Kanisa la Mwenyezi Mungu | 6. Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa
Ding Ning Mji wa Heze, Mkoa wa Shandong
Katika siku chache zilizopita, kanisa limepanga mabadiliko katika kazi yangu. Nilipopokea wajibu huu mpya, niliwaza, "Ninahitaji kuchukua fursa hii ya mwisho kuita mkutano na ndugu zangu wa kiume na wa kike, niongee nao wazi juu ya mambo, na niwaache na picha nzuri." Kwa hiyo, nilikutana na mashemasi kadhaa, na kufikia mwisho wa wakati wetu pamoja, nikasema, "Nimeulizwa kuondoka hapa na kuenda kwa kazi tofauti. Natumaini mtamkubali kiongozi ambaye anakuja kuchukua nafasi yangu na kufanya kazi pamoja naye kwa moyo mmoja na wazo moja." Mara tu waliposikia nikisema maneno haya, baadhi ya dada waliokuwepo walipauka, na tabasamu zikawatoka nyusoni. Baadhi yao walishika mikono yangu, baadhi yao walinikumbatia, na hali wakilia walisema, "Huwezi kutuacha! Huwezi kututupa kando na kupuuza mahitaji yetu! ... "Dada wa familia mwenyeji hasa hakuwa radhi kuniruhusu niende.
Aliniambia, "Ni vizuri sana kwamba uko hapa pamoja nasi. Wewe ni mtu ambaye anaweza kuvumilia shida, na wewe ni mzuri katika kushirikiana juu ya ukweli. Bila kujali ni wakati upi tulikuhitaji, daima ulikuwa hapo kutusaidia kwa uvumilivu. Kama ukienda, tutafanya nini? ... "Kwa kuona kusita kwao kutengana nami, moyo wangu ulijaa furaha na ridhaa. Niliwafariji kwa maneno haya: "Mtegemeeni Mungu. Nitakapoweza, nitarudi na kuwatembelea…."
Lakini baada ya hapo, kila wakati nilipotazama nyuma tukio hilo la kuachana na ndugu zangu wa kiume na kike, nilikuwa na wasiwasi moyoni mwangu. Nilijiuliza, "Je, maonyesho hayo ya huzuni ni yanavyotarajiwa kuwa? Kwa nini walitenda kana kwamba kuondoka kwangu kulikuwa kitu cha kutisha? Kwa nini kanisa lilitaka nibadili kazi kwa vyovyote vile?" Moyo wangu ulikuwa umefungwa katika wingu la shaka, na hivyo mara nyingi nilikuja mbele ya Mungu kutafuta majibu. Siku moja nilikuwa nikisoma "Mambo ya Kanuni Ambayo Yanapaswa Kueleweka kwa Kumtumikia Mungu" na nikaona kifungu hiki: "Wale ambao wangemtumikia Mungu ni lazima katika mambo yote wamwinue Mungu na kuwa mashahidi wa Mungu. Ni kwa njia hiyo tu wanavyoweza kufikia matunda ya kuwaongoza wengine kumjua Mungu. Na ni kwa kumwinua Mungu tu na kumshuhudia Yeye wanavyoweza kuwaleta wengine mbele ya Mungu. Hii ni moja ya kanuni za huduma kwa Mungu. Matunda ya msingi ya kazi ya Mungu ni hasa kazi ya kuwaleta watu kuijua kazi ya Mungu na hivyo kuja machoni Pake. Ikiwa wale walio katika vyeo vya uongozi hawamwinui Mungu na kuhudumu kama mashahidi wa Mungu, lakini badala yake wanajitokeza kwa maonyesho daima...,basi kwa kweli wanajiweka katika upinzani na Mungu. ... Kwa kweli wanashindana na Mungu kwa roho za watu. ... Kwa hiyo, ikiwa huduma ya watu si kumuinua Mungu na kushuhudia kwa Mungu, basi kwa kweli wanajionyesha wenyewe. Ingawa wanabeba bango la utumishi kwa Mungu, kwa kweli wanafanya kazi kwa ajili ya hadhi yao wenyewe; kwa kweli wanafanya kazi kwa ajili ya kuridhika kwa mwili. Kwa vyovyote hawamwinui Mungu au kushuhudia kwa Mungu katika kazi yao. Kama yeyote huihaini kanuni hii ya utumishi kwa Mungu, inathibitisha tu kwamba yeye humpinga Mungu "("Mambo ya Kanuni Ambayo Yanapaswa Kueleweka kwa Kumtumikia Mungu" katika Kumbukumbu za Ushirika na Mipango ya Kazi ya Kanisa I). Nilivyozidi kusoma, ndivyo moyo wangu ulivyozidi kutatizika. Nilivyozidi kusoma, ndivyo nilivyozidi kushtuka. Hisia yangu ya kujisuta ilizidishwa mara nyingi. Kutoka kwa mtazamo waliokuwa wamenionyesha ndugu zangu wa kiume na wa kike, niliweza kuona kazi yangu kweli haikuwa kuwaongoza ndugu zangu wa kiume na wa kike mbele ya Mungu, lakini badala yake kuwaongoza mbele yangu. Sasa sikuweza kujizuia kupima tena matukio mengi wakati wa