10. Usitafute Mbinu Mpya Unapomtumikia Mungu
Heyi Mji wa Zhuanghe, Mkoa wa Liaoning
Nilikuwa nimepandishwa cheo tu kuchukua jukumu la kiongozi wa kanisa. Lakini baada ya kipindi cha kazi ngumu, sio tu kuwa kazi ya kiinjili ilikuwa bila uhai kiasi, lakini ndugu zangu wa kiume na wa kike katika timu ya kiinjili walikuwa pia wakiishi katika hali hasi na ya udhaifu. Nikiwa nimekabiliwa na hali hii, sikuweza tena kudhibiti hisia zangu. Ni vipi tena ningeweza kuiamsha kazi ya kiinjili? Baada ya kupiga ubongo wangu, hatimaye nilifikiria suluhisho zuri: Kama ningefanya sherehe ya kila mwezi kwa timu ya kiinjili na kuwachagua watu waliojipambanua na wahubiri wa kielelezo, yeyote ambaye angeshinda roho zaidi kwa ajili ya Mungu angepewa thawabu, na yeyote ambaye angeshinda roho chache angeonywa. Hili halingeisisimua shauku yao tu, lakini lingewainua ndugu wa kike na wa kiume waliokuwa hasi na dhaifu. Nilipofikiria hili, nilifurahishwa sana na hili "tendo langu la werevu". Niliwaza "Wakati huu kwa kweli nitamshangaza kila mtu."