasema mengi kulihusu. Wao pia wamelisikiza mara nyingi. Nimeongea sana kulihusu. Yote ambayo nimeshiriki kuhusu tatizo hili kimsingi ni kweli, sivyo?” lakini kwa kweli, yote tu ni mafundisho, na wewe unatumia mafundisho kutatua tatizo. Mbona unasema ni mafundisho? Kila neno unalosema ni sahihi, lakini kile unachosema hakijaelekezwa kwa tatizo na hakifikii kiini cha tatizo hili–ambapo tatizo hili lipo, shida yake ni nini, kwa nini hawa watu wanaweza kufanya mambo kama hayo au ni hali gani imejitokeza ndani yao.

Ijumaa, 18 Mei 2018

Latest Gospel Movie Swahili "Siri ya Utauwa: Mfuatano" | Ufunuo Mpya Zaidi wa Roho Mtakatifu

Latest Gospel Movie Swahili "Siri ya Utauwa: Mfuatano" | Ufunuo Mpya Zaidi wa Roho Mtakatifu

Lin Bo'en ni mhubiri mzee ambaye amemwani Bwana kwa miongo mingi. Tangu alipomkubali Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, alihukumiwa, akatengwa, na akafukuzwa kutoka kwa jumuiya ya kidini na wachungaji na wazee wa kanisa, nguvu zinazompinga Kristo. Lakini ingawa Lin Bo’en alishambuliwa, akahukumiwa na kusingiziwa, hakusita kwa woga. Badala yake, imani yake ikawa thabiti zaidi kuliko ilivyowahi kuwa, na hili lilimwongoza kufahamu hatimaye kwamba wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini walikuwa wakiigiza kwa udanganyifu sura adilifu. Wakati huo huo, alikuja kujua kwamba Kristo pekee ndiye ukweli, njia, na uzima, na Kristo pekee ndiye Anaweza kumwokoa na kumtakasa na kumkamilisha mwanadamu.