Jumatatu, 12 Novemba 2018

2018 Gospel Music "Mungu Kuutawala Ulimwengu" (Swahili Subtitles)


2018 Gospel Music "Mungu Kuutawala Ulimwengu" (Swahili Subtitles)

    Ulimwengu ni mkubwa sana na usio na kikomo, na una nyota nyingi mno zisizohesabika katika mzunguko sahihi…. Unatamani kujua aliyeziumba sayari za juu za ulimwengu, na yule ambaye huamuru tao la mtupo angani? Dondoo ya kustaajabisha ya filamu ya Kikristo ya Mungu Kuutawala Ulimwengu itakuonyesha nguvu yenye uwezo ya Muumba.
    

Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo

Mwenyezi Mungu anasema, "Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum; Muumba tu ndiye anayemiliki aina hii ya mamlaka. Hivyo ni kusema kwamba, ni Muumba tu—Mungu Yule wa kipekee—ambaye anaonyeshwa kwa njia hii na ndiye aliye na hali halisi hii. Kwa nini tuzungumzie mamlaka ya Mungu? Mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanatofautiana vipi na mamlaka yaliyomo kwenye akili ya binadamu? Ni nini maalum sana kuyahusu? Na kunao umuhimu gani haswa kuyazungumzia hapa? Kila mmoja wenu lazima aweze kutilia maanani kwa umakinifu suala hili. Kwa watu wengi zaidi, “Mamlaka ya Mungu” ni fikira isiyoeleweka, ile ambayo ni ngumu sana kupata kuielewa, na mazungumzo yoyote kuihusu huenda yasizae matunda mazuri. Kwa hivyo lazima kutakuwepo na pengo kati ya maarifa ya mamlaka ya Mungu ambayo binadamu anaweza kumiliki, na hali halisi ya mamlaka ya Mungu. Ili kuliziba pengo hili, mtu lazima kwa utaratibu aweze kuelewa mamlaka ya Mungu kwa njia ya watu halisi-maishani, matukio, vitu au mambo muhimu yanayopatikana katika uwezo wa binadamu, na ambayo binadamu wanaweza kuyaelewa. Ingawaje kauli hii “Mamlaka ya Mungu” inaweza kuonekana kama isiyoeleweka, mamlaka ya Mungu kwa kweli si ya dhahania kamwe. Yeye yupo na binadamu kila dakika ya maisha yake, akimwongoza kila siku. Kwa hivyo, katika maisha ya kila siku ya kila mtu ataweza haswa kuona na kupitia dhana halisi ya mamlaka ya Mungu. Uhalisi huu ni ithibati tosha kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo, na unakuruhusu kabisa kutambua na kuelewa hoja hii kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya.
Mungu aliumba kila kitu, na baada ya kukiumba, Anao utawala juu ya kila kitu. Kuongezea kuwa na utawala juu ya kila kitu, pia anadhibiti kila kitu. Wazo hili linamaanisha nini “Mungu anadhibiti kila kitu”? Hali hii inaweza kuelezewa vipi? Hali hii inatumika vipi katika maisha halisi? Mnawezaje kuyajua mamlaka ya Mungu kwa kuelewa hoja hii kwamba “Mungu Anadhibiti kila kitu”? Kutoka kwenye kauli ile ile “Mungu anadhibiti kila kitu” tunafaa kuona kwamba kile ambacho Mungu anadhibiti si sehemu ya sayari, sehemu ya uumbaji, wala sehemu ya mwanadamu, lakini kila kitu: kuanzia kwa viumbe vile vikubwa hadi vile vidogovidogo, kuanzia kwa vile vinavyoonekana hadi visivyoonekana, kuanzia kwa nyota ulimwenguni hadi kwenye vitu vilivyo na uhai ulimwenguni, pamoja na viumbe vidogovidogo visivyoweza kuonekana kwa macho ya kawaida au viumbe vilivyo katika maumbo mengine. Huu ndio ufafanuzi hakika wa “kila kitu” ambacho Mungu “anadhibiti,” na ndio upana ambao Mungu anaonyesha ukuu Wake, urefu wa utawala na kanuni Yake.
Kabla ya binadamu hawa kujitokeza, viumbe vyote—sayari zote, nyota zote kule mbinguni—tayari vilikuwepo. Kwenye kiwango cha vitu vikubwa, vyombo hivi vya mbinguni vimekuwa vikizunguka mara kwa mara chini ya udhibiti wa Mungu, kwa uwepo wavyo wote, hata hivyo miaka mingi imepita. Ni sayari gani inaenda wapi na wakati gani haswa; ni sayari gani inafanya kazi gani, na lini; ni sayari gani inazunguka katika mzingo gani, na ni lini inatoweka au inabadilishwa—vitu hivi vyote vinasonga mbele bila ya kosa lolote dogo. Nafasi za sayari na umbali kati yazo ni masuala yanayofuata ruwaza maalum, ni masuala ambayo yanaweza kufafanuliwa kwa data yenye uhakika; njia ambazo zinasafiria, kasi na ruwaza ya mizingo yao, nyakati ambapo zinapatikana kwenye nafasi mbalimbali zinaweza kufafanuliwa kwa hakika na kufafanuliwa kwa sheria maalum. Kwa miaka na mikaka sayari zimefuata sheria hizi na hazijawahi kupotoka hata chembe. Hakuna nguvu inaweza kubadilisha au kutatiza mizingo yazo au ruwaza zao ambazo zinafuata. Kwa sababu sheria maalum zinazotawala mzunguko wazo na data yenye uhakika inayozifafanua iliamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba, zinatii sheria hizi zenyewe, kulingana na ukuu na udhibiti wa Muumba. Kwenye kiwango cha mambo makubwamakubwa, si vigumu kwa binadamu kujua zaidi kuhusu ruwaza fulani, data fulani, pamoja na sheria au matukio fulani yasiyoeleweka au yasiyoelezeka. Ingawaje binadamu hawakubali kwamba Mungu yupo, haukubali hoja kwamba Muumba aliumba na anatawala kila kitu na zaidi ya yote hautambui uwepo wa mamlaka ya Muumba, wanasayansi wa kibinadamu, wanafalaki, nao wanafizikia wanachunguza na kugundua zaidi na zaidi kwamba uwepo wa kila kitu kwenye ulimwengu, na kanuni na ruwaza zinazoonyesha mzunguko wavyo, vinatawaliwa na kudhibitiwa na nishati nyeusi kubwa na isiyoonekana. Hoja hii inampa binadamu mshawasha wa kukubaliana na kutambua kwamba kunaye Mwenyezi aliye miongoni mwa ruwaza hizi za mzunguko, anayepangilia kila kitu. Nguvu zake si za kawaida, na ingawaje hakuna anayeweza kuona uso Wake wa kweli, Yeye hutawala na kudhibiti kila kitu kila dakika. Hakuna binadamu au nguvu zozote zile zinazoweza kuuzidi ukuu Wake. Huku binadamu akiwa amekabiliwa na hoja hii, lazima atambue kwamba sheria zinazotawala uwepo wa kila kitu haziwezi kudhibitiwa na binadamu, haziwezi kubadilishwa na yeyote; na wakati uo huo binadamu lazima akubali kwamba, binadamu hawezi kuelewa kikamilifu sheria hizi. Na hizi sheria hazitokei-kimaumbile lakini zinaamrishwa na Bwana na Mungu. Haya yote ni maonyesho na mamlaka ya Mungu yanayoonyesha kwamba mwanadamu anaweza kuelewa katika kiwango cha mambo makubwa.
Kujua zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni