Jumamosi, 23 Februari 2019

Nyimbo za kuabudu | 66. Mwenyezi Mungu Ametushinda

I
Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo!
Unaonyesha ukweli na kutushinda.
Maneno Yako yanatufunua bila huruma na kutuhukumu kwa haki,
ili kwamba tujue ukweli wa upotovu wetu.
Kwamba sasa tunaweza kujichukia na kumtelekeza Shetani
ni kwa wokovu Wako kabisa. Tunakupa shukurani.
II
Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo!
Tumepotoshwa sana na Shetani.
Tunaweka mizizi yetu katika upotovu na kukua katika dhambi,
sisi ni uzao wa Shetani na tunaishi kwa kudhihirisha mfano wa Shetani.
Tukiwa tumejawa tabia za shetani, tumepoteza dhamiri na mantiki yetu.
Tunakuamini na ilhali hatujui kwamba tunakudanganya na kukuasi.
III
Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo!
Unaonyesha ukweli na kufanyiza kundi la washindi.
Hukumu Yako ni nuru kuu inayoangazia ulimwengu wote,
na ibilisi na nguvu za mpinga Kristo zinafichua asili yao ya kweli.
Unamshinda Shetani kabisa na kupata utukufu wote.
Tutakufuata na kushuhudia Kwako milele, waaminifu hadi mwisho!
IV
Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo!
Hukumu Yako ni ya haki na takatifu.
Tunaona jinsi haki Yako na utakatifu Wako vinavyopendeza.
Baada ya kutambua hekima na uweza Wako, tunakucha na kukutii.
Ni hukumu na kuadibu Kwako ambavyo vinatutakasa na kutuokoa.
Tunapatwa na Wewe tabia zetu zinapobadilika, na tutakupenda na kukuabudu milele.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni