Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumbukumbu-za Maongezi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumbukumbu-za Maongezi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 19 Mei 2018

Sura ya 21. Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu

Sura ya 21. Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kama huna uzoefu wa kitu, basi wewe hakika hutajua jinsi ya kukisimamia na utakisimamia vibaya. Hata kama unakisimamia, na ufikiri: “Mimi nimeeleza kiasi haya yote na nikasema mengi kulihusu. Wao pia wamelisikiza mara nyingi. Nimeongea sana kulihusu. Yote ambayo nimeshiriki kuhusu tatizo hili kimsingi ni kweli, sivyo?” lakini kwa kweli, yote tu ni mafundisho, na wewe unatumia mafundisho kutatua tatizo. Mbona unasema ni mafundisho? Kila neno unalosema ni sahihi, lakini kile unachosema hakijaelekezwa kwa tatizo na hakifikii kiini cha tatizo hili–ambapo tatizo hili lipo, shida yake ni nini, kwa nini hawa watu wanaweza kufanya mambo kama hayo au ni hali gani imejitokeza ndani yao.