muda niliotumia na ndugu zangu wa kiume na wa kike. Mara kwa mara nilikuwa nimemwambia dada wa familia mwenyeji, "Angalia jinsi mlivyo na bahati nyote. Familia yako nzima ni waumini. Ninapokuwa nyumbani, mume wangu hunitesa mchana kutwa. Kama hanigongi, ananilaani. Nimetekeleza wajibu wangu kwa kadri linalowezekana, na angalia kiasi cha uchungu nilichovumilia kwa sababu ya imani yangu kwa Mungu." Wakati ndugu zangu wa kiume na wa kike walipokabiliwa na shida, sikuwasiliana nao mapenzi ya Mungu; sikufanya kazi kama shahidi kwa kazi ya Mungu na upendo wa Mungu. Badala yake, mimi daima niliuweka mwili kwanza na nilijaribu kuwafanya watu kufikiri kuwa mimi ni mkarimu na mwenye huruma. Wakati wowote nilipomwona ndugu wa kiume au wa kike akifanya kitu kilichokuwa kinyume na kanuni, niliogopa kumkosea, hivyo singesaidia au kutoa mwongozo, daima nikijaribu kulinda uhusiano kati ya watu. Katika kila kitu nilichokifanya, kile nilichokijali zaidi kilikuwa ni cheo changu na picha yangu katika mioyo ya watu. ... Kusudi langu kuu lilikuwa daima kupata huruma na upendezwaji kwa wengine; hii ikawa ridhaa yangu kubwa sana. Hili kwa hakika linafichua kwamba nilikuwa ninajiinua mwenyewe, nikijitumikia mwenyewe kama shahidi. Yote niliyoyatenda kwa kweli yalikuwa ni upinzani kwa Mungu. Nilifikiria juu ya maneno ya Mungu, ambayo yanasema, “Nafanya kazi miongoni mwenu sasa lakini bado mko hivi. Kama siku moja hakutakuwa na mtu wa kuwalinda na kuwaangalia, si nyote mtakuwa wafalme wa kilima?[a] Kwa wakati huo, nani atavisafisha vitu tena na kuondoa uchafu mnaposababisha janga kubwa?” (“Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu tena yalinileta kwa ufahamu wa jinsi huduma yangu kwa Mungu kwa kweli ilikuwa ni kujishuhudia mwenyewe na kujiinua na yalinisaidia kuona matokeo mabaya ya tabia hii. Maneno ya Mungu yalinisaidia kuona kwamba asili yangu, kama ile ya malaika mkuu, ingeniongoza kuwa gaidi dhalimu, na kwamba ningesababisha maangamizi makubwa. Nilifikiria kuhusu jinsi huduma yangu kwa Mungu haikutimizwa kulingana na kanuni sahihi za huduma; haikuwa ikimwinua Mungu na kumshuhudia Mungu, si kufanya wajibu wangu. Badala yake, siku zangu zilitumiwa kujionyeshwa mwenyewe, kujishuhudia mwenyewe, kuwavuta ndugu zangu wa kiume na wa kike mbele yangu. Je, si aina hii ya huduma ni ya kudharauliwa? Je, si hii ni "huduma" ya mpinga Kristo tu? Kama haikuwa uvumilivu wa Mungu na rehema, ningekuwa tayari nimelaaniwa na Mungu na kuangushwa.
Wakati huo, nilitetemeka kwa uoga na aibu; hisia ya deni kubwa nililowiwa ikifurikisha moyo wangu, na nikasujudia chini, nikalia kwa uchungu na kumsihi Mungu: "Ewe Mungu! Kama haingekuwa ufunuo Wako na kupata nuru, sijui ni kwa kina gani ningeanguka. Kwa hakika ninakuwia Wewe zaidi ya ninavyoweza kulipa. Asante kwa wokovu Unaonipa! Asante kwa kunisaidia kuona nafsi mbaya na yenye kustahili dharau katika vina vya roho yangu. Asante kwa kunionyesha kwamba huduma yangu Kwako ilikuwa kwa kweli ni upinzani Kwako. Kama ningehukumiwa na matendo yangu, sistahili chochote isipokuwa laana Yako, lakini Hujanitendea kulingana na makosa yangu. Badala yake Umefungua macho yangu, Umeniongoza, na kunipa fursa ya kutubu na kuanza upya. Ewe, Mungu, niko radhi kuchukua uzoefu huu kama somo kuubeba kwa maisha yangu yote. Naomba kuadibu Kwako na hukumu yako ziende nami daima, na ninaomba zinisaidie mapema kutupa nafsi ya zamani ya Shetani na zinisaidie kweli kuwa mtumishi wa Mungu wa kustahi sana ili nipate kulipa deni kubwa ninalowiwa."
Tanbihi:
a. Msemo wa Kichina, maana halisi ambayo ni “magaidi wanaoimiliki milima na kujitangaza kama wafalme.”
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo Juzuu ya 1
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni