Jumanne, 4 Desemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" (Official Video)


Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" (Official Video)

    Mwenyezi Mungu anasema, "Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno."

    Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni