Jumapili, 7 Aprili 2019

Wimbo wa Injili | 1. Wimbo Wa Ufalme (I) Ufalme Umeshuka Duniani

Wimbo wa Injili | 1. Wimbo Wa Ufalme (I) Ufalme Umeshuka Duniani

Ufalme wa Mungu umekuja duniani; Mtu wa Mungu ameshiba na ni tajiri.
Nani anaweza kusimama imara na asifurahie? Nani anaweza kusimama imara na asicheze?
Ee Zayuni, inua bango lako la ushindi ili kusheherekea kwa aijili Mungu.
Imba wimbo wako wa ushindi kueneza jina Lake takatifu duniani.
Watu wasiohesabika wanamsifu Mungu kwa furaha, sauti zisizohesabika zinainua jina Lake.
Wanatazama matendo Yake mazuri. Sasa ufalme Wake duniani umekuja.
Vitu vyote duniani, jisafisheni; njooni mtoe sadaka kwa Mungu.
Nyota, rudini katika kiota chenu angani, onyesheni nguvu za Mungu juu mbinguni.
Duniani sauti zinainuka na kuimba,
zikitoa upendo usiokoma na uchaji usio na mwisho kwa Mungu.
Yeye anazisikiliza kwa makini.
Watu wasiohesabika wanamsifu Mungu kwa furaha, sauti zisizohesabika zinainua jina Lake.
Wanatazama matendo Yake mazuri. Sasa ufalme Wake duniani umekuja.
Katika siku hiyo vitu vyote vinafufuliwa, Mungu binafsi Anakuja duniani.
Maua yanachanua kwa furaha, ndege wanaimba na vitu vyote vinafurahi.
Tazama ufalme wa Shetani ukianguka wakati saluti ya ufalme wa Mungu inaposikika,
ukikanyagwa, usisimame tena kamwe, ukizamishwa chini ya wimbo wa sifa.
Watu wasiohesabika wanamsifu Mungu kwa furaha (kwa furaha),
sauti zisizohesabika zinaliinua jina Lake (jina Lake).
Wanatazama matendo Yake mazuri. Sasa ufalme Wake duniani umekuja.
Nani duniani anathubutu kusimama na kupinga?
Mungu anaposimama kati ya wanadamu,
Ameleta ghadhabu Yake na majanga yote duniani.
Dunia imekuwa ufalme wa Mungu.
Mawingu yanabingirika na kusukasuka angani, maziwa na mito yanakoroga wimbo wa furaha.
Wanyama wanaopumzika wanatoka katika mapango yao, na mwanadamu anaamshwa na Mungu kutoka kwa ndoto zao.
Sasa hiyo siku iliyongojewa kwa hamu imefika na wote wanamheshimu Mungu kwa nyimbo zao,
nyimbo za kupendeza sana.
Watu wasiohesabika wanamsifu Mungu kwa furaha (kwa furaha),
sauti zisizohesabika zinaliinua jina Lake (jina Lake).
Wanatazama matendo Yake mazuri. Sasa ufalme Wake duniani umekuja.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Tufuate: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni