II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu
1. Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu.
Maneno Husika ya Mwenyezi Mungu:
Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme.
Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kutoa wazi hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufunua ubovu wa Shetani. Aidha, ni kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kufanya tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, ukuu na udogo, wazi kama mchana. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wanaweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Muumba—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Naweza kuwapa mambo kwa ajili ya raha; na wapate kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na kwamba Shetani ni mmoja tu wa viumbe Vyangu, ambaye baadaye alinigeuka. Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita umegawanywa katika hatua tatu ili kufikia matokeo yafuatayo: Kuruhusu viumbe Wangu wawe mashahidi Wangu, kujua mapenzi Yangu, na waone kwamba Mimi Ndimi ukweli.
kutoka kwa "Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu.
…………
Wakati ambapo usimamizi mzima wa Mungu utakaribia kufika mwisho, Mungu ataweka vitu vyote kulingana na aina. Mwanadamu aliumbwa kwa mikono ya Muumba, na mwishowe lazima kabisa amrudishe mwanadamu chini ya utawala Wake; huu ndio mwisho wa hatua tatu za kazi. …
… Hatua tatu za kazi zitakapofikia tamati, patafanyika kundi la watu wanaomshuhudia Mungu, kundi la wale wanaomjua Mungu. Watu hawa wote watamjua Mungu na wataweza kuonyesha ukweli kwa matendo. Watakuwa na ubinadamu na hisia, na wote watajua hatua tatu za kazi ya wokovu ya Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo itatekelezwa mwishowe, na watu hawa ndio dhihirisho la kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi, na ndio ushuhuda wenye nguvu zaidi kwa kushindwa kwa Shetani.
kutoka kwa "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Leo kwanza kabisa tutafanya muhtasari wa fikira, mawazo, na kila hatua ya Mungu tangu Alipomuumba binadamu, na kuangalia ni kazi gani Alitekeleza kuanzia uumbaji wa ulimwengu hadi mwanzo rasmi wa Enzi ya Neema. Tunaweza basi kugundua ni fikira na mawazo yapi ya Mungu ambayo hayajulikani kwa binadamu, na kuanzia hapo tunaweza kuweka wazi mpangilio wa mpango wa usimamizi wa Mungu na kuelewa kwa kina muktadha ambao kwao Mungu alianzisha kazi Yake ya usimamizi, chanzo chake na mchakato wake wa maendeleo, na pia kuelewa kwa undani ni matokeo yapi Anayotaka kutoka katika kazi Yake ya usimamizi—yaani, kiini na kusudio la kazi Yake ya usimamizi. Kuelewa mambo haya tunahitaji kurudi hadi ule wakati wa kitambo, mtulivu na kimya wakati ambapo hakukuwa na binadamu …
Wakati Mungu alipoinuka kutoka kitandani Mwake, fikira ya kwanza Aliyokuwa nayo ilikuwa hii: kumuumba binadamu hai, halisia, binadamu anayeishi—mtu wa kuishi naye na kuwa mwenzake Yeye wa kila mara. Mtu huyu angemsikiliza Yeye, na Mungu angempa siri Zake na kuongea na yeye. Kisha, kwa mara ya kwanza Mungu aliuchukua udongo kwenye mkono na kuutumia kumuumba mtu wa kwanza kabisa aliye hai ambaye Alikuwa amemfikiria, na kisha Akakipa kiumbe hiki hai jina—Adamu. Punde Mungu alipompata mtu huyu aliye hai na anayepumua, Alihisi vipi? Kwa mara ya kwanza, Alihisi furaha ya kuwa na mpendwa, na mwandani. Aliweza kuhisi pia kwa mara ya kwanza uwajibikaji wa kuwa baba pamoja na kujali kunakoandamana na hisia hizo. Mtu huyu aliye hai na anayepumua alimletea Mungu furaha na shangwe; Alihisi Amefarijika kwa mara ya kwanza. Hili lilikuwa jambo la kwanza ambalo Mungu aliwahi kufanya ambalo halikukamilishwa kwa fikira Zake au hata matamshi Yake, lakini lilifanywa kwa mikono Yake miwili. Wakati kiumbe aina hii—mtu aliye hai na anayepumua—kiliposimama mbele ya Mungu, kilichoumbwa kwa nyama na damu, kilicho na mwili na umbo, na kilichoweza kuongea na Mungu, Alihisi aina ya shangwe ambayo Hakuwa amewahi kuhisi kabla. Kwa kweli alihisi kwamba uwajibikaji Wake na kiumbe hiki hai haukuwa na uhusiano tu katika moyo Wake, lakini kila jambo dogo alilofanya pia liliugusa moyo Wake na likaupa moyo Wake furaha. Kwa hivyo wakati kiumbe hiki hai kiliposimama mbele ya Mungu, ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuwahi kufikiria kuwapata watu wengi zaidi kama hawa. Huu ndio uliyokuwa msururu wa matukio ulioanza kwa fikira hii ya kwanza ambayo Mungu alikuwa nayo. Kwa Mungu, matukio haya yote yalikuwa yakifanyika kwa mara ya kwanza, lakini katika matukio haya ya kwanza, haijalishi vile Alivyohisi wakati huo—furaha, uwajibikaji, kujali—hakukuwa na yeyote yule wa kushiriki furaha hii na Yeye. Kuanzia wakati huo, Mungu alihisi kwa kweli upweke na huzuni ambao Hakuwahi kuwa nao mbeleni. Alihisi kwamba binadamu wasingekubali au kuelewa mapenzi Yake na kujali Kwake, au nia Zake kwa mwanadamu, hivyo basi Alihisi huzuni na maumivu katika moyo Wake. Ingawa Alikuwa amefanya mambo haya kwa binadamu, binadamu hakuwa na habari na wala hakuelewa. Mbali na furaha, shangwe na hali njema ambayo binadamu alimletea pia viliandamana kwa haraka na hisia Zake za kwanza za huzuni na upweke. Hizi ndizo zilizokuwa fikira na hisia za Mungu wakati huo. Wakati Mungu alipokuwa akifanya mambo haya yote, katika moyo Wake Alitoka katika furaha Akaingia katika huzuni na kutoka katika huzuni Akaingia katika maumivu, vyote vikiwa vimechanganyika na wasiwasi. Kile Alichotaka kufanya tu kilikuwa kuharakisha kumruhusu mtu huyu, kizazi hiki cha binadamu kujua ni nini kilichokuwa moyoni Mwake na kuelewa nia Zake haraka iwezekanavyo. Kisha, wangekuwa wafuasi Wake na kupatana na Yeye. Wasingemsikiliza tena Mungu akiongea na kubakia kimya; wasingeendelea kutojua namna ya kujiunga na Mungu katika kazi Yake, na zaidi ya yote, wasingekuwa tena watu wasiojali na kuelewa mahitaji ya Mungu. Mambo haya ya kwanza ambayo Mungu alikamilisha ni yenye maana sana na yanashikilia thamani nyingi kwa minajili ya mpango Wake wa usimamizi na ule wa binadamu leo.
Baada ya kuviumba viumbe vyote na binadamu, Mungu hakupumzika. Asingesubiri kuutekeleza usimamizi Wake wala Asingeweza kusubiri kuwapata watu Aliowapenda mno miongoni mwa wanadamu.
…………
… Mungu anaona tukio hili la usimamizi wa mwanadamu, wa kuwaokoa wanadamu, kama muhimu sana kuliko chochote kingine. Huyafanya mambo haya yote si kwa kutumia akili Zake tu, wala si kwa kutumia matamshi Yake tu, na vilevile Yeye hafanyi hivi hususan kwa juujuu tu—Yeye huyafanya mambo haya yote kwa mpango, kwa viwango, na kwa mapenzi Yake. Ni wazi kwamba kazi hii ya kumwokoa mwanadamu imeshikilia umuhimu mkubwa kwa Mungu na hata binadamu. Haijalishi kazi ilivyo ngumu, haijalishi ukubwa wa changamoto zilivyo, haijalishi ni vipi ambavyo binadamu ni wanyonge, au ni vipi mwanadamu amekuwa mwasi wa kweli, hakuna chochote kati ya haya ambacho ni kigumu kwa Mungu. Mungu hujibidiisha Mwenyewe, Akitumia jitihada Zake na kusimamia kazi ambayo Yeye Mwenyewe Anataka kutekeleza. Yeye pia Anapanga kila kitu na kuwatawala watu wote na kazi ambayo Anataka kukamilisha—hakuna chochote kati ya haya ambacho kimefanywa awali. Ndiyo mara ya kwanza Mungu ametumia mbinu hizi na kulipa gharama kubwa kwa minajili ya mradi huu mkubwa wa kusimamia na kumwokoa mwanadamu. Huku Mungu akiwa Anatekeleza kazi hii, hatua kwa hatua Anawaonyesha binadamu bila kuficha bidii Yake, kile Alicho nacho na kile Alicho, hekima na uweza, na kila dhana ya tabia Yake. Anafichua bila kuacha chochote haya yote kwa mwanadamu kidogo kidogo, Akifichua na kuonyesha mambo haya kwa namna ambayo Hajawahi kufanya awali. Kwa hivyo, katika ulimwengu mzima, mbali na watu ambao Mungu analenga kuwasimamia na kuwaokoa, hakujawahi kuwepo na viumbe vyovyote vilivyo karibu na Mungu, ambavyo vinao uhusiano wa karibu sana na Yeye. Katika moyo Wake, yule mwanadamu Anayetaka kumsimamia na kumwokoa ndiye muhimu zaidi, na Anamthamini mwanadamu huyu zaidi ya kitu kingine chochote; hata ingawa Amelipia gharama ya juu na ingawa Anaumizwa na kutosikilizwa bila kukoma na wao, Hakati tamaa na Anaendelea bila kuchoka katika kazi Yake bila ya malalamiko au majuto. Hii ni kwa sababu Anajua kwamba hivi karibuni au baadaye, binadamu siku moja wataitikia mwito Wake na kuguswa na maneno Yake, kutambua kwamba Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na kurudi upande Wake …
kutoka kwa "Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III" katika Neno Laonekana katika Mwili
Huu ni mfano wa usimamizi wa Mungu: kuwakabidhi wanadamu kwa Shetani—wanadamu ambao hawajui kile Mungu Alicho, Muumba ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na ni kwa nini inafaa kujitoa kwa Mungu—na kutoa utawala huru kwa uovu wa Shetani. Hatua baada ya hatua, Mungu Anamtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani, hadi mwanadamu amwabudu Mungu kikamilifu na kumkataa Shetani. Huu ndio usimamizi wa Mungu. Hili linasikika kama hadithi ya visasili na hii ni kwa sababu hawana fununu kuhusu yaliyomtokea mwanadamu katika maelfu ya miaka iliyopita, hata hawajui ni hadithi ngapi ambazo zimetokea katika huu ulimwengu. Na zaidi ya hayo, hii ni kwa sababu hawawezi kufahamu kinachostaajabisha sana, dunia inayoibua hofu zaidi ambayo iko zaidi ya dunia yakinifu, lakini ambayo macho yao ya mwili yanawazuia kuiona. Inasikika ya kutofahamika kwa mwanadamu. Na hii ni kwa sababu mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake. Hawa wanadamu wamepotoshwa na Shetani, lakini hawamwoni Shetani kama baba yao: hutambua uso usiopendeza wa Shetani, na kuukataa, na kuja mbele Zake Mungu na kukubali hukumu na kuadibu Kwake. Hujua kisichopendeza na jinsi kinavyotofautiana na kile kilicho kitakatifu, na hutambua ukubwa wa Mungu na uovu wa Shetani. Wanadamu kama hawa hawatamfanyia Shetani kazi tena, au kumwabudu Shetani, au kumsetiri Shetani. Hii ni kwa sababu wao ni kikundi cha watu ambao wamemilikiwa na Mungu. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuwasimamia wanadamu. …
…………
Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado Anafanya Kazi bila kuchoka na Anapania kuikamilisha. Haijalishi ni kwa kiasi gani watu wanaelewa usimamizi wa Mungu, manufaa na usaidizi wa Kazi inayofanywa na Mungu unaweza kukubalika na kila mtu. Labda, leo, hujahisi upendo wowote au maisha yaliyowezeshwa na Mungu, lakini bora tu humwachi Mungu, na hupotezi matumaini yako ya kutafuta ukweli, basi kutakuwa na siku ambapo tabasamu la Mungu litafichuliwa kwako. Kwa kuwa dhumuni la kazi ya usimamizi wa Mungu ni kuwatoa wanadamu anayemilikiwa na Shetani, sio kuwaacha wanadamu waliopotoshwa na Shetani na kumpinga Mungu.
kutoka kwa "Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Licha ya kile ambacho Mungu anafanya au mbinu ambazo Anatumia kufanya, licha ya gharama, au lengo Lake, kusudio la hatua Zake halibadiliki. Kusudio Lake ni kuweza kumshughulikia binadamu ili maneno ya Mungu yaingie ndani yake, mahitaji ya Mungu, na mapenzi ya Mungu kwa binadamu; kwa maneno mengine, ni kufanyia kazi huyu binadamu ili vyote ambavyo Mungu Anasadiki kuwa vizuri kulingana na hatua Zake, kumwezesha binadamu kuuelewa moyo wa Mungu na kufahamu kiini cha Mungu, na kumruhusu yeye kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, na hivyo basi kumruhusu binadamu kuweza kufikia kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—yote ambayo ni kipengele kimoja ya kusudio la Mungu katika kila kitu Anachofanya. Kipengele kingine ni kwamba, kwa sababu Shetani ndiye foili[a] na chombo cha huduma katika kazi ya Mungu, mara nyingi binadamu hukabidhiwa Shetani; hizi ndizo mbinu ambazo Mungu hutumia ili kuwaruhusu watu kuweza kuona maovu, ubaya, kudharaulika kwa Shetani katikati ya majaribio na mashambulizi ya Shetani na hivyo basi kuwasababisha watu kumchukia Shetani na kuweza kutambua kile ambacho ni kibaya. Mchakato huu unawaruhusu kwa utaratibu kuanza kuwa huru dhidi ya udhibiti wa Shetani, na dhidi ya mashtaka, uingiliaji kati, na mashambulizi ya Shetani—mpaka, kwa sababu ya maneno ya Mungu, maarifa yao na utiifu wao kwa Mungu, na imani yao kwa Mungu na kuweza kwao kumcha Mungu, wanashinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani na kushinda dhidi ya mashtaka ya Shetani; hapo tu ndipo watakapokuwa wamekombolewa kabisa dhidi ya utawala wa Shetani. Ukombozi wa watu unamaanisha kwamba Shetani ameshindwa, unamaanisha kwamba wao si tena chakula kwenye kinywa cha Shetani—kwamba badala ya kuwameza wao, shetani amewaachilia. Hii ni kwa sababu watu kama hao ni wanyofu, kwa sababu wanayo imani, utiifu na wanamcha Mungu, na kwa sababu wako huru kabisa dhidi ya Shetani. Wamemleta Shetani aibu, wamemfanya kuonekana mjinga, na wamemshinda kabisa Shetani. Imani yao katika kumfuata Mungu, na utiifu na kumcha Mungu kunamshinda Shetani, na kumfanya Shetani kukata tamaa kabisa na wao. Watu kama hawa ndio ambao Mungu amewapata kwa kweli, na hili ndilo lengo kuu la Mungu katika kumwokoa binadamu.
kutoka kwa "Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ulikuwa hata umeshaamuliwa kabla zaidi Nilipoiumba dunia. Watu hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho, na pia hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini Nilikuwa Nimeshamwambia adui Yangu lilipokuwa linapambana na Mimi kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kwa muda mrefu walikuwa watoto wa Shetani, na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake. ... Mwanadamu, akiwa amekanyagwa chini ya miguu ya Shetani kwa muda mrefu, amekuwa akitenda kwa mfano wa Shetani—hata kuwa na mwili wake. Wao ni ushahidi wa kuwa shahidi wa Shetani, wa uwazi. Aina hii ya Mwanadamu, uchafu kama huu, au watoto wa familia hii ya binadamu potovu, ni jinsi gani wangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu? Utukufu Wangu unatoka wapi? Shahidi Wangu yuko wapi? Adui ambaye anasimama dhidi Yangu na kuwapotosha wanadamu tayari amewachafua wanadamu, viumbe Wangu, waliojawa na utukufu Wangu na wanaoishi kulingana na Mimi. Ameiba utukufu Wangu, na kujaza binadamu na sumu iliyojawa na ubaya wa Shetani, na maji ya matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. … Nami Nitauchukua tena utukufu Wangu, ushuhuda Wangu miongoni mwa wanadamu na vyote vilivyokuwa mali Yangu, Niliyokuwa Nimewapa wanadamu hapo zamani—na kumshinda mwanadamu kikamilifu. Hata hivyo unapaswa kujua, wanadamu Nilioumba walikuwa watu watakatifu na wenye mfano Wangu na utukufu Wangu. Hapo awali hawakuwa wa Shetani, wala hawakukabiliwa na kukanyagwa kwake, bali walikuwa tu udhihirisho Wangu, walikuwa huru kutokana na sumu yake. Hivyo, Naliwajulisha wanadamu wote kwamba Ninataka tu kilichoumbwa na mkono Wangu, Wapendwa Wangu walio watakatifu ambao kamwe hawajawahi kumilikiwa na mwingine yoyote. Aidha, Mimi nitakuwa na furaha nao, na kuwaona kama utukufu Wangu. Hata hivyo, Ninachotaka sio mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani, ambaye ni wa Shetani leo, ambaye si kiumbe Changu tena. Kwa sababu Ninataka kuchukua tena utukufu Wangu katika dunia ya wanadamu, Nitashinda kikamilifu manusura waliobaki kwa wanadamu, kama ushahidi wa utukufu Wangu katika ushindi Wangu dhidi ya Shetani. Mimi huchukua tu ushahidi Wangu kama udhihirisho wa nafsi Yangu, kama kitu cha starehe Yangu. Hii ndiyo nia Yangu.
kutoka kwa "Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali. Ataanzisha ufalme Wake na kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu, kumaanisha kwamba Atarejesha mamlaka Yake duniani na kurejesha mamlaka Yake miongoni mwa viumbe vyote, Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani; hivyo Mungu hakuwa na njia ya kufanya kazi miongoni mwa viumbe Wake, na hakuweza zaidi kuwafanya viumbe Wake kumcha. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, na anapaswa kumwabudu Mungu, lakini mwanadamu kwa kweli alimpuuza Mungu na kumwabudu Shetani. Shetani alikuwa sanamu katika moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu alipoteza nafasi yake katika moyo wa mwanadamu, kusema kwamba Alipoteza maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu, na ili kurejesha maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu lazima arejeshe mfano wa awali wa mwanadamu na kumtoa mwanadamu tabia yake potovu. Ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwa Shetani, lazima Amwokoe mwanadamu kutoka kwa dhambi. Kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu polepole na kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, na mwishowe kurejesha ufalme Wake. Uangamizi wa mwisho wa wale wana wa kutotii pia utafanywa ili kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu vizuri zaidi na kuishi duniani vizuri zaidi. Kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu, Atamfanya mwanadamu amwabudu; kwa sababu Anataka kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, Atairejesha kabisa, na bila ughushi wowote. Kurudisha mamlaka Yake kunamaanisha kumfanya mwanadamu amwabudu na kumfanya mwanadamu amtii; kunamaanisha kwamba Atamfanya mwanadamu aishi kwa sababu Yake na kufanya adui zake waangamie kwa sababu ya mamlaka Yake; kunamaanisha kwamba Atafanya kila sehemu Yake kuendelea miongoni mwa binadamu na bila upinzani wowote wa mwanadamu. Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Binadamu Anaotaka ni wale wanaomwabudu, wale wanaomtii kabisa na wana utukufu Wake. Asipookoa binadamu wapotovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa binadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani. Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani utatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.
kutoka kwa "Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja" katika Neno Laonekana katika Mwili
Baada ya kutekeleza kazi Yake ya miaka 6,000 hadi leo, Mungu tayari amefichua vitendo Vyake vingi, kimsingi kumshinda Shetani na kuwaokoa binadamu wote. Anatumia fursa hii kuruhusu kila kitu mbinguni, kila kitu kilicho duniani, kila kitu kinachopatikana baharini pamoja na kila kifaa cha mwisho ambacho Mungu aliumba ulimwenguni kuweza kuona uweza wa Mungu na kushuhudia vitendo vyote vya Mungu. Huchukua fursa ya kumshinda Shetani ili kufichua vitendo Vyake kwa binadamu na kuwaruhusu watu kuweza kumsifu Yeye na kuitukuza hekima Yake kwa kumshinda Shetani. Kila kitu nchini, mbinguni na ndani ya bahari humletea utukufu, huusifu uweza Wake, kinasifu vitendo Vyake vyote na kutamka kwa sauti jina Lake takatifu. Hii ni ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani; hii ni ithibati ya Yeye kumshinda Shetani; na la muhimu zaidi, ni ithibati ya wokovu Wake kwa binadamu. Uumbaji wote wa Mungu humletea utukufu, humsifu Yeye kwa kumshinda adui Wake na kurudi kwa ushindi na humsifu Yeye kama Mfalme mkubwa mwenye ushindi. Kusudio lake si kumshinda Shetani tu, na hivyo basi kazi Yake imeendelea kwa miaka 6,000. Anatumia kushindwa kwa Shetani kuwaokoa binadamu; Anakutumia kushindwa kwa Shetani kufichua vitendo Vyake vyote na kufichua utukufu Wake wote. Atapata utukufu, na umati wote wa malaika utaweza pia kushuhudia utukufu Wake wote. Wajumbe walio mbinguni, wanadamu walio nchini na uumbaji wote ulio nchini utauona utukufu wa Muumba. Hii ndiyo kazi Aifanyayo. Viumbe vyake kule mbinguni na nchini wote utauona utukufu Wake, na atarudi kwa vifijo na nderemo baada ya kumshinda Shetani kabisa na kuruhusu binadamu kumsifu Yeye. Ataweza hivyo basi kutimiza kwa ufanisi vipengele hivi viwili. Mwishowe binadamu wote watashindwa na Yeye, na atamwondoa yeyote yule anayepinga au kuasi, hivi ni kusema, Atawaondoa wale wote wanaomilikiwa na Shetani.
kutoka kwa "Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama watu, wanaotembea na Mimi hadi leo, hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na ningali nafanya hivyo sasa. Ingawaje kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio lake linabakia lilelile. Kwa mfano, ingawaje nimejazwa na hukumu na adabu kwake binadamu, bado ni kwa ajili ya kumwokoa binadamu, ili niweze kueneza kwa njia bora zaidi injili Yangu na kupanua zaidi kazi Yangu miongoni mwa Mataifa baada ya binadamu kufanywa kuwa kamili. … Katika enzi ya mwisho, Nitafanya jina Langu litukuzwe miongoni mwa Mataifa, kufanya matendo Yangu kuonekana na mataifa mengine ili waniite Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kuyafanya maneno Yangu kutimika karibuni. Nitawafanya watu wote kujua kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote kuona kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya kutimizwa tu katika siku za mwisho.
kutoka kwa "Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia" katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni