Jumamosi, 16 Februari 2019

Nyimbo za kusifu | 63. Upendo wa Kweli Miongoni mwa Binadamu

Nyimbo za kusifu | 63. Upendo wa Kweli Miongoni mwa Binadamu

I
Unaonyesha ukweli na kumpa mwanadamu njia ya uzima wa milele.
Unavumilia maumivu ya kukataliwa na kushiriki katika taabu za mwanadamu.
Unatembea kati ya makanisa na kuwaongoza wateule Wako.
Unaishi pamoja na mwanadamu na kuteseka pamoja naye.
Umeumia katika maumivu kwa miongo.  Unamwaga upendo Wako wote kuushinda moyo wa mwanadamu.
Maneno Yako makali yamejaa upendo wa kweli.
Unahukumu na kumtakasa mwanadamu, kumjaribu na kumsafisha.
Unatamka maneno mapya kila siku, yote ili kumkamilisha mwanadamu.
Napitia hukumu Yako na naondolewa upotovu wote.
Napitia upendo Wako na moyo wangu unakugeukia Wewe.
II
Nimekuamini kwa miaka mingi lakini sikukujua kamwe.
Nikiwa nimejazwa mawazo yasiyofaa, nilijua tu jinsi ya kuomba neema.
Nilikubali kazi Yako, lakini sikukupenda kamwe.
Kwa kweli nilipoteza akili zote na sikufaa kuitwa binadamu.
Ulinionyesha huruma na upole na kufanya kila Uliloweza kuniokoa.
Hukumu Yako na usafishaji ni upendo Wako.
Kupitia kupata uzoefu wa hukumu Yako, najua haki Yako.
Tabia yangu imebadilika na upendo wangu Kwako ni safi zaidi.
Ninapoona uzuri Wako, moyo wangu unakuwa Wako.
Ninajinyenyekeza kwa mipango Yako bila majuto au malalamiko.
Nakupenda na kushuhudia, nami nitakuwa mwaminifu Kwako maisha yangu yote.

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni