Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Vita-Baina-ya-Haki-na-Uovu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Vita-Baina-ya-Haki-na-Uovu. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 7 Julai 2018

Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu, Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

Ndugu wawili wa kawaida, Beijing
Agosti 15, 2012
Julai 21, mwaka wa 2012 ilikuwa siku isiyosahaulika sana kwangu, pamoja na kuwa siku muhimu zaidi ya maisha yangu.
Siku hiyo, mvua kubwa ilikuwa ikinyesha katika Wilaya ya Fangshan jijini Beijing—ilikuwa kubwa kuliko yoyote iliyowahi kuonekana pale katika miaka sitini na mmoja. Muda mfupi baada ya saa 4 jioni, nilitoka nje mtaani ili kuangalia na nikaona kuwa maji yalikuwa kila mahali.